BAVICHA Taifa
Senior Member
- Jul 25, 2013
- 117
- 661
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
MKOA WA SHINYANGA.
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.
YAH: TAMKO LA KUIPONGEZA CHADEMA NA VIONGOZI KWA KUKUTANA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.
Mnamo, Mei 20, 2022 Ujumbe wa Chama ukiongozwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe ulikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ikulu- Chamwino Dodoma.
Baraza la Uongozi Mkoa Shinyanga linatambua kuwa, kwa muda mrefu sasa tumekuwa na jitihada mbalimbali za kuhitaji mazungumzo yenye lengo la kuleta maridhiano.
Aidha, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga linakumbuka taarifa ya Mwenyekiti Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe, aliyoitoa wakati akihutubia kikao cha Baraza Kuu, Mei 11, 2022 Mlimani City. Mhe Mwenyekiti Taifa alitujulisha wajumbe wa Baraza Kuu, Umma wa Watanzania na Dunia kuwa kutakuwa na mazungumzo baina ya CHADEMA, CCM na Serikali.
Hivyo, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga, linapenda kumpongeza Mhe Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, kwa kuongoza ujumbe wa CHADEMA kwenda kwenye Mazungumzo ya awali baina ya CHADEMA, CCM na Serikali yenye nia ya kuleta maridhiano katika Taifa.
CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, tunatambua nia njema ya viongozi wetu na tunaendelea kuunga mkono mazungumzo hayo ambayo tunaamini yatakuwa na tija kwa Taifa.
Mwisho, tunawatakia mazungumzo mema. Tunaanza na Mungu tutamaliza na Mungu
No Hate, No Fear.
Imetolewa leo Jumapili, 22 Mei 2022
Emmanuel Ntobi,
Mwenyekiti CHADEMA Mkoa Shinyanga.