Zito kisha kapoteza mwelekeo siku nyingi ninyi hamjui tu. kisha nunuliwa, hana kauli yake tena. Msimamo wote umeyeyuka.
Good analogy Tina, somebody said...BIRDS OF THE SAME FEATHERS FLY TOGETHER?... or are we dreaming!!!Gazeti la Rostam Aziz (Mtanzania), leo limeandika habari inayofanana kimaudhui na hoja ya Zitto kuwa ukiwauliza wafanyakazi wa Tanesco watakwambia kuwa Rashidi ni one of the best CEOs of our parastatals. Ikumbukwe pia kuwa Zitto alitetea mpango dhalimu wa kununua mitambo iliyotumika ya Dowans. Pia Zitto huyu huyu alishabihiana tena kimawazo na Rostam pale alipo tamka kuwa Richmond ichunguzwe upya na jopo la majaji, which is unconstitutional kwani one pillar of the state (judiciary) haiwezi kufufua upya jambo lililo amuliwa na another pillar (legislature). Leo hii Zitto ameibuka tena na kumtetea hadharani Rashidi eti ni kiongozi bora zaidi.
Swali ninalo jiuliza, Je Rostam Aziz na Zitto ni wabia? Au it's just a coincidence tu kuwa wana mawazo ya kufanana kwenye maswala nyeti, eg Dowans, Richmond na hatma ya Rashidi?
Zitto
Maoni yako mazuri lakini yanafaa darasani na majamvini kama humu tu. Uko kwetu Uswazi hayafai. Dr. Rashidi hawezi kuwa CEO bora unless analinganishwa na ma CEO wachovu. Hakuna nchi yenye ambako ili mtu apawe huduma ya umeme inabidi:-
-Abembeleze power company badala ya kampuni kumbembeleza ili afanye nayo biashara
-Mteja anunue nguzo ya umeme wakati atalipa bill ya umeme
-Mteja atoe rushwa ili apate huduma ya umeme
-Mteja apate hasara ya kuunguziwa vifaa vyake na umeme, akilalamika akatiwe umeme
-CEO atumie milioni 60 kuweka maua na mamazia nyumbani kwake wakati kuna mgawo wa umeme nchi nzima, n.k
Ubora wa CEO huyo uko wapi Zitto? You are not playing devil's advocate, you are blaspheming the public service.
Huyu jamaa kisha poteza mwelekeo, kishakula hela za watu hana tena uhuru wa kusema mambo yake. Misimamo yote kwisha.
Kauli hii ya Zitto inanikumbusha msemo maarufu utuatao....Kuandika habari kutoka JF sio tatizo na inasaidia kutangaza JF. Hata hivyo kuandika habari maliciously kutatufanya wengine tuogope kutoa mawazo yetu kwa uhuru humu katika jukwaa letu.
Habari hii imeandikwa kwa nia mbaya.
Sasa itabidi niwe msomaji tu JF. Endeleeni na mijadala bandugu.
Zitto
Aisee ni wabia hawa, zipo dalili, namuheshimu Zito lakini mwenendo wake unatia mashaka sana.Gazeti la Rostam Aziz (Mtanzania), leo limeandika habari inayofanana kimaudhui na hoja ya Zitto kuwa ukiwauliza wafanyakazi wa Tanesco watakwambia kuwa Rashidi ni one of the best CEOs of our parastatals. Je Rostam Aziz na Zitto ni wabia? Au it's just a coincidence tu kuwa wana mawazo ya kufanana kwenye maswala nyeti, eg Dowans, Richmond na hatma ya Rashidi?
Kamanda, umesema yote! Kuwepo kwa Mh. Zitto hapa kuliwezesha mijadala mingi kusikia na upande wa system upo vipi na unasimama vipi kwa hoja mbalimbali ambazo Mh. alishiriki.Tumeshindwa kukutumia mh., pia hakuna anayejali unaathirika vipi kisaikolojia kwa haya maneno. Mimi nakubaliana na wewe after all tuna wabunge wengi sana kama 300 hawaonekani humu, tunayekuona tunakupiga mawe humu humu na watu wanalisha watoto wao kwa kuuza magazeti,watu wanasema bila vithibitisho.Hakuna anayejiweka nafsi yako aone unajisikia vipi.Yet tunalilia mabadiliko wakati wapiganaji tunawapiga kabali
Hii dhambi na tabia hii imerudisha nyuma wengi, siasa kwa vijana Tz ni ndoto, watu watabaki kuwa wenyeviti wa kipaimara na harusi za ijumaa na jumamosi kwisha!
