Tamko la Rostam Aziz dhidi ya Reginald Mengi na yatokanayo. Amuita fisadi Nyangumi

Status
Not open for further replies.
hii inaonyesha jinsi gani RA alivyokuwa na fikira ndogo

manji mwezake kaweka madai ya kejeli ya tsh 1 alafu karudi nyuma RA kaingia kichwa kichwa sasa hivi atajua mahakamani kukoje

RA ana njia moja na yo ni kuwapa viongozi posho, lakini manji anajua ni nguvu ya wananchi, misaada yanga haiishi na mengi nae misaada haiishi, ukimwona mtu anamtetea RA ujue analipwa hana wider public support.

hajui corporate social responsibility
tungojee tuone kesi ya RA itakapotajwa hapo kisutu
 
Kwa nini tunataka Rostam tu ndio aende mahakamani na ushahidi wake? Mengi naye si ana ushahidi dhidi ya akina Rostam? Kwa nini asirahisishe hii kazi kwa kuwapeleka mahakamani?

Hawa wote (Mengi na Rostam) ni MAFISADI hakuna hata mmoja wao atakaye thubutu kumfunga paka kengele na kwenda Mahakamani.
 
leo sichangii kitu.
nimechoka na hawa wezi wakubwa

Heri Mimi sijasema...... nakumbuka mbali

hii inaonyesha jinsi gani RA alivyokuwa na fikira ndogo

manji mwezake kaweka madai ya kejeli ya tsh 1 alafu karudi nyuma RA kaingia kichwa kichwa sasa hivi atajua mahakamani kukoje

RA ana njia moja na yo ni kuwapa viongozi posho, lakini manji anajua ni nguvu ya wananchi, misaada yanga haiishi na mengi nae misaada haiishi, ukimwona mtu anamtetea RA ujue analipwa hana wider public support.

hajui corporate social responsibility
tungojee tuone kesi ya RA itakapotajwa hapo kisutu

Toa hoja zako wewe sio unalialia hapa kila mtu ana UHURU wa kutoa maoni yake WEWE UNAYEMTETEA MENGI UNALIPWA NA NANI? BESIDES KUMSEMA MENGI HAINA MAANA UNAMTETEA RA..... hapo ndio watu WENGI naona mnakosea SANA TENA SANA. huwezi kumtetea RA kwa kumponda MENGI and viceverse otherwise MNAONYESHA MAPUNGUFU YA AJABU KWENYE HOJA ZENU WOTE MNAOEGEMEA SIDE MOJA, tunataka hoja TUMECHOKA NA BLABALA ZENU wote mnaolipwa na hao MAPAPA/NYANGUMI mkumbuke huko AHELA mna FUNGU LENU pia linawasubiri, EBOOOOO!
 
Huo ni mchezo wa kuigiza,labda kama si TAA KUKURU ya Hosea.

Fisadi papa Rostamu Azizi bado anaota njonzi za RICHMOND, akiamini TAKUKURU itatoka na tangazo kama lile lile kwamba RICHMONDI safiiiiii..

Kamuulize swahiba wako Lowasa, Watanzania sio wa siku zile wa kushangilia matamko ya ajabu ajabu bila kutafakari!
 
RA ni fisadi tuu ila kwa kuwa uongozi ulioko madarakani amechangia mafanikio yake kwa ufisadi wake ndio maana hawamgusi lakini ni suala la muda tuu ngoma itapasuka hawezi kutamba siku zote katika nchi hii kwa kutawala kwa mlango wa nyuma wakati hana ridhaa ya wananchi.
 
Fisadi papa Rostamu Azizi bado anaota njonzi za RICHMOND, akiamini TAKUKURU itatoka na tangazo kama lile lile kwamba RICHMONDI safiiiiii..

Kamuulize swahiba wako Lowasa, Watanzania sio wa siku zile wa kushangilia matamko ya ajabu ajabu bila kutafakari!

- Mafisadi wamelia sana huko CC, eti kwa nini serikali inaruhusu wajumbe wa CC kama Rostam kutukanwa hadharani, Muungwana akaua hoja tena kwa ukali sana huku Rostam akimuangalia kwa jicho la huzuni sana, sasa Rostam ameenda Takukuru kudai Sheria ya Section 37 ya PCC Act itumike mara moja kumbana Mengi asizungumzie tena hii ishu mpaka uchunguzi utakapoisha, masikini ya Mungu hakujua kuwa Mengi tayari ameshafungua kesi, sasa inapendeza sana!

Mungu Aibariki Tanzania.

FMES!
 
Tetesi ama kuna ukweli? Kesi gani amefungua na lini? Takukuru ina mamlaka ya kumzuia mtu asiongelee kitu? Mimi nilidhani ni mahakama tu nelewesheni jamani. Mambo yameiva WEE NEED ACTIONS sio promotion za MAGAZETI a.k.a BLA BLA.
 
- Chenge amelia sana huko CC kwamba kwa nini wajumbe wanashambuliwa na serikali imenyamaza kimyaa, Rostam anataka Takukuru wamnyamazishe Mengi kwa kutumia Section 37 ya PCC Act mpaka uchunguzi uishe, hii ni aibu sana!

FMEs!
 
Habari za siku nyingi wana Jamii,

Naomba niingilie kati kwa jinsi navyofikiri mimi au kwa uwelewa wangu,

Hivi nyie hamjui kuwa mwaka 2010 ni kesho kutwa kila mtu anajikosha ili aonekane mwema, Mimi tangu nimezaliwa sijawahi kuona mzalendo anayetetea maslai ya nchi yake akaficha misaada anayoipata, Mengi amekuwa kihelehele mkubwa wa kutumia vyombo vyake vya habari kujisafisha na kuonekana mwema. kuna msemo mmoja unasema "umzaniye ndiye kumbe siye" Kwahiyo sioni sababu ya yeye kutumia vyombo vyake vya habari kujifanya anafichua siri za mafisadi papa wakati wote huo alikuwa wapi? Kwani wameanza leo? mengi asitake kutufanya sisi watoto wadogo bwana yeye mwenyewe anamaovu sana.

Anatumia vyombo vyake kujisafisha na kuonekana mwema tena alivyomjanja anajua kweli kutupata wakati wa shida yeye ndiye wa kwanza kutumia vyombo vyake kutangaza misaada aliyotoa wapo wengi wenye fedha tena zaidi yake ambao wanajua maaana ya kutoa msaada ukitaka kumsaidia mtu usijitangaze ukajisifia acha wanao ona wakusifie sasa yeye amekuwa mjanja wa kujisifia sana na kutaka kuonekana mwema na mara zote anaona kama anaonewa.

mimi naomba kitu kimoja jamani tuwe makini sana na hawa watu hasa kama wakina Mengi wanalengo la kuvuruga Amani ya Tanzania wakigombana wenyewe wanatumia wananchi ambao ndio wanaoangamia kujikosha na kukandamiza wengine huu wizi/kurindana haujaanza leo bwana tangu miaka ya nyuma Nyerere na utawara wake aliyekuwa mtovu wa nidhamu alikuwa anahamishwa na kupelekwa kitengo kingine acha wanaoweza kula wale "Nchi hii italliwa na wenye meno" Ndio maana huwa na msemo mmoja Mchawi mpatie mwana akulelee nasema tena mtu yoyote ambaye anajitokeza leo hii kutoa maovu ya watu kwangu ni mnafki siku zote alikuwa wapi?
 
Duu mwanaharakati,
Kwahiyo mtu akiona maovu asiseme kwa vile huko nyuma alikuwa hajasema? hivi unadhani swala ni kuona na kusema ama mpaka uwe umefanya uchunguzi na kujiridhisha kabla ya kusema? Mwana harakati fikiria tena mawazo yako nadhani unaweza ukawaza vema zaidi ya hapa hasa kwa ajili ya kulikomboa taifa letu midomoni mwa hao unao waita wenye meno.

Hii nchi ni yetu wote, kama meno kila mtu anayo, jiondoe kabisa katika kundi la vibogoyo, ukiamua tu na weye yako yatauma. karibu sana katika kundi la wapambanaji dhidi ya wadhurumaji ( uikwaita wenye meno)
 
Section 37 ya PCC Act inasemaje?

Soma hapa. KIfupi inazuia mtu yeyote kujadili jambo lililoko kwenye mikono ya TAKUKURU kwa uchunguzi. Ndio kimbilio la RA kuzima HOJA zinazokuja.

Sheria hii ya TAKUKURU haifai kabisa - Wanahabari

Sheria hii ya TAKUKURU haifai kabisa - Wanahabari

2007-08-02 10:25:29
Na Mwandishi Wetu

Wadau wa habari jijini Dar es Salaam, wameelezea kutoridhishwa kwao na kifungu namba 37 cha Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2007 iliyoanza kutumika Julai Mosi, mwaka huu kwamba kinabana uhuru wa habari.

Kifungu hicho cha Sheria, kinawazuia wanahabari kuripoti tuhuma ambazo zinafanyiwa uchunguzi na TAKUKURU.

Hayo yalijitokeza wakati wa kikao cha wawakilishi wa wahariri, Baraza la Habari la Taifa (MCT) na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Edward Hosea, pia alihudhuria kikao hicho ambapo wadau hao wa habari, walitaka kupata ufafanuzi kuhusiana na suala hilo.

Mwenyekiti wa kikao hicho cha wahariri, Bi. Sakina Datoo, alisema wahariri wamepata wakati mgumu mno baada ya kupata taarifa ya hivi karibuni ya TAKUKURU ambayo ilikuwa maalum kuwaonya waandishi wa habari kuzingatia matakwa ya sheria katika kuandika habari za rushwa zinazofanyiwa uchunguzi.

Taarifa hiyo ya TAKUKURU, iliyotolewa Julai 20, mwaka huu, pia ilieleza kuwa, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, atazungumza na waandishi wa habari juu ya masuala ambayo anadhani jamii inastahili kuyafahamu.

``Sheria hii inapingana na dhana nzima ya Uandishi wa Habari wa Kiuchunguzi. Kuanzia sasa, wanahabari wanashambuliwa. TAKUKURU inapambana na rushwa.

Walikuwa ni wenzetu. Sasa tutakuwa ni wasemaji tu wa kile taasisi itakachokisema,`` alisema Datoo.

Akitetea hoja hiyo, Bw. Hoseah alisema taasisi hiyo inaendeshwa kwa misingi ya sheria. Akielezea kuhusu kifungu cha sheria namba 37 kinacholalamikiwa, alisema ``hivi ndivyo sheria inavyosema.

Sheria imetungwa na Bunge, siyo TAKUKURU. Hainyimi uhuru wa vyombo vya habari.

Tunapaswa twende pamoja jinsi inavyotakiwa kutumika.``
Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa MCT, Bw. Anthony Ngaiza, alisema: ``Sheria hii ni janga kwa vyombo vya habari.

TAKUKURU haiwezi kufanya kazi bila vyombo vya habari. Unapofanya kazi kwa maslahi ya taifa, huo ni msamaha tosha. Lazima tupambane na sheria hii.``

Kifungu hicho cha Sheria namba 37, kinamzuia mtu yeyote kutoripoti tuhuma zozote zinazohusiana na rushwa bila kibali cha mamlaka husika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MOAT, Bw. Reginald Mengi alikiambia kikao hicho kuwa, taarifa ya TAKUKURU ``imetushtua. Tuko hapa kufahamu maana ya sheria hii. Imelenga nini? Imelenga kumlinda mtu au shauri?``

Wakati wa majadiliano, wachangiaji wengi walihoji jinsi gani vyombo vya habari vitafahamu kama mtu wanayemripoti anachunguzwa na TAKUKURU.

Wadau hao wa habari, walitoa wito wa kuendelea zaidi kwa majadiliano kati yao na TAKUKURU ili kuhakikishwa kwamba vyombo hivyo viwili, vinakwenda pamoja kuhusiana na sheria hiyo.

  • SOURCE: Nipashe
 
ROSTAM hajapeleka vielelezo TAKUKURU bali kawapelekea taarifa ya sehemu ambazo TAKUKURU hawaruhusiwi kupekua. By the way, ni TAKUKURU hii ya Mchungaji wa MAFISADI, Mpakwa Mafuta wa CCM, Mtume wa SERIKALI na Nabii wa WAALIFU, namaanisha ni TAKUKURU hii ya anayejiita Dr.? Edward Hosea......ni sawa na kesi ya kumfumania mkeo hakimu awe mgoni wako.
 
