TANESCO inagawa units 700 za umeme kwa wafanyakazi

Wwala sio tetesi, ni kweli wanapewa units 750 kila mwezi na wala sio jambo la kuficha.

Ni sehemu ya kazi wala haina kificho kama ilivyo kwa sumatra wanalipa wafanyakazi wao laki 3 ya mafuta kila mwezi au lesheni ya laki 3 kila mwezi ya askari.

Bodi ya mkopo wanatoa mafuta kwa kila mfanyqkazi wao,tpdc hivyo hivyo,mashirika ya hifadhi za jamii,tax exempt kwa wafanyakazi wa serikali kuu na serikali za mitaa.

Wala huna haja ya kuja kuuliza huo ujinga hapa kana kwamba ni kitu maalum sana kinachotolewa tanesco.

Ulitaka wasipewe umeme upewe wewe
Yani kila mmoja anapewa Units 750???? Kila mwezi!? Times 10 ya umeme wa Mlalahoi!
 
Kwa TIJA gani au faida ipi ?hawa wa fanyakazi wa TANESCO wanalipatia shirika hadi wapewe BONUS .....nyie Watanzania mtaendelea kupiga marktime hadi mwisho wa DUNIA

Hivi hawa Watanzania mmelogwa na nani? Nyie watu shirika lenyewe lipo ICU umeme wenyew sio wa uhakika bado wafanya kazi wanapeana BONUS hivi vitu vinatokea Tanzania tu....mm nahisi TZ ipo sayari nyingine kabisa tofaut na hii ya Dunia
 
Wadau, kuna tetesi ambazo zinaendelea kuletwa na baadhi ya wachangiaji (tetesi kwa sababu hakuna ushahidi) kuwa TANESCO wanagawa units 700 za umeme kwa wafanyakazi. Ni kweli? Itapendeza kama kuna mdau wa TANESCO atatuletea ushahidi. Kama ni kweli, naomba tusaidiane kuinyambua hii hoja vizuri. Kwanza, nina maswali mawili:
  1. Ni wafanyakazi gani na/au wangapi wanaopewa units 700?
  2. Wanapewa units hizo kila baada ya muda gani?
Ifahamike kuwa, kwa bei za sasa za umeme, units 700 gharama yake ni takribani shilingi za Kitanzania laki mbili na ushehe (kwa maana ya 292 TShs kwa kila unit, kwa wateja wa T1).

Je, ni bora TANESCO izijumuishe hizi pesa kwenye mishahara ya wanufaika au ni bora kuendelea kugawa units kama inavyosemekana?

Je, hata kama TANESCO inaendeshwa kwa hasara, kuna ubaya gani kuwa na bei maalum za wafanyakazi (kama ilivyo kwa mashirika mengine mengi nchini na duniani kote) au "bonus" za units za namna hii?
Sijakuelewa kwa hiyo bei uliyotaja.Mimi ni mtumiaji WA kawaida WA nyumbani hata hivyo nanunua unit 1 kwa shs 354 /-na ushee.yaani nikitoa tshs 5000 napata unit 14.10 hii maana yake nini ?
 
Ni kitu cha kawaida na kipo nadhani humo tanesco tangu 1970's msije msingizia mzee wa watu alietumbuliwa maana sisi waswahili ni hatari sana
 
Cha ajabu nini? Mbona WABUNGE WA CCM majuzi waligawana shs 10 M kila MMBUNGE na wakadai walikuwa wanagawana pesa zao? Mie naona ni motisha kwao sio mbaya.
 
Mbona wanajeshi na polisi wanatumia umeme bure kwenye kota zao? Mnawasema bure wafanyakazi wa Tanesco
Hizi "mbona, mbona" zinaifanya hoja yako kuwa nyepesi.
Simama kwenye hoja ya mleta mada, ..ni halali Tanesco kupeana hizo "units" ?
Haina maana kwamba kama majeshi wanapewa labda kwa makosa, basi Tanesco nao wachukue! Mambo hayaendi hivyo. Kosa halihalalishi kosa jingine
 
Ni sawa ,ndo motivation unataka mfanyakazi wa tazara alipe Bei ya treni sawa na wewe??
 
Kinachoimaliza Tanesco ni hivi;
  1. Mikataba mibovu ya kufua umeme/gas iliyoingiwa na viongozi wa awamu wa 3 na 4.
  2. Serikali na taasisi zake kutokulipa umeme wanaotumia kwa muda mrefu
 
Mbona wengine wanalipiwa kila kitu kuqnzia chakula...malazi hadi house girl na bado wanalipwa mishahara isokatwa kodi..acha ujinga www
 
Inashangaza kuona watu wanaona ni sawa kwa wafanyakazi kupewa vitu bure. Huu ni wezi na hujuma kupitiliza. Ndio maana Hii nchi haiendelei. Wafanyakazi wa kawaida wanapewa misamaha isiyo stahiki na wakurugenzi je? Uovu unafanyika mfano Tanesco wapo wafanyakazi wanapewa hizo units halafu anamwandikisha na baba mama dada kaka shemeji n.k Tufike mahali hii tabia ikomeshwe kila mahali kila mtu apewe ujira wake kwa kufanya kazi. Wale walioko vijijini Nani anawasaidia kwa kila jambo?! Huu Utaratibu ukomeshwe period! Kwa hivi na wafanyakazi wa bank wapewe tuuu pesa kwa sababu ni wafanyakazi wa bank?!
 
Sasa kama hayo ya mara viwanda vya sukari, chumvi, mikate mara vinawagawia wafanyakazi wao bidhaa mara Tanesco wanagawa units kwa wafanyakazi wao na mnayaona fair kwa nini Serikali ya CCM ilivyowagawia wabunge wake million 10 10 mliona shidah sana na kwanini serikali ya CCM ikijinufaisha mnamaind..!!??
 
Wadau, kuna tetesi ambazo zinaendelea kuletwa na baadhi ya wachangiaji (tetesi kwa sababu hakuna ushahidi) kuwa TANESCO wanagawa units 700 za umeme kwa wafanyakazi. Ni kweli? Itapendeza kama kuna mdau wa TANESCO atatuletea ushahidi. Kama ni kweli, naomba tusaidiane kuinyambua hii hoja vizuri. Kwanza, nina maswali mawili:
  1. Ni wafanyakazi gani na/au wangapi wanaopewa units 700?
  2. Wanapewa units hizo kila baada ya muda gani?
Ifahamike kuwa, kwa bei za sasa za umeme, units 700 gharama yake ni takribani shilingi za Kitanzania laki mbili na ushehe (kwa maana ya 292 TShs kwa kila unit, kwa wateja wa T1).

Je, ni bora TANESCO izijumuishe hizi pesa kwenye mishahara ya wanufaika au ni bora kuendelea kugawa units kama inavyosemekana?

Je, hata kama TANESCO inaendeshwa kwa hasara, kuna ubaya gani kuwa na bei maalum za wafanyakazi (kama ilivyo kwa mashirika mengine mengi nchini na duniani kote) au "bonus" za units za namna hii?[/QUOT

Ni kweli, wanauziwa units 700 kwa Tsh.8,000 kila mwezi japokuwa hawalazimishwi kununua.

Ila sioni tatizo wala shida yoyote wakipewa bonus kama hii.
 
Umeona kuchangie kule kule haiwezekan...ukaamua kuja na tetesi ili iwaje...elimu yako bado ndogo sana hapa umetapika ujinga wakati ulikosoma kule kwenye uzi halisi kasema vizuri
Ilikuwa lazima utumie lugha ya matusi, tuna tatizo kuelewa elimu/ustaarabu wako.
 
Back
Top Bottom