kuna taasisi mbili za ajabu sana mkoa wa morogoro na ninawasiwasi na mishahara wanayolipwa sijui ni kwasababu ipi
1. TANESCO. Tanesco ni kinara wa kukata umeme kila ifikapo mda wa saa kumi na mbili jioni mfululizo, kuanzia mda huo hadi saa sita usiku yaani ni kukata umeme na kurudisha hilo zoezi linajirudia mara kwa mara alafu ni kila siku. Saizi inaanza wiki ya pili sasa tangu waanze huo ujinga wao. Wamekuwa wakituharibia sana vitu vya thamani vinavyotumia umeme....imekuwa kero sana kila giza linapoanza kuingia hukata kata umeme mara kwa mara utadhani kwenye mitambo kuna wanafunzi wa field ambao wanajaribu kubonyeza kila kitu kuona nini kinatokea. Sasa wanatutia hasara....popote mlipo hiyo biashara kama inawalipa tangazeni kama kuanzia mida hiyo umeme sio wa uhakika hadi asubuhi kunapokucha
2. JESHI LA POLICE; linatumia nguvu kubwa sana kufukuzana na vijana barabarani...lakini hawawasaidii sana badala yake ni kama inajengwa uadui. Watoto hawana elimu wamenunuliwa boda wajikwamue kimaisha ..wewe trafic uliyesoma unavaa sare za kawaida na kuwafatilia vijana hadi nyumbani wanakoishi na kuwakamata huo ni utoto. Kumekuwa na wimbi la askari usalama kutokuvaa sare za kazi, inapotokea boda hajavaa kofia akapita mbele yake hao askari hujibeba na boda boda yao na kuanza kumfuata kwa nyuma taratibu...kijana anaposimama afanye kazi zake hapohapo wanamkamata...aisee waelimisheni kwanza acheni hizo roho...hao watu wakirudi mtaani wanaumiza wananchi ndio wanageuka waporaji, wabakaji nk
Jeshi unaanzisha semina za kuwafundisha madereva wote, unatumia wiki nzima, mnajilipa posho, mmekodi ukumbi wa bei kubwa..mnazunguka kutafuta vijana wa kuwafundisha....kumbe ni kamradi kenu mmeandaa vyeti vya bodaboda (elfu 50 sijui) na wale wa magari (100,000+_ kwa gharama mbili tofauti...sasa mnasaidia nini au mnafanya biashara kama wafanyabiashara wengine mitaani??. si mngewashauri waende veta mwezi mmoja wapata vyeti na leseni baadae.....
Hili la hawa jamaa bado linatia mashaka sana; pia mbona ujambazi wa kupora fedha watu unatokea karibu na kituo cha police tena mda wa saa kumi na mbili kweupe...mnashindwa kuwapata majambazi wanaotumia pikipiki kwelii kabisa?, kazi yenu ni ipi? msikie wananchi wameua mwizi nanyi muende mkabebe maiti? ndio kazi yenu kuu hiyo? (wanapora maduka ya jumla matatu na wanafanikiwa kutoweka hadi leo siku ya tatu kimyaa kwelii?)
Jeshi lijipambanue, usalama wa raia bado upo hatiani sana. Hata hao wafanyabiashara saizi wanafanya biashara roho zao zipo juu juu sana...mchana wanawaza kuvamiwa na usiku wanawaza kuvunjiwa.
Nilichokiona kwenu jeshi la police; mkipata taarifa huwa mnatoka kwa kujivuta alafu mnakimbiza gari baadae mnaanza kurudi kama kinyonga mnatumbua macho mkiwa mmekaa kwenye mabomba. Aisee wasaidieni wananchi kupata amani katika shughuri zao