Tunamwomba meneja TANESCO mkoa kuliangalia hili kwa jicho la undani zaidi, kwani wamiliki wa mashine za kukoboa na kusaga nafaka Makete tunanyanyaswa na uongozi wa TANESCO wilaya. bili tunapewa jioni na inapofika asubuhi tunakatiwa umeme na kupigwa faini wakati bili inaonesha muda wa kulipa bado. mfano tumepewa bili tarehe 19/12/2012 inayotaka tulipie kabla ya tarehe 24/12/2012 cha ajabu na cha kushangaza tarehe 20/12/2012 tumekatiwa huduma ya umeme na kupigwa faini ya sh 8000 je! nini maana ya muda wa kulipa? kwa nini hili jambo lijirudie mara kwa mara na kwa watu wachache? urasmu huu na kiburi cha meneja TANESCO makete kinatoka wapi? tunapiga kelele kila siku hajirekebishi tufanye nini juu ya watu kama hawa wasiowajibika ipasavyo?