Dah! Rostam anatapatapa sasa ivi mpaka raha.....!!na hakika uko aliko hata chakula hakipiti..kama mgonjwa vile...hehehehe!!! mtu na mihela yake..nakini raha hamna..hahaha!! kweli ufisadi ni mateso dah!! angetulia tu na hela zake za kihalali za urithi...sasa mungu anamuadhibu kwa ulafi na tamaa zake..uku akimtumia jemedari wake bwana mengi kumsulubu...... na wananchi tuko nyuma yake tukimpa support ya nguvu ili atimize kazi yake aliyotumwa na mungu ( kusulubu mafisadi...hasahasa Rostam)....Go Mzee!! wananchi tushaelewa sasa pumba ni zipi mchele ni upi..sasa umebakia na kazi nyepesi tu ya kuangusha hiyo empire ya mafisadi...kikubwa ilikua ni wananchi kuelewa mkweli na mzushi ni nani...na tumeshaelewa..baas!! sasa ni kuchapa tu mzee wetu huku sisi tukikushangilia..ukishindikana tutaingia sisi wenyewe mashabiki ( maana huu mpambano hata refa hauna)...mpaka tuwaangushe hawa wanyonyaji ........but i knw kwa nguvu zetu wote ..tutashinda tu!!!! ivi uyu Pundamilia ni kibaraka wa Rostam nini??? au ni Balile uyu!?
 
- Now look at this, anasema yeye Rostam ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi na kupewa dhamana nzito ya kuongoza, sasa anangoja nini kujiuzulu kwa kushindwa kutimiza wajibu wake wa kufichua "mafisadi" kama Mengi, against wananchi waliomchagua? Badala yake anasubiri aumbuliwe kwanza? Hana hata aibu huyu mkuu?

- Hapa kifungu cha tatu, sasa anaweka wazi ukweli wake kwamba kumbe wanatuibia taifa kwa sababu hakuna kiongozi wa kutusemea wananchi! Ndio maana nilisema huyu Rostam angekua na akili sana kama inavyosemekana basi angekimbilia kwenye sheria bila hizi kelele, kwa sababu jamaa politically ni mtupu sana ni mtu anayetegmeea kutumia njaaa za sisi wananchi wka faida yake tu!

-Nitaendelea kumchambua hii habari yake pole pole na sitaki kuamini kwamba huu ndio ushahidi alioupeleka Taukukuru?

FMES!

Mkuu umesema ukweli mtupu.

Kinachooneka katika sakata hili, ni lawama za "kwanini unanisema, wakati mimi sijakusema?" Mengi anaeleweka kuwa ni mlalamishi sana. Kama mfanyabiashara asiekubali kushindwa, amekuwa akitaka kufanikiwa kwa njia zozote. RA pia ni mtu wa hulka hiyo hiyo ya Mengi. Watu hawa hawana tofauti sana. Tofauti yao kubwa kwa sasa ni nani ana influence kubwa ya kufaidi matunda ya nchi hii kuliko mwenzake. Katika hili RA anaelekea kushika mpini.
 
Sikilizeni jamani. Kuna azimio la Bunge kuhusu kinara wa Takukuru Bwana Hosea ambalo linasema achukuliwe hatua za kinidhamu kuhusu kuboronga uchunguzi wa Richmond. Inasemekana Hosea alipewa maagizo na wakubwa jinsi ya kuandika ripoti ya Takukuru. Unategemea nini kutoka ofisi hii? Ingawa hatujaona vielelezo vya Rostam ni dhahiri kwamba madai yake hayafanani fanani na Ufisadi. Kushindwa kulipa mikopo si ufisadi labda kama mikopo yenyewe ilipatikana kwa ujanja na kugushi. Bishara ya InterChem ni ya mdogo wake Mengi ambaye ni mtu mzima hata hivyo Mengi katoa "evidence" kwamba hakuhusika na alisha jihudhuru Bodi Ya Nico. Sisi tunataka mafisadi waliofanya yafuatayo-

1) Kutoa hongo na kupokea rusha kama vile Radar na Ndege ya Rais
2) Kukwapua pesa kwa Ujanja kama EPA, Deep Green na Meremeta
3) Kuunda kampuni hewa (shell companies) kwa ajili ya biashara haramu
4) Kukwepa kulipa kodi ya serikali
5) Kutumia madaraka ya ofisi ya umma vibaya
6) Kufuja mali ya Umma
7) Kujipatia mali kama vile ardhi kwa njia ya udanganyifu.

