Kuna mambo nchi hii yanatia hasira kupitiliza. Yaani unajibana miaka chungu unapata zako laki 3 unasema ukamwekee mzazi wako umeme walau nae aepuke karaha za giza. Unaenda TANESCO unapewa control number ya kulipia halafu unaambiwa umeme usubiri kwani kuna watu tangu December mwaka jana hawajapata umeme. Hii maana yake nami nisubiri hadi mwakani!!
Sasa kama TANESCO hili tu la kununua Meter na kufungia mtu at a time mnashindwa sijui mtaweza lipi katika dunia hii ya teknolojia!! Kama kwenu kununua vifaa ni shida ni bora hizo hela kila mtu angeruhusiwa anunue vifaa yeye mwenyewe na nyinyi muje tu kuunganisha lakini hili mnalofanya ni jambo la kishamba lililopitiliza.
Ombi:Kama kuna mtu anaweza kunisaidia namna ya kurudisha hiyo hela yangu niliyolipia nikaifanyie mambo mengine.