TANESCO: Mgawo wa Umeme kila siku

TANESCO: Mgawo wa Umeme kila siku

maeneo yote ya jiji mchana huu umeme unawaka kama kawauda tena uko stable kwa wateja wa matumiz yote makubwa ya kati na madogo kasoro yale machache ambayo matengenezo na ukarabati wa muda mfupi kwa lengo la kuboresha huduma unaendelea
Ukarabati gani unaochukua miaka na miaka bila kuisha?
 
Jamani jaribu ni kuwa serious kidogo.Tanesco haijawahi kutangaza mgawo wa umeme na eneo kubwa umeme upo kama kawaida.msiwe wavivu wa kufuatilia vyombo vya habari.sehemu ambazo hamna umeme Tanesco wametangaza kuwa kuna matengenezo ya kuboresha miundombinu ili hali ya upatikanaji umeme uimarike.lets be positive about Tanesco.
 
We acha tu huku leo sijui ni mtu anacheza na switch toka asubuhi! Ni zima washa zima washa

Halafu wakituunguzia vitu hawana habari! Sijui kwanini tanesko wana roho mbaya namna hii
Ki ukweli kabisa mi nimeona nijiunge tu na Mobisol, na laity ningepata na alternative ya kuwasha na fridge nadhani Tanesco ningeachana nao kabisa, wana kela zaidi ya sana.
 
Jamani Valentina usemavyo kuwa kunamtu anacheza na switch siyo kweli bali nimatengenezo yanendelea please tujaribu kuwa wapole mambo yatakuwa mazuri tu jamani hiki ni kipindi cha mpito
 
TANESCO wanamhujumu Dr Magufuli asichaguliwe kwa kishindo haa haaa kumbe uchaguzi umeshapita sasa nani anahujumuwa ?.
 
Tanesco haiwezi kumhujumu anko Magu hata ck moja . Acha kupotosha umma na propaganda zako zilopitwa na wakati.Tanesco inafanya kazi kiufundi zaidi ili huduma iwe bora na ya u hakika . Na kwanza ahujumiwe ili iweje? Jipange dogo urudi kivingine. Tanesco tunasema hapa kazi tuu
 
Jamani Valentina usemavyo kuwa kunamtu anacheza na switch siyo kweli bali nimatengenezo yanendelea please tujaribu kuwa wapole mambo yatakuwa mazuri tu jamani hiki ni kipindi cha mpito
Matengenezo gani kwa stayle hii ya zima washa zima washa kila baada ya dk10?
 
Yani utadhani tunapewa bure umeme wenyewe....
Sometimes hua najiulizaga hivi; nimenunua umeme kwa prepaid (LUKU) nikiamini nitakua na umeme wa kunitoshereza say for 1 month and hence bajeti ya mafuta ya taa au mishumaa sitakua nayo na sina sababu ya kutafuta betri kwa ajili ya ka redio kangu kakichina so nitasikiliza muziki na pia Television so pia sina sababuya kua na mafuta kwenye generator, simu yangu pia yaweza isipate shida ya chaji hasa kama nipo nyumbani. Tanesco wanapo kata umeme ili hali pesa zangu wanazo na wnazitumia au wameisha zitumia, JE zile gharama ninazo ziingia kutafuta nishati mbadala hakuna namna ya wao kunifidia? Au haiwezekani tukatunga sharia ya kua tunawashitaki Tanesco kwa kutuharibia bajeti ya vitu ambavyo hatukua na mpango wa kuvinunua? Achilia mbali huo uunguzaji wa vyomba vya umeme ambao hua unatokea kila inapotekea either power cut au power fluctuation!
 
Hii ni wiki ya pili sasa,TANESCO wamekuwa wakikata umeme asubuhi saa mbili na kurudisha saa mbili usiku.Maeneo mengi ya Jiji na vitongoji vyake yamekuwa yakikatiwa umeme na kupata umeme wa mgao kila siku.Hali hii inatokea bila TANESCO na msemaji wake wa Wizara BADRA MASOUD kutuambianlolote sisi wateja na walipa kodi wa Tanzania.

