Anko Sam
JF-Expert Member
- Jun 30, 2010
- 3,254
- 906
TAMKO LA WADAU (WANACHAMA WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII) WA MIGODI NA SEKTA BINAFSI KUHUSU SHERIA No 5 YA HIFADHI YA JAMII KAMA ILVYOFANYIWA MAREKEBISHO MWEZI APRIL 2012
- Kamati haikuwa huru kwani haikundwa na wawakilishi stahiki wote walitoka kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii,
- Kamati ilitaka kukutana na waakilishi wachache tu wa wafanyakazi ambao nao walipata ujumbe ndani ya muda mfupi sana. Je wawakilishi hawa walikuwa wanpelekaa mawazo ya Watu gani ikiwa hawakupata nafasi hata ya kukutana na Wafanyakazi wenzao?
- Kikao chenyewe kililenga kufanywa kiusiri sana, kilipangwa kufanyika hotelini bila kuwepo wandishi wa habari. Sheria inayogusa hatima na maisha ya watanzania inafanywaje kwa siri namna hiyo tena ikipelekea kuwa ni azimio la Bunge?
- Uwakilishi wa wafanyakazi wa migoni pamoja makampuni mengine haukutimia lakini kamati ikalazimisha kuendelea na kikao, na cha kushangaza baadhi ya wawakilishi walipata mwaliko dakika 15 kabla ya kikao!
2. Kutofurahishwa na usiri unaoonekana katika suala ambalo lina maslahi makubwa kwa watanzania walio wengi, Tunataka vyombo vya habari vihusishwe kwa kiasi kikubwa katika hatua zote ili kujenga taswira ya uwazi katika suala hili.
3. Maboresho yote yanayokusudiwa kufanywa yahakikishe kipengele kinachozuia mafao ya kujitoa kinafutwa kabisa katika sheria hiyo na mwanachama alipwe mafao yake yote pindi ajira yake inapokoma kwa sababu yoyote ile.
4. Muda wa kulipwa mafao uwe mfupi na usiozidi siku ishirini na moja( 21) tangu siku ile mwanachama anapofungua faili lake la madai.
5. Wale wote walioathirika na sheria hii mpaka sasa ( walioacha au kuachishwa kazi ) walipwe mafao yao mara moja kwani wanateseka bila sababu za msingi,wakati pesa yao ipo mikononi mwa serikali bila hata ridhaa yao, katika hili tunamtaka waziri Gaudensia Kabaka atoe waraka maalum kwa SSRA wafute mara moja waraka wao wa zuio la Wafanyakazi kuchukua Pesa zao kwani wanaendelea kuteseka bila sababu.
6. Wadau wameonyeshwa kushangazwa kwao kwa sheria kuanza kutumika bila hata kanuni zake kutengenezwa , uharaka huu una siri gani ndani yake? Ziko sheria kadha wa kadha zilizotungwa na hazijaanza kutumika kwa sababu kanuni zake hazijaandaliwa, mfano, Sheria inayomlinda mtoto ilitungwa mwaka 2009 lakini mpaka leo haijaanza kutumika, Workmans compensation act 2008, haijaanza kutumika,, na hata sheria ya kazi na mahusiano kazini ilitungwa mwaka 2004 lakini ikaanza kutumika rasmi 2007, yote hayo yanafanyika ili kutoa fursa ya taratibu za kikanuni kuwekwa /kutengenezwa na hivyo kurahisisha utumikaji wa sheria yenyewe. Hivyo basi kwa mlolongo huu,Wafanyakazi walahoi wa Nchi hii wanaamini kwamba sheria hii haina nia Njema kabisa kwa mstakabali wa maisha yao na vizazi vyao ila ipo kwa maslahi ya Watawala. Na kama ingekuwa na maslahi hata wabunge pia walipaswa kuwemo.
7. Tunachukua fursa hii kuendelea kulaani kitendo cha mkurugenzi wa SSRA kulazimisha kuanza kutumia sheria hii pamoja na mapungufu yote yaliyojitoza kama kukosekana kwa kanuni za matumizi ya sheria hii na kusababisha usumbufu kwa wanachama ambao kimsingi ndiyo wamiliki wa fedha hizo. Kwa Mapungufu haya bado Wafanyakazi wa Migodi na Sekta binafsi tunamtaka Mkurugenzi wa SSRA Irene Isaka na Waziri wake wa Kazi Gaudensia Kabaka wajiuzuru mara moja kwa kushindwa kufanya kazi kwa Maslahi ya Wafanyakazi walalahoi wa Watanzania.
8. Tunapenda kusisitiza kwa uzito unaostahili kuwa kuwa kwa kuwa Wabunge wa Tanzania wamekuwa mstari wa mbele kutetea hoja na sheria zinazogusa maslahi yao kwa nguvu na uwezo wao wote, Mfano kuhakikisha kuwa sheria hii ya fao la kujitoa haiwahusu wao, yaani Mbunge akimaliza muda wake anapewa stahiki zake zote bila kusubili miaka 55 hadi 60, Wafanyakazi tunaahidi kwa uaminifu wote kwamba mbunge yeyote toka Chama chochote atakaye onekana kuzia Wafanyakazi kuchukua Pesa zao zote , tutamhesabu kuwa ni adui wa haki za wafanyakazi na hatutasita kuhamasisha kukataliwa kwake katika jimbo analotoka. Tutaunganisha nguvu zetu ili kuhakikisha asichaguliwe tena kwani hana msaada kwa jamii ya watanzania ambao ni wahanga wa sheria hii.
9. Tunataka kuiarifu kamati ya ukusanyaji maoni juu ya marekebisho ya sheria hii kuwa elimu yoyote kuhusu sheria hii haitakubalika iwapo fao la kujitoa halitarejeshwa kama ilivyokuwa awali. Hatuko tayari kupokea elimu yoyote kuhusiana na suala hili ambayo inakusudia kututoa kwenye lengo mahususi. Na kama bado wanahitaji maoni ni vyema wazungukie wafanyakazi wote Migodini badala ya kuita watu wachache Mahotelini.
10. Mwisho Tunataka kuionya Serikali kwamba kama haki yetu hii ya fao la kujitoa na kupewa faida kwa hela zetu zinazowekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na kufanyiwa biashara, isiporudishwa mara moja kupitia marekebisho ya sheria hii kupitia Bunge lijalo, Wafanyakazi wote wa Migodini tunaahidi kwamba yale yaliyoonekana kwa Wafanyakzi wa Mgodi wa Platinum, Malikana Afrika Kusini yanakwenda kutokea Nchini kwetu mara 10 yake. Wafanyakazi wote tutahakikisha kwamba tunahamasishana wote pamoja na familia zetu na ndugu zetu na Watanzania wenzetu wanaoguswa na uonevu huu,kuhamasisha Migomo migodini na kuhakikisha shughuli zote za Migodi Nchini zinasimama hadi pale haki yetu itakaporudishwa.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wafanyakazi.
Asanteni sana kwa kunisikiliza
Mwenyekiti wa Kamati Teule
NOTE: Wafanyakazi wote na waathirika wa sheria hii, wafanyakazi viwandani hasa wakiwemo wa Migodini kama; Bully, North Mara, Resolute, Tulawaka, Wiliamson Diamond, Buzwagi, Kabanga Nickel na El-Hilary. Tuwasiliane na wadau wa GGM kwa Mikakati ya Kwenda Bungeni October 2012.