Tamko la waislam dhidi ya kauli za maaskofu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la waislam dhidi ya kauli za maaskofu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maarifa, Jan 27, 2011.

 1. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,878
  Likes Received: 1,048
  Trophy Points: 280
  Jamani mie nimetumiwa e mail tu! just to review whats writtten. Msinihukumu bali nanyi fanyeni review zenu. Angalizo just review as a great thinker na sio mshabiki tu. Hapo tutakuwa sawa. Je wewe unasemaje?

  Habari yenyewe hii hapa!!
  TAMKO LA WAISLAMU DHIDI YA KAULI ZA MAASKOFU
  Utangulizi
  Oktoba 31, 2010 Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu ambapo wananchi walipata fursa
  ya kumchagua Rais, wabunge pamoja na madiwani. Katika uchaguzi huo, Watanzania
  kwa ujumla wao walikichagua Chama cha Mapinduzi, CCM, kuongoza tena nchi kwa
  kipindi kingine cha miaka mitano.
  Hata hivyo, wakati wananchi wakiamini kwamba wanaongozwa na watu waliowapigia
  kura, matukio yanayoendelea hivi sasa yanaashiria serikali kutelekeza majukumu
  yake na kuwaacha maaskofu wakielekeza nchi wanakotaka.
  Itakumbukwa kwamba awali kabla ya uchaguzi mkuu maaskofu walikuwa wametoa Ilani
  yao ya uchaguzi bila kueleza kipi chama chao kitakachosimamia na kutekeleza
  Ilani hiyo. Baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala, CCM, walishabikia
  Ilani hiyo na kuwatetea maaskofu. Kwa hakika taarifa za vyombo vya habari
  zilifahamisha kwamba baadhi ya watendaji waandamizi ndani ya serikali
  walishiriki katika kuandaa Ilani hiyo.
  Ilipofika wakati wa kampeni hadi kuingia siku ya kupiga kura, ilikuwa imedhihiri
  kipi kilikuwa chama cha maaskofu ambacho walitarajia kitekeleze Ilani yao.
  Haikuwa tena jambo la siri kwani walisimama wazi wazi kuwaelekeza waumini wao
  wampigie nani kura. Na katika juhudi zao za kutaka wafuasi wao wawaelewe vizuri,
  maaskofu walithubutu hata kuweka kando mafundisho ya Biblia yao juu ya masuala
  ya uzinzi wakawahimiza waumini kumpigia kura mtu wanayemtaka bila kujali kwamba
  anakabiliwa na kashfa ya kupora mke wa mtu. Waliwaambia wasihangaike na maisha
  binafsi ya ndoa ya mgombea.
  Hata hivyo, matokeo ya kura yalitoa majibu kwamba Watanzania walikuwa wameikataa
  Ilani ya Maaskofu.
  Waislamu tumelazimika kukutana na kutoa tamko hili kwa sababu matukio
  yanayotokea hivi sasa yanaonesha kuwa wale ambao Watanzania walikataa kuwapa
  uongozi na Ilani yao iliyoandaliwa na maaskofu, ndio sasa wanaielekeza nchi pa
  kwenda huku viongozi wa CCM na serikali wakijitahidi kadiri ya uwezo wao
  kunyenyekea kwa maaskofu hao.
  Tumeona na tumemsikia Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda
  akihangaika kuwapigia magoti na kuwaomba radhi maaskofu kule Sumbawanga.
  Tumesikia jinsi viongozi wanaojaribu kuwaambia maaskofu kwamba kama wanataka
  kuingia katika siasa wavue majoho na vyeo vyao vya kikanisa kama Padiri mwenzao
  waliyekuwa wakimpigania kuingia Ikulu, wanavyokemewa na kutakiwa wawaombe radhi
  maaskofu hao.
  Lililo baya zaidi maaskofu walioshindwa kuwashawishi wananchi waipokee na
  kukubali Ilani yao, wamekuja na kampeni za kuchochea uasi kwa serikali iliyopo
  madarakani. Lakini pamoja na hali hiyo, viongozi wa CCM na serikali wamebaki
  wanagwaya. Hakuna aliyeweza kupata ujasiri wa kukemea hali hii. Kinyume chake
  Waziri Mkuu na Mzee John Samwel Malecela wanahangaika huku na kule wakiwapigia
  magoti maaskofu hao na kuwakemea wanaothubutu kuwakosoa.
  Hali kama hii ni hatari kwa usalama na utulivu wa nchi. Ni hali ya kuchochea
  udini na kuweka ombwe la uongozi wa kisiasa ambao utazua balaa. Waislamu
  hatuwezi kukubali hali hii. Kwa hiyo, ama CCM na serikali vitekeleze wajibu wao
  wa kuongoza au kama wanaona hawawezi, basi waseme rasmi ili Maaskofu na wengine
  wenye Ilani zao za uchaguzi waingie tena ulingoni kuomba ridhaa ya Watanzania
  kuongoza nchi kuliko kuishi katika hiki kiini macho ambapo maaskofu na mawakala
  wao ndani ya serikali wameachwa waikokote nchi wanakotaka.
  Kiini cha Hali hii ya Kisiasa
  Hali hii ya kisiasa tunayoishuhudia leo nchini mwetu ni matunda ya mbegu
  liliyopandwa na kupaliliwa kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Wakoloni walikuwa
  na kanuni yao waliyoiita divide et impero yaani wagawe ili uwatawale. Huko
  Rwanda wakoloni waliwagawa wananchi kwa misingi ya kikabila. Watusi ambao ni
  watawala wapewe elimu ya juu na wanfundishwe kwa Kifaransa, na Wahutu ambao ni
  watawaliwa wapewe elimu duni na wafundishwe kwa Kiswahili. Ubaguzi huo wa
  kuwagawa raia wa nchi moja ulipandikiza sumu iliyokuja kusababisha Wanyarwanda
  kuuana.