Mgao unaoendelea ni wa kisirisiri?Ni kwanini Tanesco na wizara husika isitutangazie kuwa kuna mgao wa umeme unaoendelea hapa nchini?Kama leo toka saa mbili asubuhi umeme umekatwa,na TANESCO haijatoa anagalizo

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Mh.George Simbachawene,mwaka jana wakati analihutubia bunge alismea tatizo la umeme litakuwa historia kwa kuanzia na Jiji la Dsm...mbele ya Bunge Simbachawene alisema ifikapo 14/09/2015 mgao wa umeme utakuwa historia,kwani mitambo ya gas toka Mtwara kuja Kinyerezi itakuwa imekamilika,lkn mpaka sasa bado tunaelea katika dimbwi la mgao na umeme wa shida,Jamani kwani hiyo mitambo ya Gas Kinyerezi inasubiri nini??Biashara zetu zinakosa muelekeo kwa kukosa umeme wa uhakika
Mkuu si wewe tu imebidi tuingie gharama ambazo hazituhusu za kununua power bank si kwa kupenda. Simu ndo dili ikizima unakosa madili mbalimbali. Hii nchi basi tu kwa sasa nafarijika tu na uwepo wa Magufuri.

Huku Kanda ya Ziwa kila Jumapili lazima ukatwe kutwa nzima. Walitangaza ni matengenezo makubwa kwa muda wa mwezi mzima. Cha ajabu tangu asubuhi waliukata wakati ni Jumamosi.
 
Sometimes hua najiulizaga hivi; nimenunua umeme kwa prepaid (LUKU) nikiamini nitakua na umeme wa kunitoshereza say for 1 month and hence bajeti ya mafuta ya taa au mishumaa sitakua nayo na sina sababu ya kutafuta betri kwa ajili ya ka redio kangu kakichina so nitasikiliza muziki na pia Television so pia sina sababuya kua na mafuta kwenye generator, simu yangu pia yaweza isipate shida ya chaji hasa kama nipo nyumbani. Tanesco wanapo kata umeme ili hali pesa zangu wanazo na wnazitumia au wameisha zitumia, JE zile gharama ninazo ziingia kutafuta nishati mbadala hakuna namna ya wao kunifidia? Au haiwezekani tukatunga sharia ya kua tunawashitaki Tanesco kwa kutuharibia bajeti ya vitu ambavyo hatukua na mpango wa kuvinunua? Achilia mbali huo uunguzaji wa vyomba vya umeme ambao hua unatokea kila inapotekea either power cut au power fluctuation!
Hivi kama wamelemewa kwanini wasiruhusu makampuni mengine kutupatia huduma ya umeme?

Wangekua na washindani wangeshika adabu
 
marekebisho ya miundombinu ya umeme sio jambo dogo la kumalizika kwa usiku mmoja.
Yakiisha eneo moja yanahamia eneo Lingine mpaka pale mifumo yote ya usafirishaji na usambazaji ambayo mingi ni ya muda mrefu itakapokaa sawa.
Pia ukumbuke kuwa Tanzania ndio nchi yenye line ndefu kuliko nchi zote Africa mashark na ya kati Ambapo mpaka dec mwaka jana kulikuwa na kilomita zaidi ya 67,000 za line za usambazaji nchi nzima sawa na karibu mara 75 ya umbali wa safari ya kutoka dar mpaka mwanza, safari ambayo huwa inaanza saa12 asubuhi unafika saa5 usiku. line za usafirishaji zenye urefu wa km 5,000 zenye kusafirisha umeme wenye ukubwa tofaut tofaut karibu ya 120 mpaka 400kv na bado tunavyongea hapa mafundi wako site wanajenga zingine mpya na kukarabat zilizopo halafu leo hii unataka matengenezo yote hayo yakamilike kwa usiku mmoja itawezekanaje hapo ndugu????????????????????

Natumaini kwa maelezo hayo angalau umepata elimu ya kwanini matengenezo haya yanachukua muda na yanahitaji uvumilivu mwsho wa siku hali ikae sawa.
 
Hivi vilio vitaisha siku wakiachilia utengenezaji na usambazaji wa umeme kuwa biashara huria. TTCL walitunyanyasa hivi hivi enzi hizo, ona hatua tuliyopiga leo baada ya kuruhusu wawekezaji.

Siamini kama hatuwezi kuwa na makampuni mengine makubwa ya kuzalisha na kusambaza umeme yatakayoshindana na hawa jamaa maana kila siku kuna hadithi mpya na hakuna matumaini. Kwa kweli TANESCO wanatufanya kuchukia kuzaliwa Tanzania.

Leo utaambiwa kuna matengenezo makubwa vuteni subira, kesho utaambiwa mitambo ya umeme wa gesi inawashwa kwa awamu, kesho utaambiwa mtambo mmoja wa umeme wa gesi unawashwa kidogo kwanza ili kuona namna unavyofanya kazi ili kuzuia usiharibike, siku nyingine kina cha maji kwenye mabwawa kimepungua, mara hatujui sababu za Gridi kuu ya taifa kuzimika ghafla, blaaa..... blaaa..... blaaa! Mimi sina imani na TANESCO!!
 
