Tanesco na ukiritimba wa luku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco na ukiritimba wa luku

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ami, Sep 8, 2010.

 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesema kuna ongezeko la vituo bandia vya kuuzia Luku, vinavyochangia wizi wa umeme unaozalishwa na shirika hilo.

  Hayo yalisema juzi na Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Alisema kutokana na tatizo hilo, Tanesco ipo katika mchakato wa kusaka wahusika, kupitia oparesheni maalum kabla ya kuchukua hatua za kisheria.

  Alisema ingawa kuna vituo vingi vilivyowekwa na Tanesco kwa ajili ya kuuza luku, mapato yake ni kidogo kutokana na kuwepo vituo bandia.

  Alisema kuwa wanaamini katika oparesheni inayofanywa sehemu tofauti hapa nchini ndio itakayowasaidia kuwabaini wezi hao.

  "Tunaamini kuwa hii oparesheni ya kusaka wezi tunayofanya sehemu tofauti lazima itatusaidia kuwabaini wezi na kama wanatoka ndani ya Tanesco itajulikana, na hatutawaonea aibu, hatua za kisheria zitachukua mkondo wake,"alisema.

  Pia alisema Tanesco inaendelea kuwadhibiti watu wanaojiunganishia umeme kwa njia zisizo halali, hivyo sehemu ya wezi wa nishati hiyo.

  Alisema vitendo hivyo vinafanyika zaidi nyakati za usiku, na wengine wanaharibu luku kwa lengo la kupunguza matumizi yake.

  Masoud alisema tatizo jingine linaloikabili Tanesco ni kuwepo kwa wezi wa umeme wanaojiongezea `unit' tofauti na zinazotambuliwa na shirika hilo. Alisema mbali na hasara zinazotokana na uunganishwaji holela wa umeme, matumizi ya njia zisizo halali hususani kujiunganishia umeme kinyume cha taratibu, kunaweza kuhatarisha maisha yao.

  Hata hivyo Masoud alisema kwa sasa wako katika mchakato wa kufunga luku mpya kwa wateja wote, ili kupunguza tatizo la matumizi mabovu ya umeme.

  Alisema utekelezaji wa mpango utakamilkika Desemba, mwaka huu. Mhandisi Mkuu wa Tanesco, Benedict Bahati na Mhandisi wa umeme, Adolfu Kigombola, walisema kwa nyakati tofauti kuwa mpango wa kukamata wezi wa umeme, unaendelea na wanafanya mahojiano na baadhi ya watuhumiwa wa wizi huo.

  Baadhi ya mita ambazo zimekatwa ni pamoja zenye namba 0134368220 7, 0134368217 3, 0134313707, 9,01343137087 kutoka katika mtaa wa makutano ya Kariakoo na Congo.

  Mita nyingine ni zenye namba 0134005031 7,0131984498 9 na 01341564548 kutoka katika maeneo ya biashara Mwenge.


  Source: IPP MEDIA.

  Siamini kwamba kuna hilo tatizo. Isipokuwa tatizo ni hilo la kuteteta maslahi ya watu waliopewa uagentina tanesco.Hivi vituo vinavyoweza kuitwa bandia ni vile vya kutumia m-pesa na zap.


  Hakuna mwenye teknolojia ya kutoa token za luku bila kupitia hao.Hawa wana makubaliano na tanesco sasa vipi watumiaji wake waitwe ni bandia.

  Huu ni ukiritimba tu wa kuyarudisha maisha yawe magumu na kila kitu kiwe cha foleni.
   
Loading...