  Hapa kwetu wakoloni walitugawa kwa misingi ya dini. Kabla ya uhuru wa
  Tanganyika, wakoloni kwa kushirikiana na makanisa waliwaona Waislamu kama ni
  mahasimu wao kidini na kisiasa. Na kwa sababu hiyo serikali za kikoloni zikaweka
  mikakati maalum ya kuwakandamiza Waislamu katika maeneo matatu: kwanza kuwawekea
  vikwazo katika kutangaza dini yao ili wasiongezeke; pili kuwabana katika elimu
  na ili kuhakikisha kuwa Waislamu wanabanwa jukumu la kuwaelimisha Waafrika
  likawekwa mikononi mwa makanisa na kazi ya serikali ni kuzigharimia tu shule
  hizo. Lengo likiwa ni kuwabatiza Waislamu wachache watakaoruhusiwa kusoma, na
  tatu kuwabana katika ajira serikalini kwa sababu makanisa yote yalisisitiza kuwa
  kuwaajiri Waislamu serikalini ni kusaidia kuenea kwa Uislamu..
  Kwa kuwa ubaguzi huo haukuwa na kificho chochote, Waislamu wengi walijitokeza
  kupambana na ukoloni kwa matarajio kuwa serikali huru itaondosha chuki na uadui
  huo dhidi ya Waislamu. Lakini msiba mkuu wa taifa hili ni kwamba kinyume chake,
  baada ya uhuru msimamo ukawa ni ule ule wa kuwaona Waislamu kuwa ni maadui wa
  kupigwa vita na mikakati ya kuwabana Waislamu katika maeneo yale matatu
  ikaimarishwa zaidi wakati wa utawala wa Nyerere. Kuanzia 1957 mkakati uliopangwa
  na Kanisa Katoliki ukawa ni kuhakikisha kuwa nafasi zote muhimu za uongozi na
  serikali zinashikwa na wao. [Taz. Confidential Diary – Tanganyika, March-April
  1957, uk. 3-4 Maryknoll Central Archives, New York ]. Na ni mkakati huu ndio
  ambao Mwalimu Nyerere aliokuwa akimuhakikishia Askofu Rweyemamu mwaka 1970 kuwa
  anatumia mamlaka yake kama Rais na kama kiongozi wa TANU kuhakikisha kuwa anatoa
  upendeleo maalum kwa Wakristo ili wasimamie sera za Chama. Na kwamba amemteua
  padiri katika nafasi nyeti ya Chama si kwa sababu anajua siasa bali kwa sababu
  ni Mkristo safi. Lakini Nyerere huyo huyo akisimama hadharani alijidai kukemea
  udini. Na kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuliimarisha kanisa na kuwadhoofisha
  Waislamu, leo Kanisa lake limo katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa ni
  Mtakatifu!
  Sivalon anaarifu katika kitabu chake kuwa mara baada ya uhuru Kanisa katoliki
  liliwahamasisha Wakristo wote na hasa watendaji wa serikali juu ya hatari ya
  Ukomunisti na Uislamu na walikusanya nguvu zao zote katika kukabiliana na maadui
  hao.
  Matokeo ya Hujuma Hizo
  Matokeo ya hujuma hizo za kichinichini ni kwamba katika sura ya nje na katika
  propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na kisiwa
  cha amani. Lakini uhalisia wa mambo ni kuwa Tanzania ni nchi yenye jamii kubwa
  mbili. Jamii ya Wakristo wanaopewa msaada, upendeleo, ulinzi na heshima, na
  jamii ya Waislamu ambao wanachukiwa, kudharauliwa na kudhoofishwa na serikali
  kabla na baada ya Uhuru. Ifuatayo ni mifano michache tu ya baadhi ya hujuma hizo
  baada ya Uhuru.
  (1) Mwaka 1963 katika Barua ya Kichungaji, Kanisa Katoliki lilisema Waislamu
  walikuwa wanajenga umoja na mshikamano miongoni mwao, jambo ambalo ni “hatari
  kubwa kwa hatima ya Wakristo wetu” na Sivalon anabainisha kuwa Wakristo
  walimwomba Nyerere awasaidie kuvuruga umoja huo wa Waislamu. Ndio sababu ya
  Nyerere kutumia dola kuiparaganya EAMWS. Kwa kuwa Waislamu ni jamii inayotakiwa
  kuwa dhalili, hawatakiwi kuwa na umoja. Ndio maana tangu wakati wa Nyerere hadi
  leo, uchaguzi wa viongozi wa Waislamu husimamiwa na vyombo vya dola. Nia ikiwa
  ni kutokuwapa Waislamu uhuru wa kuwachagua viongozi wao. Katika taifa moja haki
  hiyo ni ya Wakristo peke yao. Sote ni mashahidi kuwa mwaka 1994 serikali
  ilimwagiza Naibu Waziri Mkuu Mh. Augustino L. Mrema kuhakikisha kuwa Bakwata
  inapitisha katiba mpya inayotakiwa na serikali. Na Maaskofu wakachangia gharama.
  Waislamu ni maadui kidini na kisiasa, lazima wadhibitiwe.

