TANESCO inagawa units 700 za umeme kwa wafanyakazi

whizkid

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
357
240
Wadau, kuna tetesi ambazo zinaendelea kuletwa na baadhi ya wachangiaji (tetesi kwa sababu hakuna ushahidi) kuwa TANESCO wanagawa units 700 za umeme kwa wafanyakazi. Ni kweli? Itapendeza kama kuna mdau wa TANESCO atatuletea ushahidi. Kama ni kweli, naomba tusaidiane kuinyambua hii hoja vizuri. Kwanza, nina maswali mawili:
  1. Ni wafanyakazi gani na/au wangapi wanaopewa units 700?
  2. Wanapewa units hizo kila baada ya muda gani?
Ifahamike kuwa, kwa bei za sasa za umeme, units 700 gharama yake ni takribani shilingi za Kitanzania laki mbili na ushehe (kwa maana ya 292 TShs kwa kila unit, kwa wateja wa T1).

Je, ni bora TANESCO izijumuishe hizi pesa kwenye mishahara ya wanufaika au ni bora kuendelea kugawa units kama inavyosemekana?

Je, hata kama TANESCO inaendeshwa kwa hasara, kuna ubaya gani kuwa na bei maalum za wafanyakazi (kama ilivyo kwa mashirika mengine mengi nchini na duniani kote) au "bonus" za units za namna hii?

UPDATE (5 Jan 17 - 12:30):
Mpaka sasa hakuna aliyekuja na ushahidi wa uhakika, japo wapo baadhi waliochangia kuwa ni kweli wanapewa units 700 (wengine wamesema ni units 750) kila mwezi kwa gharama ya TShs 10,000. Maana yake, hiyo gharama iliyobaki inabebwa na shirika. Ni jambo jema kuwa na benefits za namna hii kwa wafanyakazi hasa kwa shirika linalopata faida.

Maswali ambayo hayajajibiwa ni kama wanaopata hizi units ni wafanyakazi wote wa TANESCO au baadhi (idadi), na kama hii ni sawa kwa shirika linaloendeshwa kwa hasara (baadhi ya wachangiaji wanaoneshwa kukasirishwa na utoaji wa hizi benefits kwa TANESCO na wengine wakishambuliwa kuwa wana wivu).

Pia, kwa wale wanaoendelea kunishambulia kwa kusema kuwa nina wivu au roho mbaya (na mengineyo yanayofanana na hayo), ifahamike kuwa sio lengo langu kuona TANESCO inawanyima wafanyakazi benefits za namna hii. Lengo ni kufahamu usahihi wa jambo na athari yake (implication) kwenye matumizi/gharama/pato TANESCO na kama kuna athari kwa mtumiaji wa mwisho (mfano bei ya umeme). Mengineyo ni yatokanayo tu. Tujikite kwenye hoja tafadhali.
 
Cjaona mantiki za watu kumshambulia mtoa mada,nafikir kama kuna ukweli na unajulikana tujadili kwa hoja maana shirika ni letu sote

Yeye ndiyo anatakiwa alete ukweli!! Na hata kama ni kweli hayo ni mambo ya kawaida katika kazi!
 
Umeona kuchangie kule kule haiwezekan...ukaamua kuja na tetesi ili iwaje...elimu yako bado ndogo sana hapa umetapika ujinga wakati ulikosoma kule kwenye uzi halisi kasema vizuri

dlnobby ni uzi upi ambao yamejibiwa maswali yangu kwa ushahidi? Weka link tuone nani "katapika ujinga".
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Kumbe kweli wanapata we ng'ang'ania watakuambia tu na wenzao wengi kumbe wanajuana tunaliwa sisi tu.
 
Wwala sio tetesi, ni kweli wanapewa units 750 kila mwezi na wala sio jambo la kuficha.

Ni sehemu ya kazi wala haina kificho kama ilivyo kwa sumatra wanalipa wafanyakazi wao laki 3 ya mafuta kila mwezi au lesheni ya laki 3 kila mwezi ya askari.

Bodi ya mkopo wanatoa mafuta kwa kila mfanyqkazi wao,tpdc hivyo hivyo,mashirika ya hifadhi za jamii,tax exempt kwa wafanyakazi wa serikali kuu na serikali za mitaa.

Wala huna haja ya kuja kuuliza huo ujinga hapa kana kwamba ni kitu maalum sana kinachotolewa tanesco.

Ulitaka wasipewe umeme upewe wewe
 
Watanzania ndiyo mana hatuendelei tunapenda unafk sana kuliko kufanya kazi
,
Hivi unajua kuna wafanyakazi wanapewa
Malazi bure na mpaka chakula bure? Na ni tanzania hii hii au umekariri tanesco tu!

Mantiki ya mtoa hoja anataka afahamu kama ni kweli.Na kama ndivyo basi haki itendeke na kwa wengine.Kama watumishi wa taasisi moja wanapata incentives za aina hiyo wakati wengine wanaishi kwa mshahara tena mshahara ambao haukizi hata mwezi sasa kwa nini kuwe na upendeleo?Hawa wote ni watumishi wa umma na hao wanaojengewa nyumba mimi naamini hawapewi bure bali huuziwa na hao wanapeana bonasi wako wengi tu hasa hizi taasisi za fedha kama PPF,NSSF,PSPF,GEPF,LAPF nk.Nayo yanapaswa yachunguzwe kwani fedha hizo wanazopeana bonasi siyo za kwao ni za watumishi wa mifuko husika nao pia watumbuliwe.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom