TANESCO hakika mnaunguza maisha yetu!

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
2,345
4,168
Mwananchi mwenzangu ukipta nafasi ya kuwa mwanasiasa hebu usiipoteze, siasa ndiyo tunu na pepo ya maisha ya Mtanzania. Tumia mbinu yoyote unayoijua ila kama kuna fursa ya kuingia kwenye siasa katu usiilazie damu.

Mdogo wangu ni mhitimu wa chuo kikuu, baada tu ya kutoka chuo akaingia kitaa kupiga mitikasi na mdogo wangu sio mzembe kwa kweli ni jembe hasa yaani linapokuja suala la kazi na uhakika wa malipo akili huwa inamruka.

Akaanza kujichanganya kitaa kwa miaka minne akiniambia "Bro mimi napambana kwa namna yoyote ili niwe na changu sitaki kuwa mzigo wa mtu" binafsi nikataka kutia neno lakini nikasema ngoja nimuache kwanza.

Saidia fundi ya uashi kapiga, sijui userelemala wa kujengea nguzo kwenye maghorofa kapiga, kuuza magazeti na mifuko buguruni kapiga, hapa Dar viwanda vingi vikubwa kachapa (kuanzia NIDa, METL, cha tambi kile Vingunguti, cha plastic Kipawa, cha rangi Chang'ombe na kadhalika na kadhalika.

Ikafikia hatua nikaanza kumuonea huruma janja, maana kazi anapiga mno ila inaishia kwenye vitu vya kila siku yaani nauli, chai, chamcha, chajio, vocha, akiba ikawa kama ndoto. Kuna nyakati anakuja kwangu tunaongea sana ananiambia "Braza mi sielewi hili life, nahisi kufa kufa tu maana nikipiga hatua nne mbele ghafla najiona kumi na tatu nyuma."

Nikamwambia "Pole bro, naelewa namna unavyopitia maana hata we mwenyewe unajua bro wako nimetoka katika njia hizo hizo ila usijali mimi ndugu nitajaribu kufanya kitu kwa ajili yako, kwa sasa we relax kipande kilichobaki niachie, hata hivyo umejitahidi sana."

Nikajipinda kwa namna yangu nikamnunulia janja jokofu la kishkaji tu, nikamtafutia site huko pande fulani za Mandela, nikamuwekea na vinywaji baridi pale ahangaike navyo, na yeye mwenyewe akawa na vichenji kadhaa akaongezea na kuuza vitafunwa vya kuzugia pale dogo life likaanza.

Shida za TANESCO zinaanzia hapa

2021 Alianza mitikasi yake akawa ananunua umeme wa 5000 ambao alikuwa anapata unit 40+ na anaitumia mwezi mzima na maisha yanasonga, lakini ghafla bin TANESCO bin Maharagwe bin MacAmber mabadiliko ya kipumbavu yakatokea kwenye shughuli yake. Ile 5000 aliyokuwa ananunulia units 40+ ikawa ananunua kwa units 8 nukta kadhaa.

Kupiga simu huduma kwa wateja "Ooh nyie mwanzo mlikuwa mpo watumiaji wa chini sasa hivi mmepanda daraja mmekuwa watumiaji wa kati hivyo na gharama zinabadilika," nikasema haya.

Sasa jamani ndugu zangu hivi hawa wako serious kweli? Yule ambaye anatumia huduma mara nyingi si ndiyo anahesabika kama mzalishaji bora kwa kipato chako? Si ndiyo ambaye anapaswa kupatiwa ahueni ili aendelee kuzalisha vyema na kipato kiongezeke? Au mimi ndio elimu yangu ndogo jamani?

Hivi huu uongozi wa TANESCO ni nani aliyewaloga? Ni mganga gani huyo aliyewaambia kwamba ukimtesa Mtanzania mdogo mjasiriamali ndiyo nyie mnapata faida? Yaani hata shetani ana akili kuwazidi watendaji wote wa TANESCO. ]

Maana shetani akitaka kukutumia lazima akupe kwanza kitu kinachokunufaisha hata kwa muda naye ndio aanze kukufaidi. Ila sio hawa nyonyanyonya TANESCO, hawa ni ma-vampire, hawaangalii huyu ni nani, wananyonya hadi vinyesi tumboni wanakausha kila kitu.

Haiwezekani nchi hii ni yetu wote lakini wengine tunaishi kama vile tumekodisha. Tunajua mnatuibia lakini basi hebu mtuibie kwa aibu jamani! Hebu tuibieni lakini na sisi pia tupate hata pa kwenda kufukia vinyesi vyetu.

Tunajua mmepata hizi nafasi mlizozitamani kwa muda mrefu na kuziapia kuwa mkizipata sisi mafala tutajuta, lakini angalau msisahau na ule msemo "Ukitaka kula na kipofu usimshike mkono."

TANESCO mnaunguza maisha yetu jamani, zaidi ya asilimia 70 ya shughuli zote hapa nchini zinategema umeme, mnachotufanyia ni uhaini na uhujumu uchumi.

Huyu dogo alikuwa ananipiga tafu sana katika kuitunza familia yetu kule bushi ya wazee na wadogo, lakini hebu angalia units 8 atatoa 5000 mara ngapi kwa mwezi? Hiyo hela ya ziada mnayotuibia ndio ambayo tulikuwa tunawapa wazazi wetu, leo mnatupora yote, daah! Bado Kodi ya nyumba, Kodi ya fremu, mtaji, mahitaji ya kila siku, bado watu hawajaonga ili wadinye, kweli?

Mungu mbariki John Pombe Joseph Magufuli, jina lake likatajwe kwenye nafasi za watu wa pekee huko mbinguni.

Amina
 
Hapo Mwisho Kwenye Huyo Ulomtaja kwamba akae na wabarikiwa Huko Umekuita Mbinguni, Anyway sijui Nilitaka kusema nini.
 
Back
Top Bottom