  (2) Mwaka 1992 Serikali ya Tanzania ilitiliana saini Makubaliano ya Itifaki
  rasmi na Makanisa ya TEC na CCT. Kwa mujibu wa makubaliano hayo ambayo yalitiwa
  saini na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye wakati huo alikuwa
  Mh. Edward Lowasa serikali imewajibishwa pamoja na mambo mengine, kutenga nafasi
  za masomo kwenye vyuo vyake vya Ualimu mahsusi kwa ajili ya wanafunzi
  wanaopangwa kufundisha katika shule za Kanisa; pia kutoa ruzuku ya kuendeshea
  taasisi za Makanisa. Kuanzia 1992 hadi leo serikali imetoa mabilioni ya kodi za
  wananchi kwa Makanisa. Katika kipindi chote hicho Waislamu wamepinga ubaguzi
  huo. Lakini kwa kuwa lengo ni kuwaimarisha Wakristo ambao ni jamii inayotakiwa
  kupewa nguvu zaidi dhidi ya jamii ya Waislamu ambao wanatizamwa kama maadui,
  serikali imeyapuuza malalamiko ya Waislamu. Lakini propaganda zinaendelea kuwa
  Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na ni kisiwa cha amani.
  (3) Waislamu wameiomba serikali kujiunga na OIC kama njia mojawapo
  itakayowezesha nchi yetu kupata misaada itakayotumika kuinua hali za Waislamu
  ambao wameachwa nyuma sana katika elimu na uchumi. Makanisa yote kwa kauli moja
  yamepinga kwa nguvu zao zote pendekezo hilo. Sababu ya kupinga kwao ni kuwa
  mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanadhoofishwa katika kila hali, na
  ni makosa makubwa kuwaimarisha kiuchumi au kielimu maadui hao. Serikali
  ilipofanya utafiti wake wa kina ikajiridhisha kuwa kujiunga na OIC kuna manufaa
  na hakuna madhara yoyote. Na Mh. Bernard Membe alitamka hilo Bungeni. Mara
  akaitwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Cardinali
  Pengo na kukumbushwa mkakati wa kuwadhoofisha Waislamu. Msimamo wa serikali
  ukabadilika. Lakini propaganda za kuwazuga Waislamu zinasema Watanzania wote ni
  kitu kimoja na nchi hii haina ubaguzi!
  (4) Kwa kuwa tangu wakati wa ukoloni hadi leo mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa
  Waislamu wanaminywa kadiri iwezekanavyo katika nafasi za uongozi na ajira, ndio
  maana hadi leo, miaka 50 baada ya Uhuru Waislamu ni wachache sana katika nafasi
  zote za uongozi na ajira katika sehemu muhimu serikalini na katika vyombo muhimu
  vya maamuzi. Kisingizio kinachotolewa ni kuwa Waislamu hawataki kusoma. Lakini
  ukitazama orodha ya Wakuu wa Wilaya wote walioteuliwa na sifa zao, utaona
  dhahiri kuwa wapo Waislamu wengi wenye sifa bora zaidi ambao wangestahili kuwa
  ma-DC. Waislamu hawateliwi kwa sababu mkakati uliopo ni kuwatenga Waislamu na
  ikiwezekana kuwaondosha kabisa katika sehemu muhimu za uongozi, kwa sababu kama
  wao hawajui ukweli ni kwamba hawatakiwi kushika nafasi zozote muhimu za uongozi
  au ajira. Ndio maana asilimia 75 ya Ma-DC wote ni Wakristo na karibu wasimamizi
  wote wa Uchaguzi katika wilaya ni Wakristo. Wabunge asilimia 75 pia ni Wakristo,
  na hali ni hiyo hiyo katika Vitengo vya serikali na Mashirika ya uma. Ndio maana
  hakuonekani tatizo lolote pale taasisi yote inapokuwa na Wakristo watupu. Na
  kelele nyingi maadui wa serikali na Kanisa wanapopewa nafasi hata kama wana
  uwezo kiasi gani. Katika sura ya nje Tanzania ni taifa moja, katika uhalisia
  wake ni kuna mataifa mawili, moja nyonge na jingine lenye nguvu.
  (5) Kwa kuwa Waislamu wanahesabiwa kuwa ni maadui, ule mkakati uliowekwa na
  wakoloni wa kuwawekea vikwazo Waislamu katika kutangaza dini yao unaendelea hadi
  leo. Ipo mifano mingi sana ya Waislamu kukamatwa, kutiwa ndani na kunyanyaswa na
  vyombo vya dola kwa sababu tu ya kulingania hadharani dini yao. Kwa kuwa
  Waislamu ni maadui, basi ni muhimu kuhakikisha kuwa hawaongezeki. Wakristo
  wanayo haki ya kuitisha mkutano wa hadhara na kutangaza kuwa Yesu ni Mungu. Wao
  ni jamii inayostahiki ulinzi wa dola. Lakini pindi Mwislamu atakaposema
  hadharani kuwa Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi siyo Yesu mwana wa
  Mariamu atakuwa amekashifu dini ya dola na atakamatwa na kubughudhiwa. Lakini
  kipropaganda, Tanzania ni nchi moja na inafuata katiba moja. Lakini uhalisia ni
  tofauti.
  (6) Msimamo wa serikali na makanisa kuhusiana na mauaji ya Waislamu katika
  msikiti wa Mwembechai ni kielelezo kingine cha ukweli kuwa Tanzania ni
  mkusanyiko wa jamii mbili zenye haki na hadhi tofauti katika taifa moja. Kwa
  kushinikizwa na Maaskofu serikali iliwauwa Waislamu watatu Mwembechai pasi na
  hatia yoyote. Waislamu waliiomba Mahaka, Bunge na hata Rais aunde Tume ya
  uchunguzi. Mihimili yote ya dola ilikataa. Kiongozi wa Kanisa Katoliki akenda
  mbali zaidi. Akahalalisha mauaji hayo. Kwa sababu waliouliwa ni wale maadui wa
  ile jamii nyoge isiyotakiwa kustawi. Lakini alipouliwa mbwa “Imigresheni” mwaka
  huo huo wa 1998, Jaji Mkuu wa wakati huo Mh. Francis Nyalali aliamuru uchunguzi
  wa kuuliwa mbwa huyo na hakimu akaadhibiwa. Jaji Mkuu alichukua uamuzi huo bila
  kuombwa na mtu. Lakini wale waliowauwa Waislamu walipongezwa na kupandishwa
  vyeo. Uhasama wa serikali na makanisa dhidi ya jamii ya Waislamu ni wa kiwango
  cha kutisha. Msimamo ukawa huo huo walipouliwa Waislamu Unguja na Pemba 2001 kwa
  kuandamana kudai Katiba Mpya. Lakini kipropaganda tunaambiwa Watanzania wote
  wanahaki sawa.
  (7) Rais wa Marekani George W. Bush alipotangaza Vita vya Msalaba dhidi ya
  Waislamu mwaka 2001, serikali ya Tanzania ikapata uhalali zaidi wa kuzidi
  kuwakandamiza Waislamu. Serikali ikawa radhi kuvunja Katiba ya nchi kwa
  kupitisha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya 2002 ili zipatikane fursa zaidi za
  kuwanyoongesha Waislamu. Waislamu waliipinga sheria hiyo kwa nguvu zao zote,
  lakini kwa kuwa wao ni jamii inayotakiwa kupigwa vita hawakusikilizwa. Bunge
  ambalo nalo lina Wakristo wengi likaipitisha haraka sheria hiyo. Naam, tangu
  imepitishwa hadi leo, sheria hiyo imetumika kuwadhuru Waislamu wasiokuwa na
  hatia yoyote, na kufunga taasisi zilizokuwa zikiwasaidia Waislamu. Misaada ni
  haki ya Wakristo, siyo Waislamu. Pamoja na madhila yote hayo Waislamu wanatakiwa
  waendelee kuamini kuwa Tanzania ni nchi moja inayojali raia wake wote.
  (8) Wakati serikali ikidai kuwa Tanzania ni taifa ambalo raia wote wana haki
  sawa, lakini serikali hiyo hiyo kwa makusudi kabisa inafanya jitihada za
  waziwazi za kuwahamasisha Wakristo wawaone Watanzania ambao ni Waislamu kuwa ni
  maadui zao na maadui wa taifa lao. Januari 2001 Waziri Mkuu Mh. Frederick Sumaye
  alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa serikali inazo taarifa
  kuwa kundi la magaidi waliopata mafunzo nchi za nje limerejea nchini na magaidi
  hao wanapanga kuilipua hospitali ya Muhimbili. Kufuatia kauli hiyo Waislamu
  watatu wa Muhimbili ambao ni Waislamu akiwemo Profesa wa Micro-Biology walitiwa
  mbaroni. Japo baadaye waliachiwa kwani hawakuwa na hatia yoyote, lengo la
  serikali la kupandikiza sumu ya chuki lilikuwa limetimia. Tarehe 24 Agosti 2001
  Waislamu walifanya maandamano kupinga kufungwa kwa Dibagula kwa kusema Yesu si
  Mungu. Serikali kupitia jeshi la polisi likawatangazia wananchi wote kuwa
  Waislamu wamepanga kuyalipua makanisa siku ya Jumapili ya tarehe 2 Septemba
  2001. Na serikali ikawahakikishia Wakristo kuwa itaweka maaskari wa kuwalinda na
  hiyo shari ya Waislamu. Lengo la uzushi huu ni kuwachochea Wakristo wawachukie
  Waislamu na hivyo waunge mkono hatua za serikali za kuwapa kipondo. Hivi sasa
  huo umekuwa ni mchezo wa kawaida. Kila baada ya muda Fulani serikali kwa kpitia
  jeshi la polisi hutoa taarifa za kuonesha kuwa kuna mpango wa shambulio la
  kigaidi. Na watuhumiwa siku zote ni Waislamu. Serikali na makanisa yanawachukia
  Waislamu kiasi cha kuwa tayari kushirikiana na wasiokuwa Watanzania katika
  kuwahujumu Waislamu. Ni dhahiri kuwa katika mazingira kama haya, Maaskofu
  wakipata kisingizio chochote watakuwa tayari kuwauwa Waislamu kama
  walivyoshiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda.
  (9) Papa John Paul II alipoitembelea Tanzania mwaka 1990, Kanisa Katoliki
  lilimkabidhi Ripoti yenye anwani: Activities of the Church in Tanzania. Katika
  ripoti yake hiyo Kanisa Katoliki limetaja kuwapo kwa Tume ya Majeshi ya Kivita
  [Commission of Armed Forces] ndani ya Kanisa hilo. Tangu wakati huo hadi leo
  Waislamu wameitaka serikali iwaondoshe hofu kwa kuweka wazi kazi za Tume hiyo ya
  Majeshi ya Kivita ndani ya Kanisa. Serikali haijajibu na wala haijajishughulisha
  na taarifa nzito kama hizo. Hatujui kama Tume hiyo ya Majeshi ya kivita inafanya
  kazi ndani ya Jeshi la Wananchi au nje ya jeshi hilo. Lakini kwa muktadha wa
  hali ya uhasama wa serikali na hasa wa Maaskofu dhidi ya Waislamu wanaowahesabu
  kuwa ni maadui zao, si vigumu kukisia kwa nini Kanisa Katoliki limeunda Tume ya
  Majeshi ya Kivita. Lakini serikali ambayo haishughulishwi kabisa na Tume ya
  Majeshi ya Kivita ya Wakatoliki imekuwa na tabia ya kuwakamata na kuwatia ndani
  Waislamu kwa kesi za kuwabambikia zisizokuwa na kichwa wala miguu. Lakini
  propaganda zinasema Tanzania ni nchi moja yenye katiba inayolinda haki za watu
  wote. Mwenye mach haambiwi tazama.
  Dalili ya Mvua ni Mawingu
  Alipokuwa akitoa mada yake juu ya “Mifumo ya Viashiria vya Migogoro” katika
  Mkutano wa Kumi na Moja wa Hali ya Siasa Tanzania ulioandaliwa na REDET mwaka
  2003, Mh. Bernard L. Membe alisema kwamba migogoro mingi duniani na hasa vita
  vya wenyewe kwa wenyewe vina dalili na viashiria vyake. Akasema miongoni mwa
  dalili kubwa kuwa nchi karibu itaingia katika machafuko ya vita vya wenyewe kwa
  wenyewe ni kutokea kwa mgawanyiko au kutokea kutoelewana kwa viongozi ndani ya
  chama au serikali tawala.

  Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia viongozi mbalimbali wa serikali
  wakiwamo mawaziri wakipingana hadharani juu ya maamuzi waliyoyafanya wenyewe.
  Lakini pia katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia pia mgongano wa waziwazi
  kati ya wabunge wa CCM na Chama chao. Na wote hao hawachoki kujisifu kuwa
  wanamuenzi Mwalimu Nyerere. Lakini mwaka 1993, Nyerere katika Kitabu chake
  Tanzania! Tanzania! Aliandika na tunanukuu:
  Ziko jitihada sasa hivi za kugombanisha Wabunge na chama chao kwa kutumia hoja
  ya hadhi ya Bunge. Ni nani huyu anayefanya kazi hii? Ni haki kabisa ya vyama vya
  upinzani kujaribu kugombanisha Wabunge wa chama kinachotawala na chama chao.
  Lakini viongozi wa chama kinachotawala pamoja na Serikali yenyewe wanapojaribu
  kufanya mambo ambayo yatagombanisha Wabunge wa CCM na chama chao, tuna haki ya
  kuwauliza viongozi hao wanafanya kazi hii kwa niaba ya nani, na chama chao ni
  chama gani? [uk. 41]
  Pamoja na kuyajua yote hayo hivi sasa kuna msuguano ulio dhahiri kabisa baina ya
  Wabunge wa CCM na Chama chao. Kiashiria kingine alichokitaja Mh. Membe ni kwa
  serikali kushindwa kuyashughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi
  yanayoelekezwa serikalini.
  Maazimio ya Waislamu
  Kwa kuzingatia muktadha wa hali ya kisiasa ilipofikia hivi sasa, Waislamu
  tumefikia maamuzi yafuatayo:
  (1) Maadam Mfumo Kristo umeimarika kiasi cha kuweza kuitisha serikali na
  viongozi wake na wakatishika, na maadam Mfumo huo Kristo una nguvu za kuweza
  hata kuvitisha na kuvikemea vyombo vya dola na vikasalimu amri, Waislamu tutake
  tusitake, kama alivyohadharisha Mh. Membe, ukweli unabaki kuwa hautapita muda
  mrefu, dhulma hii ya udini italisambaratisha Taifa letu, kama udini
  ulivyoisambaratisha Ivory Coast ambayo katika miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa
  mfano wa kuigwa.

  Hivyo basi wajibu wetu wa mwanzo ni kuufikisha ujumbe huu kwa Waislamu wote
  nchini, na kuwataka wazingatie kuwa kwa kuwa wanabaguliwa na kudhalilishwa
  katika nchi hii kwa sababu ya Uislamu wao, basi ni wajibu wao na wao kushikamana
  kama Waislamu.
  (2) Kwa kuwa kila wanchosema Maaskofu ndicho kinachofuatwa na serikali, na kwa
  kuwa Maaskofu wamekwishatamka hadharani na kwa sauti kali kuwa katika nchi yetu
  hakuna kabisa udini na atakayesema kuna udini basi ni yeye ndiye anayetaka
  kuleta udini, na kauli hiyo kudakwa na mawakala wa Maaskofu katika serikali, ni
  dhahiri kuwa dhulma za udini zinazoendelea kuwakandamiza Waislamu miaka 50 baada
  ya Uhuru hazitaondoshwa na Katiba mpya. Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania
  ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia
  huru na sawa na wenzao. Waislamu popote tulipo tunao wajibu wa kuorodhesha
  dhulma zote za udini tunazofanyiwa na kupigania ziondolewe kwanza na kulipwa
  fidia.
  (3) Kwa kuwa tangu ukoloni hadi leo Waislamu wanahesabiwa na serikali na
  Maaskofu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na wasiostahiki haki sawa na wengine, na
  kwa kuwa Waislamu wameazimia kutokukubali tena kudhulumiwa na kuonewa kwa namna
  yoyote ile iwayo, ni wazi kuwa hakuwezi kuwa na katiba itakayoweza kulinda haki
  za madhalimu na wadhulumiwa kwa wakati mmoja. Ingawa kwa propaganda za kisiasa
  Tanzania ni nchi moja, lakini kiuhalisia ni nchi yenye jamii mbili zenye hadhi
  na haki tofauti kabisa. Umefika sasa wakati wa kugawana nchi ili Waislamu
  wanaochukiwa na kunyimwa fursa sawa na Wakristo waishi katika maeneo yenye
  Waislamu wengi na Wakristo waishi katika maeneo yenye Wakristo wengi. Mwalimu
  Nyerere alipigania kwa nguvu zake zote Nigeria igawanywe ili Wakatoliki ambao
  walikuwa wanadhulumiwa Nigeria wajitenge na waruhusiwe kuishi katika nchi ya
  Biafra. Na katika kijitabu alichokiandika 1966 Nyerere alisema madai ya
  kuhifadhi umoja wa kitaifa wa Nigeria hayana maana yoyote pale ambapo baadhi ya
  raia wa taifa hilo wanadhulumiwa. Ushahidi wa dhulma za Waislamu upo wazi.
  Kugawana nchi kutawawezesha Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi na kujiunga na
  OIC bila ya kuwakera Maaskofu. Ni wajibu wetu kulifikisha hili kwa Waislamu
  wenzetu nchi nzima ili lijadiliwe zaidi kabla halijafikishwa rasmi

  (4) Kwa kuwa hakuwezi kuwa na amani ya kweli bila ya haki, na kwa kuwa amani ya
  Tanzania inashikiliwa na Waislamu walioruhusu dhulma hiyo, Waislamu tunayo dhima
  kubwa kwa kustawi kwa Mfumo Kristo ambao sasa hapana shaka yoyote
  unalisambaratisha Taifa. Lakini kama alivyosema Nyerere, anayedhulumiwa ni mtu
  anayeteseka. Asipopambana na huyo dhalimu, yeye ataendelea kuteseka wakati
  dhalimu anastarehe kwa amani. Akiamua kupambana, wote yeye na dhalimu
  watateseka. Baada ya miaka 50 ya kuachia kundi moja la jamii likistarehe na hali
  Waislamu wanateseka, umefika wakati sasa wa kugawana machungu ya udini
  tuliyoyabeba peke yetu kwa miaka hamsini.
   
 2. BULLDOZZER

  BULLDOZZER Senior Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tamko limetulia!
  Muda utawadia!
  Wanafiki Kujutia!
  Nchi wataikimbia!
   
 3. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,878
  Likes Received: 1,048
  Trophy Points: 280
  Jamani mko wapi mbona hamchangii?? au ni refu mno?? mmezoea heading za line TATU? Mie nimeleat kama lilivyo bila kuchakachua!
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
   
 5. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mbovu sana haina mantiki. Nitatoa adhabu ya kuondoa kopo la kuchambia misikiti yote.
   
 6. BULLDOZZER

  BULLDOZZER Senior Member

  #6
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
   
 9. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nilishasema tugawane hii nchi halafu tuwaone watakavyouana hamkusikia!
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ama kweli debe tupu haliachi kutika. Katika magazeti ya leo yametoa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne. Ukiangalia karibu 98% ya shule zilizoongoza ni seminari za kikiristu na 2% ni sekondari za Serikali. Sijaona hata seminari moja ya kiislamu.

  Ukiangalia wanafunzi waliofanya vizuri best top ten majina yote ya kikiristu sijaona hata jina moja la kiislamu.

  Bado masheikh wanaona wakiristu wanapendelewa shame on their face. Wakiristu wamejenga hospitali Bugando, KCMC etc wao kama masheikh watuonyesha referall hospital yao moja kama sio ukosefu wa akili. Bora hata Agha Khana anawashinda waislamu wanazo Hospitals

  Nyerere alitaifisha shule zetu wakiristu ili na nyinyi waislamu muweze kusoma kwa kuondoa kisingizio eti mkienda shule mtabatizwa leo hii mnasema ndiyo adui namba moja wa uislamu Tanzania. Ama kweli shukurani ya punda ni mateke.