Kama Mengi kafanya moja wapo ya haya basi naye ni FISADI which I doubt. Mbio za Roostam are the last kicks of a dying horse.
 
Mengi asipeleke mpaka kesi ifunguliwe na yeyote kwani TAKUKURU ni zao la akina Rostam

Mwambieni asitupe kneejerk reaction!!!!!!!!!! Kwani kama Rostam alijipanga basi angefanya ki-master kama aliyoiba

Dwon with the fisadis

TAKUKURU iliyoisafisha Richmond/Dowans ya Rostam? (bila mafanikio of course)
Mengi USILOGWE ukapeleka vielelezo huko, watampelekea RA, na watajaribu kuvipotosha.
Kaa navyo. Keep tight hadi kesi Mahakamani.
RA aka the real president anapeleka TAKUKURU kwa kuwa anajua ni watu wake.
Shame on mafisadi!
 
Hapana, ila ana uchungu na madeni yanayoua makampuni ya Taifa. Na amekuwa mtu wa kwanza niliyewahi kumsikia kapeleka ushahidi TAKUKURU wa hao watu HAZINA wanaokula na Mengi.

Mengi ametoa stakabadhi lukuki za malipo ya madeni ya Bonite bottlers lakini wakili hakuonyesha, na kama kungekuwa na mwandishi wa maana angeomba aonyeshwe, nyaraka inayosema deni limelipwa lote, collection account imefungwa. Huwezi kuonyesha vistakabadhi vya payment plan uliyoanza kulipa lipa wakati collection officials wa benki wanakusumbua sumbua. Tuonyeshe nyaraka ya tamati la hilo deni.

Zaidi, wakili wa Mengi akadai deni la kampuni tanzu ya IPP, Anche Mwedu sijui AntiMwedu sio halali kwa sababu NBC walidhamini tu kuingizwa kwa bidhaa za Mengi. Hili dili lilikuwa ni la Mengi na "kampuni ya Kihindi" ya kutengeza chupa za chai. Mengi akaletewa mashine za kutengeza balbu badala ya chupa za chai, yani "katapeliwa" na hao wahindi, kwa mujibu wa wakili wake. NBC ilipoanza kudai Mengi akawaruka, na kesi iko kwenye rufaa, maana yake kesi haijafikia finality, NBC bado wanawadai hao Enchi Mwedo, kama bado haja declare bankruptcy huyo Mzee Mengi.

Kwa hiyo, kama benki zinafilisika, moja ya sababu ni write-off accounts za delinquent creditors. Na katika hao, Rostam anaonyesha, fingerprints za Mengi zimejaa kwenye collection accounts za ma benki kama NBC.

Uwezo mzuri wa kufikiri TATIZO NI NAMNA YA KUFIKIRI"NBC IPI ???"
 
Kuna kitu kimoja ambacho hamjakielewa kwa nini Rostam kaenda TAKUKURU. Ni hivi huu ni mtego kwa mengi ili kwamba nae ajibu mapigo kwa kupeleka vielelezo vyake dhidi ya tuhuma za RA huko huko ili hatimaye TAKUKURU ile ile iliyoitakasa Richmond imchunguze na imwondolee tuhuma za ufisadi Mh RA.

Namshauri Mengi kama ana ndoto za kupeleka ushahidi wake huko TAKUKURU aache kabisa maana tunajua nyaraka nyeti ambazo zingethibitisha wizi wa Rostam walishaziiba kuanzia BRELA hadi BoT. Certificates of Incorparation za Richmond nazo hazipo tena kule BRELA maana Richmond ilifutwa rasmi kwenye daftari la msajiri wa makampuni mwaka jana rasmi. Labda ushahidi pekee unaweza kumsadia ambao sijui kama una nguvu za kisheria ni Ripoti ya kamati ya Dr. Harrison Mwakyembe (MB).

NI hayo tu wakuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom