Tanesco hili nalo neno.

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Kuna Mbunge ameliona hili juu ya utaratibu wa sasa wa Tanesco la wateja kugharimia vifaa vy a nguzo na nyaya pale mteja anapotaka kuanganishiwa huduma ya umeme.

Hatukatai kwamba ni utaratibu waliojiwekea lakini mbona mteja anapogharimia umbali mrefu na baadae wakajitokeza wateja wengine kwenye mkondo(line) iliyogharimiwa na mteja mwenzao hawampi japo asilimia kidogo ya service charge?

Kwa hili Tanesco wataendelea kuibiwa kwani nafikiri wengi wanajilipa gharama za nguzo na nyaya walizotoa na baadae kutumiwa na wateja wengine pia bila wao kufikiriwa chochote.

WanaJF kuna mwenye la kusema juu ya hili? Ni mtizamo tu, nawasilisha.
 
Hatukatai kwamba ni utaratibu waliojiwekea lakini mbona mteja anapogharimia umbali mrefu na baadae wakajitokeza wateja wengine kwenye mkondo(line) iliyogharimiwa na mteja mwenzao hawampi japo asilimia kidogo ya service charge?
hapo umesema ukweli kabisaaaaaaaaaaa.....hata watu wa dawasco wanatabia hiyo.....tunawaomba wabadirike.....
 
Pape ni kweli hadi umeenda shule huelewi tofauti ya TANESCO na DAWASCO??Hebu usituzengue buree tu!
 
Mimi ningeishauri TANESCO iwajibike kuakikisha kila mteja anaye hitaji huduma ya umeme wanampelekea kwa gharama zao. Wanachopaswa kudai kwa mteja tu niyale matumizi ya umeme.
Wakifanya hivyo watapata wateja wengi na pia watajipatia kipato kikubwa zaidi.
 
Ulimbo,
Ni kweli kabisa wala hakuna haja ya kupiga ramli mapato yataongezeka kwani uzalendo pia utaongezeka kwa wanaotumia kwa jinsi wateja watakapopatiwa bila kugharimia nguzo na nyaya ambazo kwa hakika si mali yao.
 
Bora sisi ambao tumeamua kutumia solar tu. Tanesco wezi sana.
Ukienda pale unapigwa tarehe utadhani wanakupa bure kumbe unalipia
 
Ni kweli kabisa utapigwa tarehe mpaka uchoke hata kufatilia, jamani nina swali, hivi baada ya kulipia hizo gharama inachukua muda gani mpaka waku letee hizo nguzo?
 
kwakweli mda maalumu akuna miaka ya nyuma atamiaka utasubiri na umelipa kila kitu ila kama unaweza kumlipa mpiga zeze utachagua ck ya kuwekewa
 
Back
Top Bottom