Kwanini "Service charge" ya TANESCO ni tatizo linalohitaji utatuzi wa haraka!

Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
6,167
5,610
Kwanza kabisa kwa wale wanaotumia umeme wanajua kwamba tulikuwa na mfumo wa zamani ambao Tanesco walitembelea nyumba zetu na kufanya matengenezo na ukaguzi wa mambo mbalimbali ikiwamo mita za umeme. Sina hakika kama hichi ndio chanzo cha haya makato, lakini ni dhahania yangu kuwa ndizo "service" tulizolipia nyakati hizo.

Sasa ni nyakati mpya. Ukitaka LUKU unalipia, na umeme unaotumia pia unalipia. Sasa service charge ni za nini? Service ipi hasa ambayo unatozwa wakati mwingine mpaka 5000/= au zaidi kwa mwezi?

Hebu tulinganishe makato haya kuona tatizo hili jinsi lilivyo kubwa:
Ukiwa na akaunti ya kawaida benki unalipia kama 700/= kwa mwezi. Ukiwa na akaunti ya kampuni, unalipia kama 7000/= kwa mwezi. Ukiwa na LUKU unalipia kama 5000 kwa mwezi.

Nadhani hata neno LUKU halina maana hapa. Kwa sababu LUKU ni lipia kadri unavyotumia. Naomba niweke mifano miwili tu hai kuonyesha tatizo hili sio dogo kama wengi wanavyolichukulia:
Kuna watu wawili hawakuwepo nyumbani kwa miezi 6. Mmoja alinunua umeme wa elfu 60 na mwingine elfu 50. Wa elfu 60 alipata unit 0 na wa pili alipata unit zisizofika 10.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wanatumia umeme husika kwa miezi yote sita. Iko wapi hapo concept ya Lipia Kadri unavyotumia?

Lakini katika makato hayo kuna makato ya REA. Ni makato yenye lengo jema kabisa, kusaidia kupeleka umeme vijijini ili kusukuma maendeleo. Hivi tukiwa wakweli, watu wangapi vijijini wataweza kulipia 5000/= au zaidi kwa ajili ya "service charge"?

Kabla sijamalizia naomba kuelimishwa kwa nini umeme una makato mengi hivi ilhali ndiyo primer energy kwa maendeleo yetu? Kwanza bei ya umeme wenyewe kwa unit ni mkubwa sana (295/= kwa unit). Hapo bado kuna VAT (18%), EWURA (1%), REA (3%) na service charge (5000+/= @month).

Nadhani ni wakati wa kutuondolea haya makato. Mtu anayehitaji Tanesco service na ailipie kwa wakati huo atakapoihitaji. Haya makato ya kiujumla jumla tu yanaumiza sana wananchi. Niisihi serikali iliangalie hili kama moja ya mambo yanayorudisha nyuma sana maendeleo yetu. Umeme ni nishati muhimu sana na hivyo ni vyema ikaangaliwa kwa ukaribu kabisa ili kuleta mapinduzi ya kiteknolojia.
 
Nakubaliana na wewe. Dili za watu zinabadilishwa majina na kuitwa service charges na zote anawekewa mlaji!!!
Hakuna huruma!
 
TANESCO waliwahi kupeleka hati ya maombi ya kuongeza bei kwa muda ( Sikumbuki lilikuwa bunge la ngapi), wabunge walikuikubalia TANESCO kuongeza bei kwa makubaliano ya baada ya muda washushe. Nafikiri muda haujafika.

Binafsi umenikuna sana kwanza,huwa sipati jibu ya hizo tozo zitozwazo na TANESCO.

18% VAT haina tatizo inaeleweka
1% EWURA ya kazi gani? Kama ni kitengo kilianzishwa na serikali kwa nini serikali isiwajibike na vitengo vyake kwa hiyo 18%?
3% REA ili iweje,kama mtu unapanua biashara, mtaji si uwe wa kwako? Watumiaji kulipia umeme vijijini,kwani hao watu wa vijijini hawaliipii service line?

Service charge kwa siku hizi ni wizi mtupu.

Mabenki (baadhi) wana account zinazofanana na LUKU, kwa mfano Standard Chartred bank wanayoinaitwa HIFADHI current account- Pay as much as you consume", hii account haina charge yoyote ya mwezi( No single cent charged) wanakucharge tu pale unapotumia.

LUKU ni the same, walitakiwa watucharge tu pale tunapotumia plus 18% VAT hizo charges nyingine ni wizi mtupu!
 
Hili ni jipu gumu naamini kulitumbua ni kazi watu wamegeuza tanesco ulaji wao kabisa na hili jipu litatesa sana watanzania
 
Najua watu wengi wameandika kuhusu Tanesco na naomba kwa wasimamizi wa Jukwaa hili wauache uzi huu kama ulivyo ili wahusika (ambao nina hakika watausoma) wapate kujua kwa kina.

Kwanza kabisa kwa wale wanaotumia umeme wanajua kwamba tulikuwa na mfumo wa zamani ambao Tanesco walitembelea nyumba zetu na kufanya matengenezo na ukaguzi wa mambo mbalimbali ikiwamo mita za umeme. Sina hakika kama hichi ndio chanzo cha haya makato, lakini ni dhahania yangu kuwa ndizo "service" tulizolipia nyakati hizo.

Sasa ni nyakati mpya. Ukitaka LUKU unalipia, na umeme unaotumia pia unalipia. Sasa service charge ni za nini? Service ipi hasa ambayo unatozwa wakati mwingine mpaka 5000/= au zaidi kwa mwezi?

Hebu tulinganishe makato haya kuona tatizo hili jinsi lilivyo kubwa:
Ukiwa na akaunti ya kawaida benki unalipia kama 700/= kwa mwezi. Ukiwa na akaunti ya kampuni, unalipia kama 7000/= kwa mwezi. Ukiwa na LUKU unalipia kama 5000 kwa mwezi.

Nadhani hata neno LUKU halina maana hapa. Kwa sababu LUKU ni lipia kadri unavyotumia. Naomba niweke mifano miwili tu hai kuonyesha tatizo hili sio dogo kama wengi wanavyolichukulia:
Kuna watu wawili hawakuwepo nyumbani kwa miezi 6. Mmoja alinunua umeme wa elfu 60 na mwingine elfu 50. Wa elfu 60 alipata unit 0 na wa pili alipata unit zisizofika 10.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wanatumia umeme husika kwa miezi yote sita. Iko wapi hapo concept ya Lipia Kadri unavyotumia?

Lakini katika makato hayo kuna makato ya REA. Ni makato yenye lengo jema kabisa, kusaidia kupeleka umeme vijijini ili kusukuma maendeleo. Hivi tukiwa wakweli, watu wangapi vijijini wataweza kulipia 5000/= au zaidi kwa ajili ya "service charge"?

Kabla sijamalizia naomba kuelimishwa kwa nini umeme una makato mengi hivi ilhali ndiyo primer energy kwa maendeleo yetu? Kwanza bei ya umeme wenyewe kwa unit ni mkubwa sana (295/= kwa unit). Hapo bado kuna VAT (18%), EWURA (1%), REA (3%) na service charge (5000+/= @month).

Nadhani ni wakati wa kutuondolea haya makato. Mtu anayehitaji Tanesco service na ailipie kwa wakati huo atakapoihitaji. Haya makato ya kiujumla jumla tu yanaumiza sana wananchi. Niisihi serikali iliangalie hili kama moja ya mambo yanayorudisha nyuma sana maendeleo yetu. Umeme ni nishati muhimu sana na hivyo ni vyema ikaangaliwa kwa ukaribu kabisa ili kuleta mapinduzi ya kiteknolojia.
Najua watu wengi wameandika kuhusu Tanesco na naomba kwa wasimamizi wa Jukwaa hili wauache uzi huu kama ulivyo ili wahusika (ambao nina hakika watausoma) wapate kujua kwa kina.

Kwanza kabisa kwa wale wanaotumia umeme wanajua kwamba tulikuwa na mfumo wa zamani ambao Tanesco walitembelea nyumba zetu na kufanya matengenezo na ukaguzi wa mambo mbalimbali ikiwamo mita za umeme. Sina hakika kama hichi ndio chanzo cha haya makato, lakini ni dhahania yangu kuwa ndizo "service" tulizolipia nyakati hizo.

Sasa ni nyakati mpya. Ukitaka LUKU unalipia, na umeme unaotumia pia unalipia. Sasa service charge ni za nini? Service ipi hasa ambayo unatozwa wakati mwingine mpaka 5000/= au zaidi kwa mwezi?

Hebu tulinganishe makato haya kuona tatizo hili jinsi lilivyo kubwa:
Ukiwa na akaunti ya kawaida benki unalipia kama 700/= kwa mwezi. Ukiwa na akaunti ya kampuni, unalipia kama 7000/= kwa mwezi. Ukiwa na LUKU unalipia kama 5000 kwa mwezi.

Nadhani hata neno LUKU halina maana hapa. Kwa sababu LUKU ni lipia kadri unavyotumia. Naomba niweke mifano miwili tu hai kuonyesha tatizo hili sio dogo kama wengi wanavyolichukulia:
Kuna watu wawili hawakuwepo nyumbani kwa miezi 6. Mmoja alinunua umeme wa elfu 60 na mwingine elfu 50. Wa elfu 60 alipata unit 0 na wa pili alipata unit zisizofika 10.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wanatumia umeme husika kwa miezi yote sita. Iko wapi hapo concept ya Lipia Kadri unavyotumia?

Lakini katika makato hayo kuna makato ya REA. Ni makato yenye lengo jema kabisa, kusaidia kupeleka umeme vijijini ili kusukuma maendeleo. Hivi tukiwa wakweli, watu wangapi vijijini wataweza kulipia 5000/= au zaidi kwa ajili ya "service charge"?

Kabla sijamalizia naomba kuelimishwa kwa nini umeme una makato mengi hivi ilhali ndiyo primer energy kwa maendeleo yetu? Kwanza bei ya umeme wenyewe kwa unit ni mkubwa sana (295/= kwa unit). Hapo bado kuna VAT (18%), EWURA (1%), REA (3%) na service charge (5000+/= @month).

Nadhani ni wakati wa kutuondolea haya makato. Mtu anayehitaji Tanesco service na ailipie kwa wakati huo atakapoihitaji. Haya makato ya kiujumla jumla tu yanaumiza sana wananchi. Niisihi serikali iliangalie hili kama moja ya mambo yanayorudisha nyuma sana maendeleo yetu. Umeme ni nishati muhimu sana na hivyo ni vyema ikaangaliwa kwa ukaribu kabisa ili kuleta mapinduzi ya kiteknolojia.
 
Really terrible, tunanyonywa mpaka tumezoea! Kwa hakika inahitajika waondoe vijigharama fichama hivi ambavyo wanyonge ambao makato haya ni regressive wanaumia sana.

Ni wakati sasa watambue kwamba wananchi wanafahamu haya mambo. Na hizi gharama za kificho zikipungua watu watanunua umeme, hakutakuwa na mtu anaiba umeme, watu wataipenda kampuni hii ya umma, wakisikia transformer inataka kuhujumiwa watashiriki kuokoa hasara, LAKINI ni mpaka hawa na TRA watambue kwamba kila pande iwe na haki pamoja na kutimiza wajibu...
 
Kote huko tuna kata kata Kona mkombozi wa kwanza ni kufanyiwa Kazi Kwa maazimio yote ya kashfa ya Escrow kwenye bunge la kumi,kwani Tanesco ime bebeshwa mizigo mizito sana.kuhusu kuondoa makato ya REA na EWURA hayo yali pitishwa na bunge letu Kwa sasa ni sheria ya nchi hivyo tutumie wawakilishi wetu kuomba zitolewe
 
Ni kweli ni unyonyaji sana lakin siku hzi tanesco wamepunguza gharama kwa watu wanaotumia chini ya unit 75 per month unatolewa service charge ewura na rea na unit moja unanunua 150 per month nenden mchekiwe kwenye system issue ni nyumba za kupanga matumiz huwa makubwa sana kuliko mwenye nyumba yake
 
Bei ya mita iko juu sana, ndio maana unalipa kidogokidogo
mnufaika wa service charge. kwa hiyo tanesco hawataki kutumia pesa yao kuwekeza? kuna siku tutalipia ndizi zifuatwe bukoba ili tuuziwe tena. wamebakiza kupiga mashine tu. ila kila baya limefanyika.
 
Bei ya mita iko juu sana, ndio maana unalipa kidogokidogo
Unamaanisha kwa vile bei ya basi ni kubwa sana,wamiliki wa mabasi wanavyotaka kununua basi jingine waweke tozo mfichamo kwenye bei ya nauli?
Hivi kwenye basi kuna service charge?
Bei ya unit inatosha pamoja na VAT, tozo zingine wabunge wapitie upya. Masuala ya Ndioooooooooo ndo yanatusumbua kwa sasa.
 
Jamani,

Ni kweli "Service Charge" ya Tanesco ni sawa na wizi! "Service" ipi, kama inayofanywa na Mekanika kwenye Gari kwa kumwaga Oil, kucheki vitu vingine, kubadilisha "Filter" n.k. Sasa hawa Tanesco, wanafanya "Service" ipi? Kama Mteja ananunua Umeme, kwa Bei iliyopangwa na Tanesco, ambayo maana yake siyo Bei ya Hasara ila ni ya kibiashara ikimaanisha kuna Faida ndani yake, sasa wanapotaka kufanya "Service" yoyote, si watumie fedha tunazolipia huduma/biashara ya Umeme? Kuwekewa Mashine ya LUKU tumelipia, kuwekewa "Service Line" tumelipia. Umeme tunalipia, sasa Tozo ya "Service" ya nini? Pia kwa nini mnatukata vitu kama REA na EWURA? Sisi kwa nini tunatozwa ushuru huo huku tunakatwa VAT ya Asiliamia 18% na Serikali? Kama Serikali ina nia njema, kama inavyoonyesha, ya kuwapatia Umeme Wananchi wa Vijijini, kwa nini isitumie "resources" zake inazozipata kupitia Kodi ya VAT? Kama imeanzisha Mamlaka ya EWURA, kwa nini tuigharimie sisi wateja wa Umeme? Kwa nini?
Serikali hii lazima iondoe hivi vikodi vyenye kero, vinavyoongeza gharama kwa mlaji wa mwisho, ambaye kwa kawaida ni Mtu masikini tu?

Bwassa.
 
Hi sevice charge wanadai kama vile mtaani kwenu umeme umekatika kwa shoti basi vile wakija kutengeneza ndiobwanajiect kama ni sevice chargi ni dhulma tu
 
Najua watu wengi wameandika kuhusu Tanesco na naomba kwa wasimamizi wa Jukwaa hili wauache uzi huu kama ulivyo ili wahusika (ambao nina hakika watausoma) wapate kujua kwa kina.

Kwanza kabisa kwa wale wanaotumia umeme wanajua kwamba tulikuwa na mfumo wa zamani ambao Tanesco walitembelea nyumba zetu na kufanya matengenezo na ukaguzi wa mambo mbalimbali ikiwamo mita za umeme. Sina hakika kama hichi ndio chanzo cha haya makato, lakini ni dhahania yangu kuwa ndizo "service" tulizolipia nyakati hizo.

Sasa ni nyakati mpya. Ukitaka LUKU unalipia, na umeme unaotumia pia unalipia. Sasa service charge ni za nini? Service ipi hasa ambayo unatozwa wakati mwingine mpaka 5000/= au zaidi kwa mwezi?

Hebu tulinganishe makato haya kuona tatizo hili jinsi lilivyo kubwa:
Ukiwa na akaunti ya kawaida benki unalipia kama 700/= kwa mwezi. Ukiwa na akaunti ya kampuni, unalipia kama 7000/= kwa mwezi. Ukiwa na LUKU unalipia kama 5000 kwa mwezi.

Nadhani hata neno LUKU halina maana hapa. Kwa sababu LUKU ni lipia kadri unavyotumia. Naomba niweke mifano miwili tu hai kuonyesha tatizo hili sio dogo kama wengi wanavyolichukulia:
Kuna watu wawili hawakuwepo nyumbani kwa miezi 6. Mmoja alinunua umeme wa elfu 60 na mwingine elfu 50. Wa elfu 60 alipata unit 0 na wa pili alipata unit zisizofika 10.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wanatumia umeme husika kwa miezi yote sita. Iko wapi hapo concept ya Lipia Kadri unavyotumia?

Lakini katika makato hayo kuna makato ya REA. Ni makato yenye lengo jema kabisa, kusaidia kupeleka umeme vijijini ili kusukuma maendeleo. Hivi tukiwa wakweli, watu wangapi vijijini wataweza kulipia 5000/= au zaidi kwa ajili ya "service charge"?

Kabla sijamalizia naomba kuelimishwa kwa nini umeme una makato mengi hivi ilhali ndiyo primer energy kwa maendeleo yetu? Kwanza bei ya umeme wenyewe kwa unit ni mkubwa sana (295/= kwa unit). Hapo bado kuna VAT (18%), EWURA (1%), REA (3%) na service charge (5000+/= @month).

Nadhani ni wakati wa kutuondolea haya makato. Mtu anayehitaji Tanesco service na ailipie kwa wakati huo atakapoihitaji. Haya makato ya kiujumla jumla tu yanaumiza sana wananchi. Niisihi serikali iliangalie hili kama moja ya mambo yanayorudisha nyuma sana maendeleo yetu. Umeme ni nishati muhimu sana na hivyo ni vyema ikaangaliwa kwa ukaribu kabisa ili kuleta mapinduzi ya kiteknolojia.
Kwanza naomba usipotezwe na maneno ''service charge'' ufikirie ni gharama ya Tanesco kuja nyumbani kwako kufanya service. Hizi fedha zinatozwa kwa sababu ya gharama za ku-mantain zile line za umeme kutoka kwenye source ya umeme mpaka pale nyumbani kwako. Kwa kifupi ni gharama za ku-transmit umeme kutoka from the source to the end point. Ni kama unavyoagiza pizza ukiwa nyumbani... inabidi ulipe gharama ya pizza na gharama ya kuletewa. Na hii service charge ipo sehemu nyingi duniani. Mara yangu ya kwanza kuishi nchi moja Europe nilichukua likizo ya miezi mitatu. Niliporudi nilikuta bill ya umeme inanisubiri (tulikuwa tunalipa bill kila baada ya miezi mitatu). Ilikuwa ni bill ya kipindi kile ambacho sikuwepo. Nikaenda kuulizia vipi nichajiwe umeme ambao sijatumia? Jibu nililopata ni ''hizi ni gharama za service! Yaani utumie umeme au usitumia, lakini kama umeingia contract ya kununua umeme wao ni laizima kuna basic cost ambayo utalipa plus gharama ya umeme. Labda uniambia kuwa hizo gharama za service ni kubwa sana Tanzania nitakubali...
 
Wanatakiwa wabuni jinsi ya kuongeza kipato siyo kuwaibia wananchi. Hili ndio tatizo la kuwa na kampuni moja ya umeme (Monopolies) na sithani kama regulator wananguvu za kutetea wananchi. Nchi kama UK wana regulator OFGEM ambaye anahakikisha fair price na fine pale umeme unapokatika katika bila sababu za msingi.
 
Back
Top Bottom