Tamko la PCT Kuhusu Sensa Nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la PCT Kuhusu Sensa Nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwamakula, Jun 15, 2012.

 1. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,891
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  PENTECOSTAL COUNCIL OF TANZANIA (PCT)
  TAMKO LA BARAZA LA MAASKOFU WA KIPENTEKOSTE KUHUSU VURUGU ZA ZANZIBAR
  1. UTANGULIZI
  Ndugu waandishi wa vyombo vya habari, tumewaiteni hapa leo ili kutoa TAMKO la Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste kuhusu vurugu zilizotokea Zanzibar tarehe 28/05/2012 na kusababisha kuchomwa kwa Makanisa na uharibifu mkubwa wa mali za Makanisa na mchakato wa Sensa.
  TAMKO hili la Maskofu wa Kipentekoste ni matokeo ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Maaskofu Wakuu wa madhehebu yote ya Kipentekoste uliofanyika tarehe 12/06/2012.
  AwaIi ya yote niwakumbusheni kuwa, nchi yetu ya Tanzania imekuwa ikisifika Ulimwenguni kote kuwa ni kisiwa cha amani na nchi ya kidemokrasia inayozingatia uhuru wa kufanya ibada, kutangaza dini na watu kukusanyika kwa masuala ya imani kwa hiari yao (kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, 1977, Ibara ya 18,19 na 20)
  2. MIHADHARA YA KIDINI
  Kumetokea uvunjifu wa Amani kwa njia ya Mihadhara huko Zanzibar. Jambo ambalo linatakiwa kuangalia chanzo chake ambacho ni kusambaza kanda za hamasa mitaani na mihadhara isiyo na kibali cha Serikali. Kanda tunazo ambazo zinauzwa mitaani bila hofu zikiwakashfu hata viongozi wa nchi bila hofu yeyote.
  Vurugu ya Zanzibar yamechomwa na kuvunjwa Makanisa 25, Biblia 55 na vitabu vya nyimbo kadhaa, wakristo kwa kumtii Mwokozi wao Kristo Yesu na viongozi wao, yaani Maaskofu wakuu, wamenyamaza na kutulia wakingoja hatua zitakazochukuliwa na Serikali yao tukufu kwa uchokozi wa namna hii, ikizingatiwa kuwa kikundi kilichohusika kina usajili kamili na viongozi wake wanajulikana. Tunaomba Wizara husika ikiangalie vizuri maana kinamkashifu hata Mufti.
  Ikizingatiwa kuwa kama zingekuwa ni qurani 55 zimechomwa na misikiti 25 dunia nzima kungezuka maandamano na vurugu sehemu sehemu.
  Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste linatambua ya kwamba Serikali ya Zanzibar inakubali Makanisa kuwepo Visiwani kama yanatakiwa basi yasisumbuliwe yalindwe kisheria.
  Serikali ionyeshe imani kwa wahanga kwa kuwasaidia kujenga Makanisa yaliyobomolewa na kuhakikisha wanaoongoza harakati hizo wanakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya Dola ili sheria ichukuwe mkondo wake.

  1. SENSA
  Baraza la Maaskofu wakuu wa Kipentekoste Tanzania inatambua kuwa mwaka huu ni mwaka wa Sensa ya watu na makazi. Sensa ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa letu; hutusaidia kupata takwimu muhimu sana zinazoisaidia serikali katika mgawanyo wa rasilimali tulizo nazo.
  Baraza la Maaskofu wakuu wa Kipentekoste Tanzania inatoa wito kwa watanzania wote kushiriki kikamilifu katika sensa, kwa kuwa ni muhimu kwa ajili ya mipango, uchumi na maendeleo ya Taifa.
  Baraza la Maaskofu wakuu wa Kipentekoste Tanzania inaomba serikali kutoweka maswali yenye lengo la kutaka kujua dini, dhehebu au imani ya mtu au kabila la mtu. Maswali ya namna hii hayafai na hayana faida wala tija kwa taifa letu. Watanzania hatupaswi kutambuana kwa dini wala kabila zetu.
  Baraza la Maaskofu wakuu wa Kipentekoste Tanzania itaendelea kuwaelimisha na kuwahimiza waumini wetu kuhusu umuhimu wa sensa.
  2. HITIMISHO
  Tunapenda kuwashukuruni sana ndugu zetu waandishi wa habari kwa ushirikiano wenu na kazi nzuri mnayoifanya ya kutoa habari kwa umma wa Watanzania.
  Baraza la Maaskofu wakuu wa Kipentekoste Tanzania inawaomba Watanzania wote kuendeleza umoja wa Taifa letu na kudumisha Muungano wetu. Tusiwasikilize watu wanaotaka kutugawa kwa misingi ya udini, ubara na uzanzibar, ukabila, n.k. Watu wa aina hii in wa kuwapinga kwa nguvu zetu zote.
  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

  Nawasilisha,


  ………………………….. …..………….…………..…
  ASK. DANIEL AWETI ASK. DAVID MWASOTA
  MAKAMU M/KITI PCT-TAIFA. KATIBU MKUU-PCT

  Tarehe: Tarehe:
   

  Attached Files:

 2. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,585
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Na wengine na wengine pia watakuja na matamko yao hata tuchanganyikiwe tusijue la kuamua.
  Serikali nendeni kwenye sensa msiyumbishwe na matamko.
   
 3. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hili tamko limejaa busara, acha matamko ya kipuuzi ya Kundecha, Ponda na wajinga wenzao. Soma busara hii ya hali ya juu uelimike!
   
 4. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,814
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nakupa 100%
   
 5. H

  Hute JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,014
  Likes Received: 2,299
  Trophy Points: 280
  toka lini ishmael/ismail akashindana na isaka
   
 6. H

  Han'some JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  <3<3<3<3<3
   
Loading...