TANESCO na mwendelezo wa siasa za mgao wa umeme.

aggrey kimambo

Senior Member
Aug 10, 2015
129
142
Maajabu hayaniishi katika hili bado, TANESCO watoke hadharani waseme mgao wa umeme hausababishwagi na upungufu wa maji kwenye mabwawa yanayozalisha umeme, bali ni vitu vingine. Na wavitaje hivyo visababishi vingine maana imeshajidhihirisha siyo upungufu wa maji. Maana mvua zote hizi mpaka za mafuriko tulitegemea kusiwe na mgao hata kidogo wa umeme.

Kwamfano huku moshi leo umeme upo, kesho haupo siku nzima,(na ni continious circle)hili swala linatuathiri sisi wafanyabiashara wadogo tunaotegemea umeme kama mainbody ya biashara. Tanesco acheni figisu figisu bhana, TRA wanakomaa wanatufungia maduka, bidhaa hazinunuliki, pesa imekuwa ngumu na TANESCO nao wanaleta figisu.

Huo utumbuaji wa majipu uwe na faida kwetu sisi wananchi wa kawaida kwenye kufanya Urahisi wa maisha, kama utumbuaji huo unaendana na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu kwetu, TUTACHOKA.

TANZANIA NCHI YA KUFIKIRIKA.
 
Miaka mitano itaisha na serikali haitakuwa imefanya lolote kupunguza makali ya maisha kwa mwananchi wa kawaida. Mwanzo mgumu hakuna asiyejua hilo cha muhimu inahitajika mikakati endelevu wananchi wajue, tunatoka wapi tunaenda wapi. Kutumbua majipu kukishaisha nini kitafuata.
 
....tafuta namba zao wapigie simu uwaulize,mbona kama unawaogopa?!,hiyo huduma km unailipia kuipata ni haki yako,kama namba zao huna,nenda kwenye ofisi zao.
 
Availability of power depends on number of other factors apart from its generation. Once power is generated is transmitted through transmission lines for a long distances. Transmission lines are exposed to so many risk , i.e sabotages by unfaithful people, natural disasters, and natural depreciation of the infrastructures. Routine maintenance and preventive maintenance are all important operations which lead to power backouts
 
Back
Top Bottom