TANCOAL watekeleza agizo la Waziri Biteko, wakabidhi tani 30 za makaa ya mawe

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1586149605395.png


Kampuni ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe Tancoal imetekekeleza ombi la waziri wa madini Doto Biteko kwa kukabidhi tani 30 za makaa ya mawe,juu ya kumsaidia mzee Reuben Mtitu maarufu kwa jina la mzee Kisangani wa Kijiji cha Mkiu wilayani Ludewa Mkoani Njombe kutokana na changamoto ya upatikanaji wa makaa hayo kwa ajili ya kuyeyusha chuma ili kutengeneza bidhaa zake kama visu na nyundo.

Akizungumza wakati akikabidhi tani 30 za Lori la makaa yam awe,afisa utawala na mahusiano ya hamii wa kampuni ya Tancoal Richard Nditi,amesema kwa vikao tofauti kwa kushirikiana na waziri wa madini Doto Biteko wamepanga kumfikishia mzee huyo tani 60 kwa mwaka.

“Kampuni imepanga kukuletea tani 60 kwa mwaka kwa hiyo tumeleta tani hizi 30 utazitumia na wakati wowote tutaleta tani 30 nyingine ili kukunga mkono kwenye shughuli zako hizi,na tunaamini kwa kukuwezesha nishati hii unaweza ukaongeza wigo wa shughuli zako na kuongeza fursa za ajira kwa vijana katika eneo hili la Ludewa”alisema Richard

Maganga Laurence ni afisa mradi wa shirika la taifa la Maendeleo (NDC) ambaye pia ni mwakilishi wa shirika kwenye mradi wa makaa yam awe Ngaka (Tancoal),kwa niaba ya mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya taifa amesema wamekabidhi tani 30 kwa sasa na baadaye tani nyingine 30 kukamilisha tani 60 kwa kuwa serikali kwa kushirikiana na Tancoal ni kuwasaidia wajasiriamali wadogo.

“Mikakati iliyopo mojawapo ni kudumisha mahusiano na jamii,hivyo lilivyokuja ombi la mzee Mtitu kwa Tancoal na NDC kwa pamoja tumeona tulete tani hizi,na vile vile ninampongeza mzee mtitu alivyopata maono ya kuanzisha kiwanda hiki”alisema Maganga Laurence

Reuben Mtitu maarufu kama Mzee Kisangani anayemiliki mradi wa kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa zinazotokana na chuma,ameishukuru serikali na kampuni hiyo kwa kuwa mkaa ndio hitaji kubwa kwake na ameahidi kuingia katika utekelezaji kwa nguvu zote.

“Madhumuni ya waziri alivyotutembelea ni kuona mradi unakua endelevu,napenda kuwahakikishia Tancoal kwa kushirikiana na serikali sisi tunaingia kwenye utekeleaji wa kuzalisha chuma ili tuweze kujikimu sisi wenyewe lakini pia kwa manufaa ya taifa”alisema Mzee Reuben Mtitu

Nicolaus Mgaya ni Diwani wa kata ya Lubonde na Verdiana Mnzeru ni mtendaji wa kata hiyo wameishukuru pia serikali kwa kumuwezesha mzee huyo kwa kuwa shughuli anazofanya ni kwa manufaa ya kata,wilaya na taifa kwa ujumla hivyo wememtaka mzee Kisangani kuutumia vema mkaa huo ipasavyo pamoja na kuwezesha ajira kwa vijana.

Tancoal na Ndc wamefikisha mkaa huo kutokana ombi la waziri Doto Biteko alipofika machi 14 2020 wilayani Ludewa mkoani Njombe alipotembelea mradi wa kiwanda cha kuzalisha zana mbali mbali zinazotokana na madini ya chuma kinachomilikiwa na Mzee Kisangani na kukutana na changamoto ya makaa ya mawe anayokumbana nayo mzee huyo hatu iliyokuwa ikimlazimu kufanya kazi wakati tu anapopata malighafi hiyo kwa kuvizia na kuokota makaa yanayodondoshwa barabarani wakati yakisafirishwa.
 
Back
Top Bottom