TAMWA yakemea dhuluma za kingono kwa Watoto

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Ripoti ya jeshi la polisi iliyotolewa mwaka 2020 inataja miongoni mwa ukatili dhidi ya Watoto wa kiume na wa kike ulioripotiwa kwa kiwango kikubwa kuwa ni dhuluma za kingono ambapo katika mwaka wa 2020 kuliripotiwa visa 7263 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo vilirekodiwa visa 5803, hii ikiwa ni sawa na visa 615 kwa mwezi.

Ukatili huu haukubaliki! Tuchukue hatua!

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Mimba za mapema kwa wasichana wenye umri wa kuanzia miaka 10-19 huchagiza maradhi kama kifafa cha mimba, maambukizi kwenye mfumo wa uzazi na watoto kuzaliwa na uzito mdogo au kuzaliwa kabla ya wakati.

Tuungane kupinga mimba za mapema kwa kuwalinda na kuwapa haki watoto.
 
Back
Top Bottom