Jamani jaribu ni kuwa serious kidogo.Tanesco haijawahi kutangaza mgawo wa umeme na eneo kubwa umeme upo kama kawaida.msiwe wavivu wa kufuatilia vyombo vya habari.sehemu ambazo hamna umeme Tanesco wametangaza kuwa kuna matengenezo ya kuboresha miundombinu ili hali ya upatikanaji umeme uimarike.lets be positive about Tanesco.

Ni kweli ilitangazwa na mikoa inayoathirika na ukataji huu wa umeme ni yote ya kanda ya kati, Kaskazini, magharibi (isipokuwa Kigoma) na ile ya kanda ya Ziwa
Victoria yote kwa siku za j'mosi leo na kesho j'pili kuanzia saa 2:00asb - 11:00 jioni.

Tatizo ni moja kuwa TANESCO sio wakweli, ni waongo kupindukia. Kukata wanakata umeme ndani ya muda waliotaja au hata kuwahi kabla ya muda huo lakini kurejesha umeme ni mbinde. Mfano leo huku maeneo ya Shinyanga mmerejesha umeme saa 12:30 jioni nje ya muda mliosema!!

Hata huu uliorejeshwa mnakata na kuwasha kila baada ya dakika kadhaa. Mfano muda ninapo posti hii post yangu umekatika zaidi ya mara tano ndani ya masaa mawili tangu mturejeshee!!

Hili ni jambo la kawaida kweli hili!!!??

Na lazima muelewe kuwa sisi watanzania ni waelewa sana na tunajua kuna kitu kinachoitwa matatizo ya kiufundi ya hapa na pale, lakini sasa ndiyo hivi kweli!!??

Hapana, TANESCO ni jipu tena baya linalonuka na kuoza. Sijui ni kwa nini huyu mtumbua majipu halioni? Je, ana maslahi nalo labda??.......NO WAY TUNATAKA IMMEDIATE SOLUTION YA HII KITU, tumechoka na ngonjera zenu hizi!!

Lazima wakubali kuwa imefika wakati mpaka hawana hata uhakika ni wakati gani umeme utakuwepo!!
 
Ni wapi huko unapokatika ovyo. Wengine tumesahau lini umeme ulikatwa.
 
marekebisho ya miundombinu ya umeme sio jambo dogo la kumalizika kwa usiku mmoja.
Yakiisha eneo moja yanahamia eneo Lingine mpaka pale mifumo yote ya usafirishaji na usambazaji ambayo mingi ni ya muda mrefu itakapokaa sawa.
Pia ukumbuke kuwa Tanzania ndio nchi yenye line ndefu kuliko nchi zote Africa mashark na ya kati Ambapo mpaka dec mwaka jana kulikuwa na kilomita zaidi ya 67,000 za line za usambazaji nchi nzima sawa na karibu mara 75 ya umbali wa safari ya kutoka dar mpaka mwanza, safari ambayo huwa inaanza saa12 asubuhi unafika saa5 usiku. line za usafirishaji zenye urefu wa km 5,000 zenye kusafirisha umeme wenye ukubwa tofaut tofaut karibu ya 120 mpaka 400kv na bado tunavyongea hapa mafundi wako site wanajenga zingine mpya na kukarabat zilizopo halafu leo hii unataka matengenezo yote hayo yakamilike kwa usiku mmoja itawezekanaje hapo ndugu????????????????????

Natumaini kwa maelezo hayo angalau umepata elimu ya kwanini matengenezo haya yanachukua muda na yanahitaji uvumilivu mwsho wa siku hali ikae sawa.

Hatutaki blah blah hizi na kama wewe ni msemaji wa TANESCO tafadhali nyamaza kimya, tunachotaka ni umeme!!!

Hizi nyimbo nyimbo zenu ambazo sasa zimekosa hata mwitikia korasi hatutaki!!!!????

Can't you try to move one extra mile to make sure that you come up with one permanent solution about this!!??

Mnatuona watanzania wajinga na mafala sana siyo kiasi ambacho leo mkija na maelezo haya kesho mnakuja na mengine na yet mnataka tuwaelewe???

NO WAY, ELSE TANESCO IPOTELEE MBALI KULE na zije kampuni zingine ziwekeze katika sekta ya nishati ya umeme ili wateja tuwe na choice kama ilivyo ktk sekta ya mawasiliano!!!!
 
niko hapa kutatua na kukusikiliza kama una Tatizo lolote na huduma za TANESCO. Nieleze una Tatizo gani niweze kukusaidia Tafadhali na si vinginevyo, ni vyema ukajaribu kutumia Lugha ya Staha ndugu mteja. karibu sana kama una tatizo lolote tutakusaidia kama zinavyoelekeza taratibu na kanuni za utoaji huduma za shirika.
 
Back
Top Bottom