GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 4,023
- 5,412
Tanesco wameendelea kujihakikishia nafasi ya kwanza ya ubabaishaji uliopitiliza kwa kuendeleza mgao unaoendelea kimya kimya pamoja na kutoa ahadi lukuki zenye matumaini ya kitume kuwa sasa wamejipanga kufuta kabisa kero za umeme hapa nchini.Tanesco mkubali tu kuwa hamna uwezo wala mbinu ya kumaliza tatizo la umeme hapa nchini na hasa hapa Dar,Haiwezekani wateja wanaolipia umeme kwa wakati pamoja na charge zote mlizoweka,wakaambulia kutumia umeme kidogo kwa kuwa muda mwingi mnakata umeme.Huu ni wizi wa mchana, nyie mnachukua chenu mapema lakini huduma hamtoi kwa visingizio vya kuboresha mitambo eti imekuwa chakavu.Naona kuna ukosefu wa watu waliosomea mambo ya huduma hii na pengine hakuna watu weredi katika shirika hilo zaidi ya vishoka na wababaishaji.Mnastahili kutumbuliwa kwa kweli.