  Masheikh hao wamekosa hata akili ya mtoto wa chekechea. Kwa taarifa ni kwamba wabunge hawateuliwi na mtu (achilia mbali wale 10 wa Rais). Wabunge wanachaguliwa na wananchi sasa hizo lawama za kuwa wabunge 75% wakiristu zinatoka wapi?

  Ukweli ni kwamba waislamu including hao masheikh ni mbumbumbu mzungu wa reli na kwa mantiki hiyo mtabaki kulalamika hadi ahera. Kalaghabaho. Sasa kwa tamko kama hili kweli serikali makini itaweza kuwasikiliza? Hata mnacholalamikia hamafahamu Je mnailamimikia Serikali au Maaskofu au Wakiristu wote au Wakatoriki?!

  Kama nyinyi waislamu mnajinadi kwamba nyinyi ndiye mnayemfahamu Mungu wa kweli, Mbona basi huyo Mungu wenu wa kweli hawasaidii kitu chochote na Sisi wakiristu tunao abudu Binadamu Yesu kuwa ni Mungu tuna mafanikio kuliko nyinyi?!

  Mimi nafikiri huyo Mungu wenu mnayempigania (Sic) badala ya Mungu kuwapigania nyinyi (Binadamu) because is a creator si Mungu bali Shetani. Mliingizwa mkenge na Muhammed (houseboy wa wa Khadija) Njooni kwa Yesu mpate amani na hayo malalamiko yatakwisha KARIBUNI
   
 12. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #12
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160


  • Topical
   [​IMG]
   JF Senior Expert Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] Join DateFri Dec 2010Posts673Thanks39Thanked 110 Times in 53 Posts Rep Power21


   Did you find this post helpful? [​IMG] | [​IMG]
   [​IMG] Tamko la waislamu (FULL TEXT)

   TAMKO LA WAISLAMU DHIDI YA KAULI ZA MAASKOFU

   Utangulizi
   Oktoba 31, 2010 Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu ambapo wananchi walipata fursa ya kumchagua Rais, wabunge pamoja na madiwani. Katika uchaguzi huo, Watanzania kwa ujumla wao walikichagua Chama cha Mapinduzi, CCM, kuongoza tena nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

   Hata hivyo, wakati wananchi wakiamini kwamba wanaongozwa na watu waliowapigia kura, matukio yanayoendelea hivi sasa yanaashiria serikali kutelekeza majukumu yake na kuwaacha maaskofu wakielekeza nchi wanakotaka.

   Itakumbukwa kwamba awali kabla ya uchaguzi mkuu maaskofu walikuwa wametoa Ilani yao ya uchaguzi bila kueleza kipi chama chao kitakachosimamia na kutekeleza Ilani hiyo. Baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala, CCM, walishabikia Ilani hiyo na kuwatetea maaskofu. Kwa hakika taarifa za vyombo vya habari zilifahamisha kwamba baadhi ya watendaji waandamizi ndani ya serikali walishiriki katika kuandaa Ilani hiyo.

   Ilipofika wakati wa kampeni hadi kuingia siku ya kupiga kura, ilikuwa imedhihiri kipi kilikuwa chama cha maaskofu ambacho walitarajia kitekeleze Ilani yao. Haikuwa tena jambo la siri kwani walisimama wazi wazi kuwaelekeza waumini wao wampigie nani kura. Na katika juhudi zao za kutaka wafuasi wao wawaelewe vizuri, maaskofu walithubutu hata kuweka kando mafundisho ya Biblia yao juu ya masuala ya uzinzi wakawahimiza waumini kumpigia kura mtu wanayemtaka bila kujali kwamba anakabiliwa na kashfa ya kupora mke wa mtu. Waliwaambia wasihangaike na maisha binafsi ya ndoa ya mgombea.

   Hata hivyo, matokeo ya kura yalitoa majibu kwamba Watanzania walikuwa wameikataa Ilani ya Maaskofu.

   Waislamu tumelazimika kukutana na kutoa tamko hili kwa sababu matukio yanayotokea hivi sasa yanaonesha kuwa wale ambao Watanzania walikataa kuwapa uongozi na Ilani yao iliyoandaliwa na maaskofu, ndio sasa wanaielekeza nchi pa kwenda huku viongozi wa CCM na serikali wakijitahidi kadiri ya uwezo wao kunyenyekea kwa maaskofu hao.

   Tumeona na tumemsikia Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda akihangaika kuwapigia magoti na kuwaomba radhi maaskofu kule Sumbawanga. Tumesikia jinsi viongozi wanaojaribu kuwaambia maaskofu kwamba kama wanataka kuingia katika siasa wavue majoho na vyeo vyao vya kikanisa kama Padiri mwenzao waliyekuwa wakimpigania kuingia Ikulu, wanavyokemewa na kutakiwa wawaombe radhi maaskofu hao.

   Lililo baya zaidi maaskofu walioshindwa kuwashawishi wananchi waipokee na kukubali Ilani yao, wamekuja na kampeni za kuchochea uasi kwa serikali iliyopo madarakani. Lakini pamoja na hali hiyo, viongozi wa CCM na serikali wamebaki wanagwaya. Hakuna aliyeweza kupata ujasiri wa kukemea hali hii. Kinyume chake Waziri Mkuu na Mzee John Samwel Malecela wanahangaika huku na kule wakiwapigia magoti maaskofu hao na kuwakemea wanaothubutu kuwakosoa.

   Hali kama hii ni hatari kwa usalama na utulivu wa nchi. Ni hali ya kuchochea udini na kuweka ombwe la uongozi wa kisiasa ambao utazua balaa. Waislamu hatuwezi kukubali hali hii. Kwa hiyo, ama CCM na serikali vitekeleze wajibu wao wa kuongoza au kama wanaona hawawezi, basi waseme rasmi ili Maaskofu na wengine wenye Ilani zao za uchaguzi waingie tena ulingoni kuomba ridhaa ya Watanzania kuongoza nchi kuliko kuishi katika hiki kiini macho ambapo maaskofu na mawakala wao ndani ya serikali wameachwa waikokote nchi wanakotaka.

   Kiini cha Hali hii ya Kisiasa
   Hali hii ya kisiasa tunayoishuhudia leo nchini mwetu ni matunda ya mbegu liliyopandwa na kupaliliwa kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Wakoloni walikuwa na kanuni yao waliyoiita divide et impero yaani wagawe ili uwatawale. Huko Rwanda wakoloni waliwagawa wananchi kwa misingi ya kikabila. Watusi ambao ni watawala wapewe elimu ya juu na wanfundishwe kwa Kifaransa, na Wahutu ambao ni watawaliwa wapewe elimu duni na wafundishwe kwa Kiswahili. Ubaguzi huo wa kuwagawa raia wa nchi moja ulipandikiza sumu iliyokuja kusababisha Wanyarwanda kuuana.

   Hapa kwetu wakoloni walitugawa kwa misingi ya dini. Kabla ya uhuru wa Tanganyika, wakoloni kwa kushirikiana na makanisa waliwaona Waislamu kama ni mahasimu wao kidini na kisiasa. Na kwa sababu hiyo serikali za kikoloni zikaweka mikakati maalum ya kuwakandamiza Waislamu katika maeneo matatu: kwanza kuwawekea vikwazo katika kutangaza dini yao ili wasiongezeke; pili kuwabana katika elimu na ili kuhakikisha kuwa Waislamu wanabanwa jukumu la kuwaelimisha Waafrika likawekwa mikononi mwa makanisa na kazi ya serikali ni kuzigharimia tu shule hizo. Lengo likiwa ni kuwabatiza Waislamu wachache watakaoruhusiwa kusoma, na tatu kuwabana katika ajira serikalini kwa sababu makanisa yote yalisisitiza kuwa kuwaajiri Waislamu serikalini ni kusaidia kuenea kwa Uislamu..

   Kwa kuwa ubaguzi huo haukuwa na kificho chochote, Waislamu wengi walijitokeza kupambana na ukoloni kwa matarajio kuwa serikali huru itaondosha chuki na uadui huo dhidi ya Waislamu. Lakini msiba mkuu wa taifa hili ni kwamba kinyume chake, baada ya uhuru msimamo ukawa ni ule ule wa kuwaona Waislamu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na mikakati ya kuwabana Waislamu katika maeneo yale matatu ikaimarishwa zaidi wakati wa utawala wa Nyerere. Kuanzia 1957 mkakati uliopangwa na Kanisa Katoliki ukawa ni kuhakikisha kuwa nafasi zote muhimu za uongozi na serikali zinashikwa na wao. [Taz. Confidential Diary – Tanganyika, March-April 1957, uk. 3-4 Maryknoll Central Archives, New York ]. Na ni mkakati huu ndio ambao Mwalimu Nyerere aliokuwa akimuhakikishia Askofu Rweyemamu mwaka 1970 kuwa anatumia mamlaka yake kama Rais na kama kiongozi wa TANU kuhakikisha kuwa anatoa upendeleo maalum kwa Wakristo ili wasimamie sera za Chama. Na kwamba amemteua padiri katika nafasi nyeti ya Chama si kwa sababu anajua siasa bali kwa sababu ni Mkristo safi. Lakini Nyerere huyo huyo akisimama hadharani alijidai kukemea udini. Na kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuliimarisha kanisa na kuwadhoofisha Waislamu, leo Kanisa lake limo katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa ni Mtakatifu!

   Sivalon anaarifu katika kitabu chake kuwa mara baada ya uhuru Kanisa katoliki liliwahamasisha Wakristo wote na hasa watendaji wa serikali juu ya hatari ya Ukomunisti na Uislamu na walikusanya nguvu zao zote katika kukabiliana na maadui hao.

   Matokeo ya Hujuma Hizo
   Matokeo ya hujuma hizo za kichinichini ni kwamba katika sura ya nje na katika propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na kisiwa cha amani. Lakini uhalisia wa mambo ni kuwa Tanzania ni nchi yenye jamii kubwa mbili. Jamii ya Wakristo wanaopewa msaada, upendeleo, ulinzi na heshima, na jamii ya Waislamu ambao wanachukiwa, kudharauliwa na kudhoofishwa na serikali kabla na baada ya Uhuru. Ifuatayo ni mifano michache tu ya baadhi ya hujuma hizo baada ya Uhuru.

   (1) Mwaka 1963 katika Barua ya Kichungaji, Kanisa Katoliki lilisema Waislamu walikuwa wanajenga umoja na mshikamano miongoni mwao, jambo ambalo ni "hatari kubwa kwa hatima ya Wakristo wetu" na Sivalon anabainisha kuwa Wakristo walimwomba Nyerere awasaidie kuvuruga umoja huo wa Waislamu. Ndio sababu ya Nyerere kutumia dola kuiparaganya EAMWS. Kwa kuwa Waislamu ni jamii inayotakiwa kuwa dhalili, hawatakiwi kuwa na umoja. Ndio maana tangu wakati wa Nyerere hadi leo, uchaguzi wa viongozi wa Waislamu husimamiwa na vyombo vya dola. Nia ikiwa ni kutokuwapa Waislamu uhuru wa kuwachagua viongozi wao. Katika taifa moja haki hiyo ni ya Wakristo peke yao. Sote ni mashahidi kuwa mwaka 1994 serikali ilimwagiza Naibu Waziri Mkuu Mh. Augustino L. Mrema kuhakikisha kuwa Bakwata inapitisha katiba mpya inayotakiwa na serikali. Na Maaskofu wakachangia gharama. Waislamu ni maadui kidini na kisiasa, lazima wadhibitiwe.

   (2) Mwaka 1992 Serikali ya Tanzania ilitiliana saini Makubaliano ya Itifaki rasmi na Makanisa ya TEC na CCT. Kwa mujibu wa makubaliano hayo ambayo yalitiwa saini na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye wakati huo alikuwa Mh. Edward Lowasa serikali imewajibishwa pamoja na mambo mengine, kutenga nafasi za masomo kwenye vyuo vyake vya Ualimu mahsusi kwa ajili ya wanafunzi wanaopangwa kufundisha katika shule za Kanisa; pia kutoa ruzuku ya kuendeshea taasisi za Makanisa. Kuanzia 1992 hadi leo serikali imetoa mabilioni ya kodi za wananchi kwa Makanisa. Katika kipindi chote hicho Waislamu wamepinga ubaguzi huo. Lakini kwa kuwa lengo ni kuwaimarisha Wakristo ambao ni jamii inayotakiwa kupewa nguvu zaidi dhidi ya jamii ya Waislamu ambao wanatizamwa kama maadui, serikali imeyapuuza malalamiko ya Waislamu. Lakini propaganda zinaendelea kuwa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na ni kisiwa cha amani.

   (3) Waislamu wameiomba serikali kujiunga na OIC kama njia mojawapo itakayowezesha nchi yetu kupata misaada itakayotumika kuinua hali za Waislamu ambao wameachwa nyuma sana katika elimu na uchumi. Makanisa yote kwa kauli moja yamepinga kwa nguvu zao zote pendekezo hilo. Sababu ya kupinga kwao ni kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanadhoofishwa katika kila hali, na ni makosa makubwa kuwaimarisha kiuchumi au kielimu maadui hao. Serikali ilipofanya utafiti wake wa kina ikajiridhisha kuwa kujiunga na OIC kuna manufaa na hakuna madhara yoyote. Na Mh. Bernard Membe alitamka hilo Bungeni. Mara akaitwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Cardinali Pengo na kukumbushwa mkakati wa kuwadhoofisha Waislamu. Msimamo wa serikali ukabadilika. Lakini propaganda za kuwazuga Waislamu zinasema Watanzania wote ni kitu kimoja na nchi hii haina ubaguzi!

   (4) Kwa kuwa tangu wakati wa ukoloni hadi leo mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanaminywa kadiri iwezekanavyo katika nafasi za uongozi na ajira, ndio maana hadi leo, miaka 50 baada ya Uhuru Waislamu ni wachache sana katika nafasi zote za uongozi na ajira katika sehemu muhimu serikalini na katika vyombo muhimu vya maamuzi. Kisingizio kinachotolewa ni kuwa Waislamu hawataki kusoma. Lakini ukitazama orodha ya Wakuu wa Wilaya wote walioteuliwa na sifa zao, utaona dhahiri kuwa wapo Waislamu wengi wenye sifa bora zaidi ambao wangestahili kuwa ma-DC. Waislamu hawateliwi kwa sababu mkakati uliopo ni kuwatenga Waislamu na ikiwezekana kuwaondosha kabisa katika sehemu muhimu za uongozi, kwa sababu kama wao hawajui ukweli ni kwamba hawatakiwi kushika nafasi zozote muhimu za uongozi au ajira. Ndio maana asilimia 75 ya Ma-DC wote ni Wakristo na karibu wasimamizi wote wa Uchaguzi katika wilaya ni Wakristo. Wabunge asilimia 75 pia ni Wakristo, na hali ni hiyo hiyo katika Vitengo vya serikali na Mashirika ya uma. Ndio maana hakuonekani tatizo lolote pale taasisi yote inapokuwa na Wakristo watupu. Na kelele nyingi maadui wa serikali na Kanisa wanapopewa nafasi hata kama wana uwezo kiasi gani. Katika sura ya nje Tanzania ni taifa moja, katika uhalisia wake ni kuna mataifa mawili, moja nyonge na jingine lenye nguvu.

