Tandale Vs Msasani,Oysterbay na Masaki

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
TANDALE VS USHUANI

Kuna jamaa mmoja huku Tandale alisikia tu kwamba kuna jamaa anamchukulia mke wake, yaani kila anaposepa asubuhi saa tisa alfajiri kwenda kuchukua daladala, mwanamke anaingiza mwanaume kisiri ambaye analala naye mpaka asubuhi.

Hizo zilikuwa tetesi kwake na hata alipoambiwa, hakusema kitu, alibaki kimya huku akianza kufuatilia kimyakimya. Wala haikuchukua zaidi ya wiki, huku akiwa ameondoka, jirani yake akampigia simu na kumwambia kwamba kama kawaida jamaa amezama chumbani.

Jamaa hakutaka kwenda kwenye kibarua chake, alfajiri hiyohiyo akarudi nyumbani kwake, akaenda dirishani, akamsikia mke wake akiongea na jamaa huku wakicheka, wala hazikupita dakika nyingi, kitanda kikaanza kusikika kikilalamika na miguno ya mahaba.

Jamaa ilimuuma lakini hakuwa na jinsi, hakutaka kuvamia, alichokifanya, akamfuata balozi wa nyumba kumi na kumwambia waelekee nyumbani kwake, wakaelekea huko.

Jamaa akaona hiyo haitoshi, akawaamsha mpaka wapangaji na kuwaambia kwamba chumbani kwake kulikuwa na mtu anamlia mke wake, wapangaji walivyokuwa washakunaku, wakaenda nje ya mlango, kila mtu akawa na hamu ya kufuamania.

Mlango ukagongwa, mke alipouliza nani, jamaa akasema mimi mumeo, fungua mlango. Ndani ilikuwa ni balaa, mke mapigo ya moyo yanamdunda, presha imepanda huku msela naye akimlalamikia Mungu kwa nini alimpa baba mwenye nyumba wazo la kuweka ‘silingi bodi’.

Baada ya mlango kugongwa sana, mke akafungua na jamaa akamfumania mgoni wake. Kitu kilichowashangaza majirani na hata balozi, jamaa hakumpiga mgoni wala mkewe, alichokifanya ni kumpekua mifukoni mgoni wake, akamkuta na shilingi elfu tano, jamaa akamwambia ondoka.
Jamaa akamwambia mke wake kwamba amemsamehe ila asirudie.
Kuanzia siku hiyo, kila mke akiweka chakula mezani kwa ajili ya kula, mume anachukua ile shilingi elfu tano na kuiweka mezani na kusema huyu ni yule mgoni wangu niliyechangia naye mke, kwa hiyo naye inabidi awe mezani tule wote.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya kila siku, muda wa chakula mezani, jamaa anachukua elfu tano ileile na kuiweka mezani, mke akiiangalia ile hela na akikumbuka maneno ya mume wake, moyo ulikuwa ukimuuma mno, akaendelea kukaa na majuto moyoni na mpaka leo hii, bado staili hiyohiyo ya shulingi elfu tano inaendelea.
****
Achana na hicho, kilikuwa kionjo tu sasa tuingie kwenye ishu yenyewe,
Nadhani watu wote duniani wanajua kwamba nimezaliwa Tandale, si ndiyoeee? Nani hajui kwamba Tandale ilikuwa noma kwa wizi wa kukabana? Nani alikuwa hajui kwamba Tandale, hasa kipindi cha zamani ukisikia mwanafunzi kamaliza kidato cha nne anaonekana kasoma sana? Nani alikuwa hajui kwamba familia nyingi za Tandale zilikuwa zikila mlo mara moja kwa siku? Nani alikuwa hafahamu kwamba majambazi wengi walikuwa wakitoka Tandale na fujo za hapa na pale?

Kuna mengi yalikuwa yakitokea zamani lakini kwa sasa yamekwisha. Leo hii Tandale kunajengwa maghorofa, leo hii Tandale watu hawapigani roba, leo hii Tandale watu wanasoma mpaka chuo halafu inakuwa kawaida sana, leo hii Tandale inatoa wanamuziki wanaoitikisa Tanzania, leo hii Tandale inatoa watu wengi wenye vipaji, leo hii Wazungu kutoka Marekani wanakuja Tandale na kujenga madaraja, hakika ni mabadiliko ya kasi sana.

Tandale iko poa sana. Nakumbuka miezi kadhaa iliyopita nilikwenda Msasani, nilikuwa kwenye kazi zangu za uandishi wa habari kipindi hicho. Nikaingia kwenye mtaa ambao ukanifanya nimuulize jamaa niliyemkuta kwamba ule ulikuwa mtaa gani, akaniambia ni Msasani, nikaona hapana, Msasani ninayoisikia haiwezi kuwa hivi, nikauliza kwa mtu mwingine akasema kwamba ni Msasani.

