whizkid
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 357
- 240
Wadau, kuna tetesi ambazo zinaendelea kuletwa na baadhi ya wachangiaji (tetesi kwa sababu hakuna ushahidi) kuwa TANESCO wanagawa units 700 za umeme kwa wafanyakazi. Ni kweli? Itapendeza kama kuna mdau wa TANESCO atatuletea ushahidi. Kama ni kweli, naomba tusaidiane kuinyambua hii hoja vizuri. Kwanza, nina maswali mawili:
Je, ni bora TANESCO izijumuishe hizi pesa kwenye mishahara ya wanufaika au ni bora kuendelea kugawa units kama inavyosemekana?
Je, hata kama TANESCO inaendeshwa kwa hasara, kuna ubaya gani kuwa na bei maalum za wafanyakazi (kama ilivyo kwa mashirika mengine mengi nchini na duniani kote) au "bonus" za units za namna hii?
UPDATE (5 Jan 17 - 12:30):
Mpaka sasa hakuna aliyekuja na ushahidi wa uhakika, japo wapo baadhi waliochangia kuwa ni kweli wanapewa units 700 (wengine wamesema ni units 750) kila mwezi kwa gharama ya TShs 10,000. Maana yake, hiyo gharama iliyobaki inabebwa na shirika. Ni jambo jema kuwa na benefits za namna hii kwa wafanyakazi hasa kwa shirika linalopata faida.
Maswali ambayo hayajajibiwa ni kama wanaopata hizi units ni wafanyakazi wote wa TANESCO au baadhi (idadi), na kama hii ni sawa kwa shirika linaloendeshwa kwa hasara (baadhi ya wachangiaji wanaoneshwa kukasirishwa na utoaji wa hizi benefits kwa TANESCO na wengine wakishambuliwa kuwa wana wivu).
Pia, kwa wale wanaoendelea kunishambulia kwa kusema kuwa nina wivu au roho mbaya (na mengineyo yanayofanana na hayo), ifahamike kuwa sio lengo langu kuona TANESCO inawanyima wafanyakazi benefits za namna hii. Lengo ni kufahamu usahihi wa jambo na athari yake (implication) kwenye matumizi/gharama/pato TANESCO na kama kuna athari kwa mtumiaji wa mwisho (mfano bei ya umeme). Mengineyo ni yatokanayo tu. Tujikite kwenye hoja tafadhali.
- Ni wafanyakazi gani na/au wangapi wanaopewa units 700?
- Wanapewa units hizo kila baada ya muda gani?