   (5) Kwa kuwa Waislamu wanahesabiwa kuwa ni maadui, ule mkakati uliowekwa na wakoloni wa kuwawekea vikwazo Waislamu katika kutangaza dini yao unaendelea hadi leo. Ipo mifano mingi sana ya Waislamu kukamatwa, kutiwa ndani na kunyanyaswa na vyombo vya dola kwa sababu tu ya kulingania hadharani dini yao. Kwa kuwa Waislamu ni maadui, basi ni muhimu kuhakikisha kuwa hawaongezeki. Wakristo wanayo haki ya kuitisha mkutano wa hadhara na kutangaza kuwa Yesu ni Mungu. Wao ni jamii inayostahiki ulinzi wa dola. Lakini pindi Mwislamu atakaposema hadharani kuwa Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi siyo Yesu mwana wa Mariamu atakuwa amekashifu dini ya dola na atakamatwa na kubughudhiwa. Lakini kipropaganda, Tanzania ni nchi moja na inafuata katiba moja. Lakini uhalisia ni tofauti.

   (6) Msimamo wa serikali na makanisa kuhusiana na mauaji ya Waislamu katika msikiti wa Mwembechai ni kielelezo kingine cha ukweli kuwa Tanzania ni mkusanyiko wa jamii mbili zenye haki na hadhi tofauti katika taifa moja. Kwa kushinikizwa na Maaskofu serikali iliwauwa Waislamu watatu Mwembechai pasi na hatia yoyote. Waislamu waliiomba Mahaka, Bunge na hata Rais aunde Tume ya uchunguzi. Mihimili yote ya dola ilikataa. Kiongozi wa Kanisa Katoliki akenda mbali zaidi. Akahalalisha mauaji hayo. Kwa sababu waliouliwa ni wale maadui wa ile jamii nyoge isiyotakiwa kustawi. Lakini alipouliwa mbwa "Imigresheni" mwaka huo huo wa 1998, Jaji Mkuu wa wakati huo Mh. Francis Nyalali aliamuru uchunguzi wa kuuliwa mbwa huyo na hakimu akaadhibiwa. Jaji Mkuu alichukua uamuzi huo bila kuombwa na mtu. Lakini wale waliowauwa Waislamu walipongezwa na kupandishwa vyeo. Uhasama wa serikali na makanisa dhidi ya jamii ya Waislamu ni wa kiwango cha kutisha. Msimamo ukawa huo huo walipouliwa Waislamu Unguja na Pemba 2001 kwa kuandamana kudai Katiba Mpya. Lakini kipropaganda tunaambiwa Watanzania wote wanahaki sawa.

   (7) Rais wa Marekani George W. Bush alipotangaza Vita vya Msalaba dhidi ya Waislamu mwaka 2001, serikali ya Tanzania ikapata uhalali zaidi wa kuzidi kuwakandamiza Waislamu. Serikali ikawa radhi kuvunja Katiba ya nchi kwa kupitisha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya 2002 ili zipatikane fursa zaidi za kuwanyoongesha Waislamu. Waislamu waliipinga sheria hiyo kwa nguvu zao zote, lakini kwa kuwa wao ni jamii inayotakiwa kupigwa vita hawakusikilizwa. Bunge ambalo nalo lina Wakristo wengi likaipitisha haraka sheria hiyo. Naam, tangu imepitishwa hadi leo, sheria hiyo imetumika kuwadhuru Waislamu wasiokuwa na hatia yoyote, na kufunga taasisi zilizokuwa zikiwasaidia Waislamu. Misaada ni haki ya Wakristo, siyo Waislamu. Pamoja na madhila yote hayo Waislamu wanatakiwa waendelee kuamini kuwa Tanzania ni nchi moja inayojali raia wake wote.

   (8) Wakati serikali ikidai kuwa Tanzania ni taifa ambalo raia wote wana haki sawa, lakini serikali hiyo hiyo kwa makusudi kabisa inafanya jitihada za waziwazi za kuwahamasisha Wakristo wawaone Watanzania ambao ni Waislamu kuwa ni maadui zao na maadui wa taifa lao. Januari 2001 Waziri Mkuu Mh. Frederick Sumaye alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa serikali inazo taarifa kuwa kundi la magaidi waliopata mafunzo nchi za nje limerejea nchini na magaidi hao wanapanga kuilipua hospitali ya Muhimbili. Kufuatia kauli hiyo Waislamu watatu wa Muhimbili ambao ni Waislamu akiwemo Profesa wa Micro-Biology walitiwa mbaroni. Japo baadaye waliachiwa kwani hawakuwa na hatia yoyote, lengo la serikali la kupandikiza sumu ya chuki lilikuwa limetimia. Tarehe 24 Agosti 2001 Waislamu walifanya maandamano kupinga kufungwa kwa Dibagula kwa kusema Yesu si Mungu. Serikali kupitia jeshi la polisi likawatangazia wananchi wote kuwa Waislamu wamepanga kuyalipua makanisa siku ya Jumapili ya tarehe 2 Septemba 2001. Na serikali ikawahakikishia Wakristo kuwa itaweka maaskari wa kuwalinda na hiyo shari ya Waislamu. Lengo la uzushi huu ni kuwachochea Wakristo wawachukie Waislamu na hivyo waunge mkono hatua za serikali za kuwapa kipondo. Hivi sasa huo umekuwa ni mchezo wa kawaida. Kila baada ya muda Fulani serikali kwa kpitia jeshi la polisi hutoa taarifa za kuonesha kuwa kuna mpango wa shambulio la kigaidi. Na watuhumiwa siku zote ni Waislamu. Serikali na makanisa yanawachukia Waislamu kiasi cha kuwa tayari kushirikiana na wasiokuwa Watanzania katika kuwahujumu Waislamu. Ni dhahiri kuwa katika mazingira kama haya, Maaskofu wakipata kisingizio chochote watakuwa tayari kuwauwa Waislamu kama walivyoshiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda.

   (9) Papa John Paul II alipoitembelea Tanzania mwaka 1990, Kanisa Katoliki lilimkabidhi Ripoti yenye anwani: Activities of the Church in Tanzania. Katika ripoti yake hiyo Kanisa Katoliki limetaja kuwapo kwa Tume ya Majeshi ya Kivita [Commission of Armed Forces] ndani ya Kanisa hilo. Tangu wakati huo hadi leo Waislamu wameitaka serikali iwaondoshe hofu kwa kuweka wazi kazi za Tume hiyo ya Majeshi ya Kivita ndani ya Kanisa. Serikali haijajibu na wala haijajishughulisha na taarifa nzito kama hizo. Hatujui kama Tume hiyo ya Majeshi ya kivita inafanya kazi ndani ya Jeshi la Wananchi au nje ya jeshi hilo. Lakini kwa muktadha wa hali ya uhasama wa serikali na hasa wa Maaskofu dhidi ya Waislamu wanaowahesabu kuwa ni maadui zao, si vigumu kukisia kwa nini Kanisa Katoliki limeunda Tume ya Majeshi ya Kivita. Lakini serikali ambayo haishughulishwi kabisa na Tume ya Majeshi ya Kivita ya Wakatoliki imekuwa na tabia ya kuwakamata na kuwatia ndani Waislamu kwa kesi za kuwabambikia zisizokuwa na kichwa wala miguu. Lakini propaganda zinasema Tanzania ni nchi moja yenye katiba inayolinda haki za watu wote. Mwenye mach haambiwi tazama.

