TANESCO BIG UP!

TANESCO BIG UP!

Shukran
Number ya metre bado haijabadilishwa, naomba ulifatilie zaidi hili
metre number: 24211954755
TANESCO

Lakini pia ikumbukwe nadai units 100
Ndugu mteja,

Pole kwa changamoto unayopitia. Tunakufahamisha kuwa taarifa yako imewasilishwa idara husika, na tunaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha unapata huduma stahiki. Namba mpya ya kumbukumbu ya taarifa yako ni ILL112026TB-14554, kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji. Tunaomba uvumilivu wako wakati suala lako likishughulikiwa.

Asante.^NI
 
Watu wanaweza ona kama utani ila moja ya shirika ambalo wapo serious kwenye call centre ni TANESCO. Nimeshapiga karibia mara tatu na sikupata tabu

Very professional

Wakiweka na supply ya kueleweka itakuwa safi zaidi maana hapo ndipo kuna mtihani mzito
 
Habari, ndugu mteja.

Tunashukuru sana kwa ujumbe wako wa pongezi.

Kuhusu suala la mita, tafadhali fahamu kuwa ikiwa kila floor kwenye ghorofa ina mita yenye jina tofauti tofauti, kodi ya jengo itatozwa kwa kila mita. Ni kwasababu kwa utaratibu wa nyumba za ghorofa, makato ya huduma hufanyika kwa kila floor

Hata hivyo, ikiwa mita zote zina jina moja na zinakatwa kodi ya jengo, unashauriwa kutembelea ofisi za Halmashauri husika na kujaza fomu ya maombi ili makato ya kodi ya jengo yafanyike kupitia mita moja.

Asante. ^NI
Okay
Asante sana
Jina ni Moja.

Nitaenda offisi ya aridhi Manispaa.
 
Tanesco wapo vizuri sana wanajitambua wanajali wateja na kwenye changamoto wanatatua kwa wakati hongera nyingi kwao ila wakae na hao wanaopanga bei tushushiwe umeme ifike walau 150 au 100 kwa unit
Ndugu mteja,

Asante kwa pongezi, tumepokea na tumepokea na tutazidi kwenda hatua zaidi katika kukupatia huduma bora.

Tafadhali fahamu kuwa suala la bei ya manunuzi ya umeme hufanyiwa tathmini mara kwa mara na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwa kuzingatia gharama za uzalishaji na uendeshaji wa huduma. Baada ya kufanya tathmini na kujiridhisha, EWURA ndiyo yenye mamlaka ya kufanya uamuzi kuhusu mabadiliko ya bei za umeme.

Hata hivyo, tunathamini maoni yako, tumepokea kwa hatua zaidi. Upatikanaji wa umeme wa uhakika ni muhimu katika kuchochea shughuli za kiuchumi na maendeleo ya taifa.

Asante.^NI
 
Hakika, TANESCO 10/10 kwenye customer care. Ukishaongea nao, wanafuatilia kujua kama umefanikiwa kutatua changamoto yako.

Wapewe maua yao.
 
Kwa sasa tanesco wako level nyingine kwa huduma, hata mafundi wako smart hakuna wale wazee wa chochote...hizi initiatives zilianza kipindi cha makamba na maharage, sio hawa wajuzi

Nafikiri mashirika yote ya umma yaende retreat tanesco badala ya kwenda ulaya kupiga picha...
Ndugu mteja,

Tunashukuru kwa pongezi, tunaenda hatua zaidi katika kukupatia huduma bora.

Asante.^NI
 
Hakika, TANESCO 10/10 kwenye customer care. Ukishaongea nao, wanafuatilia kujua kama umefanikiwa kutatua changamoto yako.

Wapewe maua yao.
Ndugu mteja,

Tunashukuru kwa pongezi, tunaenda hatua zaidi katika kukupatia huduma bora.

Asante.^NI
 
Watu wanaweza ona kama utani ila moja ya shirika ambalo wapo serious kwenye call centre ni TANESCO. Nimeshapiga karibia mara tatu na sikupata tabu

Very professional

Wakiweka na supply ya kueleweka itakuwa safi zaidi maana hapo ndipo kuna mtihani mzito
Ndugu Mteja,

Asante sana kwa pongezi zako. Tunakuahidi kuendelea kuboresha huduma zetu ili uendelee kufurahia huduma bora.

Pia, tumepokea maoni yako kwa hatua zaidi.

Asante.^NI
 
Japokuwa sio rushwa lakini wahudumu wa tanesco wakija kunihudumia na jua kali hili huwa nawapa tips za elfu 10 10 hata wawe sita maana ofisi yangu kwa asilimia mia inahitaji umeme ndio niingize kipato
Ndugu Mteja,

Tunakushukuru kwa kuthamini juhudi za watumishi wetu katika kukuhudumia. Tunathamini mchango na ushirikiano wako.

Hata hivyo, tunakuhimiza kutumia njia rasmi za malipo kwa huduma zote zinazotolewa na TANESCO.

Asante.^NI
 
Kwa kweli TANESCO wanajitahidi sana, jamaa wapo active kupita kiasi. Juzi nilipiga 180 kutoa changamoto yangu fulani, aisee haikupita nusu saa jamaa hawa hapa. Nilijikuta natoa machozi ya furaha na kujiona nimethaminiwa sana. Taasisi zote za umma zikifanya kazi kama hawa jamaa, nadhani itapunguza sana manung'uniko ya wananchi.
Kwa hapa Marekani, Tanesco walivyo sharp nawafananisha na wale watoa huduma baada ya kupiga line 911.
 
Back
Top Bottom