TANESCO, maamuzi yenu ni maangamizi yetu

TANESCO, maamuzi yenu ni maangamizi yetu

bato

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
3,959
Reaction score
3,476
Wakuu,naomba msaada tutani.
Mwishoni mwa mwezi jana nilifungiwa umeme kwenye kibanda changu.Jana nilikwenda tanesco kulipia umeme 50units walizoniwekea za kuanzia. Nililipa 25,000tsh!! Receipt nikapewa.Baada kuuliza inakuwaje,nikaambiwa kuwa kila mwezi wateja tunatakiwa kulipa 7,000tsh kama service charges bila kujali kama umenunua umeme au la!! Ikitokea hukununua umeme mwezi/miezi iliyotangulia,itabidi ulipe kwanze service charges (7,000/mo)ndipo ununue umeme.
Hili ni shirika la umma au shirika la kuuma umma.
 
yamenikuta hayo..hivi service charge wanayokata ni ya nini? nina imani bei ya unit wanayotuuzia inatakiwa iwe imejumuisha masuala yote ya kuwafanya wao waweze kutoa huduma kwa faida...wenye ufahamu tuelimisheni
 
Usijali, nunua tu kwani huna mbadala wa Tanesco. Utakataa kama unaweza kupata mbadala. Tumeomba hili shirika libinafsishwe lakini hakuna wa kukusikia. Huyu ni mg'ombe wa maziwa wa wakubwa zako weye. Mkatie majani tu wakubwa wasihangaike
 
Hata Mimi limenikuta nimenunua umeme wamenikata service charge 11389 nikawa mpole.
 
haa haa tanesco nijanga la taifa,bill kubwa umeme hakuna,ukiongea ukweli unaitwa mpinzani.
 
Hili shirika linatutia umaskini. Wanakata umeme bila taarifa. Mchana huu wamekata umeme wao bila taarifa kama siku zote. Nafanya biashara ya vyakula, Ni hatari!! Nilalamike wapi?? Haya ni madharau kwa wateja. Kwao li-tanesco mteja ni mtumwa
 
Mbona Tanesco ndo mambo yao siku zote!!
 
wakuu, kuna dada majuzi aliniambia kama wewe ni mtumiaji wa umeme chini ya Units 70 kwa Mwezi basi inatakiwa uwe excluded kwenye mambo ya kulipa service charges...so kama Uko kwenye nafasi ya kufuatilia, inaweza kukusaidia.
 
Yaani kuna dada mmoja nesi aliwekewa mita ya LUKU ikawa inasumbua haiingizi umeme ndani. Akawafuata tanesco wanamuahidi tu kuwa wanakuja hawaji akazira. Alikaa karibu mwaka na kitu ndio akaamua kulivalia njuga tatizo hilo. Walikuja wakarekebisha tatizo umeme ukawaka. Yuniti zake 50 za mkopo ndio akaanza kuzitumia. Sasa zilipoisha alipoenda kurecharge aliambiwa alipe kwanza service charge ambayo wakati huo ilishafikia zaidi ya laki moja!!! Alilipa ndio akanunua umeme. Yaani LUKU ni maumivu sana.
Kinachonikera unalipa service charge elf 7 na bado kila yunit unayonunua bei yake imehusisha VAT,REA,sijui na nini. Wakati huo huo wateja wa mita za kawaida ukiangalia bili imeandikwa service charge 0, VAT 0,REA,0 nk. Yaani utafikiri hizo LUKU tulienda kuziomba.
Halafu wakikufungia mwishoni mwa mwezi mfano julai 22, ukatumia hizo yuniti 50 hadi agosti 18 kwa mfano, utakapoenda kurecharge unalipishwa service charge ya julai na ya agosti!! Ndio mambo ya tanesco hayo, yaani wanatia hasira sana.
 
wakuu, kuna dada majuzi aliniambia kama wewe ni mtumiaji wa umeme chini ya Units 70 kwa Mwezi basi inatakiwa uwe excluded kwenye mambo ya kulipa service charges...so kama Uko kwenye nafasi ya kufuatilia, inaweza kukusaidia.

Wahuni tu hao watu, ukienda wanasema utumie kwanza mwaka mzima ili waangalie mwenendo wa matumizi yako ndio wakuhamishie kwa watumiaji wadogo! Mwaka mzima maana yake ni 7000 mara 12 ni 84,000. Ulipe hizo kwanza ndio wakuhamishe!!
 
Hii nchi wananchi ndio mnao ibeba.Lieni sana lakini ikifika oktoba ndio ntajua kama mna akili au mnalalamika tu.
 
Hili shirika linatutia umaskini. Wanakata umeme bila taarifa. Mchana huu wamekata umeme wao bila taarifa kama siku zote. Nafanya biashara ya vyakula, Ni hatari!! Nilalamike wapi?? Haya ni madharau kwa wateja. Kwao li-tanesco mteja ni mtumwa

Halafu eti utumwa uliisha zamani! Utumwa wa sasa ni mbaya kuliko wa zamani maana unatumikishwa bila kujiona hadi uhisi maumivu hapo ulishaliwa sana.
 
Tupo kama 5 tuliopata hasara ya kuharibikiwa biashara zetu baada ya umeme kukatika bila taarifa. Kati yetu,3 tumesajili biashara zetu,tunalipa kodi mbalimbali. Tunataka kulishtaki tanesco. Kuna wakili Yuko naye mtaani.
 
Yani nimekuja arusha since jumapili umeme unakatwa saa 12 asubui unarudi saa tano usiku, nauliza wenyeji wananiambia ndo kawaida
 
Niliwahi kuwauliza wahusika kuhusu hiyo service charge maelezo yao ni kwamba hiyo ni tahadhari ya kukarabati miundombinu ya umeme, ndio maana pakitoea uharibifu kwenye nguzo au transformer hapo mtaani kwenu hamdaiwi gharama za matengenezo!
 
Yaani hii Tanesco inanikera sana nimelipia service charge huu unaenda mwezi wa tatu hawajakuja kuniungia umeme hadi naingia gharama za kununua jenereta nikiwauliza wanasema nguzo hamna
 
Back
Top Bottom