Inaboa sana, wazo lako zuri litakusaidia mkuu! tunakujali mkuu!
Huyu jamaa kisha poteza mwelekeo, kishakula hela za watu hana tena uhuru wa kusema mambo yake. Misimamo yote kwisha.
utumbo mwingine huo!
kwa hiyo na mimi nikisema RWECHU ni fisadi then watu wataniamini?
Mkuu ukiweka vithibitisho havitaisaidia JF tu, ila vitaongeza heshima yako wewe! maana mawazo yako hayana tofauti na ya mtaani , na kwa tabia hii CCM haitatoka madarakani mkuu, kwa nini umejiingiza kwenye kundi la wapumbavu! wewe sio mmoja wapo, story za vijiweni hazitusaidii
Just imagine wewe ndio Zito na mtu kaandika ulivyoandika wewe na pengine ni completely false.Ikiwa kweli ukatuhabarisha tutapona wengi!
Rwechu huyu sio wewe usiige wengine, wameshajichokea
mwandoshi wa makala hii toka gazeti la kulikoni yumo hmu janvini na huwa hachangii mada, kzi yake ni kuandika maoni ya watu kisha kupleka gazetini, na hawa kulikoni huwa hawana jipya habari zao zote 97% huwa zinatoka hku janvini then wanasema ''uchanbuzi wa kina''
Pre-emptive strategy...........!
Umpende usimpende Rashidi, ni one of the best CEOs of our Parastatals.
Mkuu kupendwa na wafanyakazi wa chini siyo jambo baya,but perfomance is what matters,kwa hiyo unataka kuniambia hao wanabodi,wanasiasa,Dr Idrissa na wafanyakazi wa chini wako kambi moja,na hiyo kambi nyingine hatuijui,ama ndiyo hiyo waliyoko hao "mameneja?' Mh Zitto keshasema kuwa "kuna wanasiasa" wako behind some few applicants ambao anadai "wameline up" Sasa kwani Dr Idrissa hana wanasiasa ambao wako nyuma yake?Mh Zitto yeye si mwansiasa?Rostama Aziz,Lowassa ambao wanahusishwa na Richmond/Dowans si wanasiasa?Hao na Dr Idrissa pamoja na Zitto hawataki mitambo inunuliwe?Mwandishi ameishiwa. hana maana.
Jamani lazima tukumbuke Zitto ni mtanzania kama wananchi wengine. na vile vile tunatakiwa tujuwe Zitto hayupo juu ya sheria za nchi. Yeye anao uhuru wa kutoa maazo yake kama mtanzania yoyote ili mradi tu asivunje sheria za nchi.
Kwa hakika hata mimi na kwa ninavyomfahamu Dr Idriss siwezi amini kabisa kama aneeza fanya mabaya dhidi ya Tanesco. Hata vyombo vyenu vya habari vya huko vimesema wazi kuwa Dr anapendwa sana na wafanyakazi wa chini na anachukiwa na mameneja. Sababu kuu ni kuwapunguzia posho zao walizojiwekea na kuwalipa wafanyakazi wa kawaida.
nakuunga mkono Zitto kwa kuona wazi juhudi na kazi zote na maamuzi sahihi ya Dr Idrissa.
Tuache siasa kwenye kitu cha kitaalamu.
Jumuisho la yote kwa mwandishi wa habari hiyo ni kwamba Mh. Zitto anampiga debe Dr. Rashid ilhali Mh. ametoa ufahamu wake juu ya utendaji kazi wa Dk. Rashid.Ndg. Kibunango, Je ni meneno gani ambayo gazeti limemnukuu vibaya Zitto? Tuwe makini na sweeping statements, mimi nimefuatilia kwa makini mjadala wa JF kuhusu Dk. Rashidi. Kulikoni imenukuu verbatim (neno kwa neno) michango aliyoitoa Zitto kwenye JF. Naomba upitie habari ya Kulikoni kwa makini utuonyeshe ni maneno gani Zitto amekuwa misquoted. Ni vizuri tukajenga hoja kwa facts kuliko kutoa sweeping statements.