Tanesco msitufanyie usanii kwa lengo la kutuhadaa Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco msitufanyie usanii kwa lengo la kutuhadaa Watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Aug 18, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tanesco inaelekea wanataka kutuhadaa -- wanajaribu sasa kuonyesaha kuwa kwa kiasi kikubwa matatizo yao ya kifedha yanatokana na madeni waliyolimbikiza wateja hali kadhalikawezi wa umeme.

  Hilo sikatai lakini ni ukweli usiopingika kwamba matatizo yao makubwa yanatokana na ufisadi dhidi ya shirika hilo uliokuwa ukifanywa, na unaoendelea kufanywa na maafisa wa shirika hilo wakishirikiana na vigogo wa serikali.

  Kikubwa hapa ni ule mtindo wa kuyapa makampuni binafsi kuweka mitambo, kufua umeme na kuiuzia Tanesco kwa mikataba kandamizi sana hadi kufikia kwamba Tanesco sasa hivi inayalipa makampuni hayo zaidi ya Sh bilioni 42 kwa mwezi.

  Hebu fikiria iwapo badala yake, serikali ingekuwa imeiwezesha Tanesco kwa kuipatia mitambo hiyo, isingekuwa inalipa fedha hizo.

  Mtindo huu, kwa kisingizio cha kupata umeme wa dharura ni 'brainchild' ya Jk tangu akiwa waziri wa nishati wakati wa awamu ya Msee Ruksa pale walipoleta IPTL iliyoanza kuinyonga Tanesco, na kuna kesi mahakamani kati ya IPTL na Tanesco/serikali hadi leo haijaisha.

  Miaka 10 ya Mkapa hakukuwekwa kampuni yoyote ya kufua umeme wa aina hii, lakini alipoingia JK tu, makampuni hayo yakaanza kuja kama nyuki -- kuanzia Richmond, hadi sasa yako zaidi ya 10 yanayoinyonya Tanesco ile mbaya.

  Eti sasa Tanesco inataka/inajaribu kuonyesha kwamba matatizo yao ya kifedha ni kutokana na madeni na wezi wa umeme.

  Mimi naona hiyo ni janja tu, wanataka kuficha ufisadi mkubwa unaofanyika, kila mwezi viongozi wa serikali wananufaika na mabilioni kutoka makampuni hayo yanayoiuzia Tanesco umeme.

  Nawasilisha hoja.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hayo usemayo. Hayo madeni yametokana na ufisadi na uzembe wa wao wenyewe Tanesco. Mafundi wa Tanesco wanapoenda kukta umeme kwa wadaiwa sugu, hawakati -- hupewa rushwa na kuondoka. Pengine serikali inaingilia kati kwa kisingizio eti taasisi inayotakiwa kukatwa umeme ni nyeti, huku wanapewa bajeti kila mwaka.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Madeni ya Mashirika na watu binafsi yanachangia almost 20% ya hasara kwa Tanesco. Zinazobaki zote ni Ulaji wa watu!
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Washagundua kuwa ni rahisi kuwadanganya watz so wanachofanya ni kucapitalize kwenye weakness hiyo!!!!
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndo maana namuona yule dada Badra akionyesha ukali kuhusu wezi -- huku akijua wazi makampuni hayo ya ukamuaji yananyonya mabilioni kila mwezi. Ajue kwamba si Watz wote wanweza kuhadaika.

  Halafu nashangaa Ewura, inayotakiwa kutetea wananchi, inatetea/inaficha madhambi ya Tanesco/serikali, kwa kila mara kukubali kupandisha bei ya umeme, kufidia hasara inayotokana na ufisadi.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani matatizo ya kifedha ya Tanesco yanatokana na: makampuni ya ufuaji umeme wa 'dharura' + mafundi wa Tanesco ambao ni wala rushwa + madeni ya wateja + wezi wa umeme. Kwa mpangilio huo.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi network solution alifanya kazi gani na wakati gani? TANESCO ni mahala pema pa kupitia.
   
Loading...