Tamko la UWABATA juu ya vifurushi

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
23,363
47,938
Ndugu zangu wa (UWABATA),Chama Cha wanaume bahiri Tanzania hili swala tusiliache lipite hivihivi!,moja kwa moja Kama UWABATA limenishika na kuniteteresha kiuchumi!

Ktk pitapita nimeona kweli vifurushi vimepanda bei tena ya kutupwa!.

Kwa kufuata kauli aliyoitoa mama yetu samia rais wa jamhuli ya Muungano wa Tanzania ya kwamba "ZEGE HAILALI" Basi nasi vivyohivyo hatutakiwi kulaza damu juu ya hili,ni jambo la kuhuzunisha sana na kama chama lazima tutoe tamko ya nini kifanyike baada ya mitandao kutubadilikia!.

Kutokana na kauli mbiu yetu ya mwezi huu yani "YA KUTOLEA MWIKO" kwa mamlaka niliyonayo uongozi umeamua kubadili kauli hii ili kutia mkazo juu ya vifurushi,hivyo kauli yetu ya mwezi huu itakuwa ni "UWABATA BILA VIFURUSHI INAWEZEKANA"

Kama chama tumeamua kutonunua vifurushi ili kubana matumizi pia Kama sehemu ya mgomo na kuonyesha kutofurahishwa na mabadiliko haya!.. Uongozi umeandika barua kwenda ktk ngazi za juu na nyengine ndio tupo tunaiandika ili ikamfikie rais wetu mpendwa!,Ipo na barua nyengine itaandikwa jioni ili ikamfikie spika wa bunge! Halafu kesho katibu atawasilisha barua nyengine itakayoenda mahakama kuu maana hili ni janga la kitaifa!.

Uongozi unawaomba wanachama wake kuwa watulivu kwasasa,wale wanachama wakorofi mnaombwa kutokufika ktk ofisi za mitandao msije mkaghafirika na kuleta fujo mkapelekwa gerezani!,chama kwa sasa kinauhaba wa fedha hivyo utajitoa mwenyewe gerezani ni vyema zaidi kuwa watulivu.

NB:Wanachama mnaombwa muendelee kujitolea mchango wa kusajili chama chetu ktk ngazi ya taifa,fedha inayohitajika ni alfu ishirini (20000),mpaka Sasa imechangwa mia tano(500).. Uongozi unaomba mjitahidi ili chama kipate kusajiliwa ngazi ya taifa na baadae kimataifa.

Onyo: Tunaelekea sikukuu ya pasaka hivyo wanachama mnaombwa kuwa makini na wadada waombaji wa nauli pamoja na wale ya kutolea!,pia Uongozi unawahasa wanachama kuweka makufuri ktk mifuko yao ya kuhifadhia chochote kitu!.

Gazeti hili liwafikie wanachama wote wa UWABATA.
By mwenyekiti msaidizi madomoro mafilo nawatakia sikukuu njema.
 

Hplp2275H

JF-Expert Member
Jan 21, 2021
556
1,618
Serikali inatafuta namna ya kuuchokonoa umma uandamane.
Wanataka kuona nguvu ya umma.

Uwabata Tunalianzisha soon.
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
23,363
47,938
Serikali inatafuta namna ya kuuchokonoa umma uandamane.
Wanataka kuona nguvu ya umma.

Uwabata Tunalianzisha soon.
Hali itakapofika majinuni chama Kama chama kitawaruhusu wanachama wake kuandamana hivyo jiandaeni kwa lolote.
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom