TANESCO Kisarawe hawaendani na kasi ya Rais Magufuli

Tafakuli

Member
Mar 26, 2011
85
80
Hivi karibuni Tanesco kisarawe wamesambaza nguzo za umeme katika eneo la kwa Mbiki mtaa wa Zavala. Wakazi wa eneo hilo ambao walihamishwa kutoka Kigilagila takriban miaka saba iliyopita walipata na kuona mwanga umewafikia kwa kukosa huduma hito kwa muda mrefu. Cha kushangaza watu walijaza fomu tokea mwezi 8 mwishoni na kuja kufanyiwa ukaguzi mwezi wa 9 mwanzoni. Baada ya ukaguzi waliambiwa wiki moja au mbili watatumiwa meseji ya kwenda kulipia gharama za kuunganishwa ume. Cha ajabu mwezi umekatika bila meseji hizo kutumwa na hazijatumwa hadi sasa. Sasa watu wanajiuliza hawa tanesco hawataki fedha? Au wamezidiwa. Ktk hali ya kawaida wangechangamkia pesa lkn wala hawasituki. Hv hawa kweli ndio watumishi anaowataka JPM? Nadhani Meneja wa hapo ameshindwa kazi ashushwe awe mtumishi wa kawaida kwa sababu abalikosesha mapato Shirika
 
Wata toaje Huduma ya Umeme wakati hii tu wanayo toa wameshidwa himudu kila Simu wana kata umeme huku Chanika
 
Kasi ya Magu inaanzia Chato, huko Kisarawe ni mbali sana lakini wasijali mpaka 2020 watapata umeme.
 
Back
Top Bottom