Ilikuwa ni choka mbaya. Unajua mpaka mtoto wa Tandale anafika mtaa halafu anashangaa jinsi ulivyo na kuuliza basi jua huo umekaa vibaya mno. Nikauliza swali moja muhimu kwamba siku za mvua kubwa inakuwaje, akaniambia ni balaa, sehemu inajaa maji kama mto.

Kiukweli nimewahi kuona sehemu hohehae lakini kule Msasani nilipofika ilikuwa balaa sana, ilikuwa ni zaidi ya Tandale. Swali pekee nililojiuliza, kwa nini watu wanaisema sana Tandale na wakati huku Msasani, ni bora ya Tandale?

Nikaachana na hapo, wiki iliyopita tu nilikwenda Mikocheni, sifahamu kama ni A au B. Nilipofika kule, kulikuwa kama Tandale, sikuchoka kuuliza, kwa kuwa nilikuwa na mwenyeji wangu, nikamuuliza ile ilikuwa wapi, akaniambia Mikocheni.

Nilishangaa mno, inakuwaje Mikocheni inakuwa hivi kama Tandale lakini watu bado wanaisakama Tandale? Nikasema labda kwa sababu Mpoki anaitaja sana Tandale hasa kwa Mtogole. Nikasema kwamba inawezekana naye Mpoki haifahamu Tandale, yeye anaizungumzia Tandale ya mwaka 1999 na si hii ya 2014.

Labda hajui kwamba bosi wa Tanesco anaishi Tandale, labda hajui kwamba Mbunge wa Kinondoni naye anakaribia kuja Tandale, lakini inawezekana hajui kwamba kwa Mtogole kumejengwa lodge nyingi ambazo kwa siku mtu hulipia elfu arobaini kulala, labda hajui mengi kuhusu Tandale na ndiyo maana anakaa kuiponda Tandale. Mbali na hiyo, hapohapo kwa Mtogole kuna maduka makubwa ya nguo, ukiingia ni kama upo katika maduka ya sehemu nyingine, fulana elfu thelathini kwenda juu na kila mwezi mzigo mpya unaletwa.

Mbali na hivyo, haohao wanawasifia wanamuziki wao kwa kuimba vizuri, hivi hawajui wanamuziki wengi huwa wanakwenda Tandale kurekodi kwa Maneke katika Studio ya AM Record?

Mgeni anakuja kunitembelea, akifika mtaani kwetu, namwambia kwamba hii unaiyoiona ndiyo Tandale, anabaki akishangaa kwamba inakuwaje Tandale anayoisikia ipo hivi? Mbona haoni vile vitu alivyokuwa akivisikia? Mbona alikuwa akitembea na simu yake aina ya Samsung S4 toka kituoni mpaka home na hakukabwa? Kwa nini na wakati alijua Tandale ni uswahili na kuna wezi?

Kuna mwanamke alikuja na kutuuliza hivi...

MDADA: Samahani, hivi nilikuwa nauliza msiba wa mzee (Anamtaja jina) ni wapi hapa Sinza?

SISI: Dada, hapa siyo Sinza, wewe umetoka wapi?

MDADA: Gongo la Mboto.

SISI: Hapa siyo Sinza, hapa ni Tandale.

MDADA: (Akashtuka) Tandale! Hapa Tandale! Mmmh! Mbona nilivyosikia na jinsi kulivyo hakupo hivyo?

SISI: Ndiyo hivyo. Shuka na hii barabara, hapo kituoni chukua gari uendelee na safari mpaka Sinza, si mbali sana.

Mdada akasepetua zake.

TANDALE kupo poa sana, na vyumba vimepanda bei, kutoka elfu 20 kwa mwezi mpaka 50 kwa baadhi ya nyumba.

Huwa sipendi kusikia mtu akiidiss Tandale kwa sababu kila lisemwalo, daah! Mbona halipo hivyo. Tena nzuri kuliko zote, siku hizi hadi mabinti wa Kiarabu wapo......Chezea Tandale wewe!!!

MTUACHE TULALE SASA NA TANDALE YETU!!!
 
Dar hakuna sehemu ambayo haijaendelea.Manzese Kuna mahoteli ya uhakika .Wazungu na wachina hufikia huko kwa wingi ziko Hadi hoteli za kimataifa manzese ambazo hata masaki,osyterbay na msasani hazipo
 
dar ni mji wa ajabu,mfano masaki kuna vibanda vya mabati vya kuuza mihogo.na gomzi kuna majengo smart sana tu.
 
Back
Top Bottom