   Dalili ya Mvua ni Mawingu
   Alipokuwa akitoa mada yake juu ya "Mifumo ya Viashiria vya Migogoro" katika Mkutano wa Kumi na Moja wa Hali ya Siasa Tanzania ulioandaliwa na REDET mwaka 2003, Mh. Bernard L. Membe alisema kwamba migogoro mingi duniani na hasa vita vya wenyewe kwa wenyewe vina dalili na viashiria vyake. Akasema miongoni mwa dalili kubwa kuwa nchi karibu itaingia katika machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni kutokea kwa mgawanyiko au kutokea kutoelewana kwa viongozi ndani ya chama au serikali tawala.

   Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo mawaziri wakipingana hadharani juu ya maamuzi waliyoyafanya wenyewe. Lakini pia katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia pia mgongano wa waziwazi kati ya wabunge wa CCM na Chama chao. Na wote hao hawachoki kujisifu kuwa wanamuenzi Mwalimu Nyerere. Lakini mwaka 1993, Nyerere katika Kitabu chake Tanzania! Tanzania! Aliandika na tunanukuu:

   Ziko jitihada sasa hivi za kugombanisha Wabunge na chama chao kwa kutumia hoja ya hadhi ya Bunge. Ni nani huyu anayefanya kazi hii? Ni haki kabisa ya vyama vya upinzani kujaribu kugombanisha Wabunge wa chama kinachotawala na chama chao. Lakini viongozi wa chama kinachotawala pamoja na Serikali yenyewe wanapojaribu kufanya mambo ambayo yatagombanisha Wabunge wa CCM na chama chao, tuna haki ya kuwauliza viongozi hao wanafanya kazi hii kwa niaba ya nani, na chama chao ni chama gani? [uk. 41]
   Pamoja na kuyajua yote hayo hivi sasa kuna msuguano ulio dhahiri kabisa baina ya Wabunge wa CCM na Chama chao. Kiashiria kingine alichokitaja Mh. Membe ni kwa serikali kushindwa kuyashughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi yanayoelekezwa serikalini.

   Maazimio ya Waislamu
   Kwa kuzingatia muktadha wa hali ya kisiasa ilipofikia hivi sasa, Waislamu tumefikia maamuzi yafuatayo:

   (1) Maadam Mfumo Kristo umeimarika kiasi cha kuweza kuitisha serikali na viongozi wake na wakatishika, na maadam Mfumo huo Kristo una nguvu za kuweza hata kuvitisha na kuvikemea vyombo vya dola na vikasalimu amri, Waislamu tutake tusitake, kama alivyohadharisha Mh. Membe, ukweli unabaki kuwa hautapita muda mrefu, dhulma hii ya udini italisambaratisha Taifa letu, kama udini ulivyoisambaratisha Ivory Coast ambayo katika miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa mfano wa kuigwa.

   Hivyo basi wajibu wetu wa mwanzo ni kuufikisha ujumbe huu kwa Waislamu wote nchini, na kuwataka wazingatie kuwa kwa kuwa wanabaguliwa na kudhalilishwa katika nchi hii kwa sababu ya Uislamu wao, basi ni wajibu wao na wao kushikamana kama Waislamu.

   (2) Kwa kuwa kila wanchosema Maaskofu ndicho kinachofuatwa na serikali, na kwa kuwa Maaskofu wamekwishatamka hadharani na kwa sauti kali kuwa katika nchi yetu hakuna kabisa udini na atakayesema kuna udini basi ni yeye ndiye anayetaka kuleta udini, na kauli hiyo kudakwa na mawakala wa Maaskofu katika serikali, ni dhahiri kuwa dhulma za udini zinazoendelea kuwakandamiza Waislamu miaka 50 baada ya Uhuru hazitaondoshwa na Katiba mpya. Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia huru na sawa na wenzao. Waislamu popote tulipo tunao wajibu wa kuorodhesha dhulma zote za udini tunazofanyiwa na kupigania ziondolewe kwanza na kulipwa fidia.

   (3) Kwa kuwa tangu ukoloni hadi leo Waislamu wanahesabiwa na serikali na Maaskofu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na wasiostahiki haki sawa na wengine, na kwa kuwa Waislamu wameazimia kutokukubali tena kudhulumiwa na kuonewa kwa namna yoyote ile iwayo, ni wazi kuwa hakuwezi kuwa na katiba itakayoweza kulinda haki za madhalimu na wadhulumiwa kwa wakati mmoja. Ingawa kwa propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja, lakini kiuhalisia ni nchi yenye jamii mbili zenye hadhi na haki tofauti kabisa. Umefika sasa wakati wa kugawana nchi ili Waislamu wanaochukiwa na kunyimwa fursa sawa na Wakristo waishi katika maeneo yenye Waislamu wengi na Wakristo waishi katika maeneo yenye Wakristo wengi. Mwalimu Nyerere alipigania kwa nguvu zake zote Nigeria igawanywe ili Wakatoliki ambao walikuwa wanadhulumiwa Nigeria wajitenge na waruhusiwe kuishi katika nchi ya Biafra. Na katika kijitabu alichokiandika 1966 Nyerere alisema madai ya kuhifadhi umoja wa kitaifa wa Nigeria hayana maana yoyote pale ambapo baadhi ya raia wa taifa hilo wanadhulumiwa. Ushahidi wa dhulma za Waislamu upo wazi. Kugawana nchi kutawawezesha Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC bila ya kuwakera Maaskofu. Ni wajibu wetu kulifikisha hili kwa Waislamu wenzetu nchi nzima ili lijadiliwe zaidi kabla halijafikishwa rasmi

   (4) Kwa kuwa hakuwezi kuwa na amani ya kweli bila ya haki, na kwa kuwa amani ya Tanzania inashikiliwa na Waislamu walioruhusu dhulma hiyo, Waislamu tunayo dhima kubwa kwa kustawi kwa Mfumo Kristo ambao sasa hapana shaka yoyote unalisambaratisha Taifa. Lakini kama alivyosema Nyerere, anayedhulumiwa ni mtu anayeteseka. Asipopambana na huyo dhalimu, yeye ataendelea kuteseka wakati dhalimu anastarehe kwa amani. Akiamua kupambana, wote yeye na dhalimu watateseka. Baada ya miaka 50 ya kuachia kundi moja la jamii likistarehe na hali Waislamu wanateseka, umefika wakati sasa wa kugawana machungu ya udini tuliyoyabeba peke yetu kwa miaka hamsini.


   WABILLAHI TAWFIQ
   [​IMG] [​IMG] Reply [​IMG] Reply With Quote [​IMG] Thanks
  • Remove Your Thanks
   The Following 39 Users Say Thank You to Topical For This Useful Post:

   Adili (20th January 2011), Aikaotana (19th January 2011), Anold (21st January 2011), Baba Mtu (19th January 2011), babayah67 (19th January 2011), ByaseL (20th January 2011), Fernandes Rodri (19th January 2011), Ibrah (20th January 2011), Invisible (19th January 2011), Junius (21st January 2011), KALAMAZOO (20th January 2011), kalamuzuvendi (19th January 2011), KAUMZA (20th January 2011), kayumba (21st January 2011), kishalu (21st January 2011), Lekanjobe Kubinika (20th January 2011), limited (19th January 2011), M TZ 1 (19th January 2011), mapambano (20th January 2011), matungusha (22nd January 2011), MFUKUNYUKU (21st January 2011), Mohammed Shossi (19th January 2011), mpevu (19th January 2011), Mtumishi (19th January 2011), muhogomchungu (19th January 2011), Mzee Mwanakijiji (19th January 2011), Nyumbu- (21st January 2011), Nyunyu (19th January 2011), oba (20th January 2011), Questt (20th January 2011), Recta (20th January 2011), rreporter2010 (20th January 2011), Safari_ni_Safari (20th January 2011), Shkh Yahya (21st January 2011), Sn2139 (20th January 2011), STEIN (20th January 2011), Steve Dii (19th January 2011), Wun (24th January 2011), Xuma (21st January 2011) ​


   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
 14. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  No comment
   
Loading...