Tamko la kuipongeza CHADEMA na viongozi kwa kukutana na Rais Samia

BAVICHA Taifa

Senior Member
Jul 25, 2013
117
661
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

MKOA WA SHINYANGA.

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

YAH: TAMKO LA KUIPONGEZA CHADEMA NA VIONGOZI KWA KUKUTANA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.

Mnamo, Mei 20, 2022 Ujumbe wa Chama ukiongozwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe ulikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ikulu- Chamwino Dodoma.

Baraza la Uongozi Mkoa Shinyanga linatambua kuwa, kwa muda mrefu sasa tumekuwa na jitihada mbalimbali za kuhitaji mazungumzo yenye lengo la kuleta maridhiano.

Aidha, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga linakumbuka taarifa ya Mwenyekiti Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe, aliyoitoa wakati akihutubia kikao cha Baraza Kuu, Mei 11, 2022 Mlimani City. Mhe Mwenyekiti Taifa alitujulisha wajumbe wa Baraza Kuu, Umma wa Watanzania na Dunia kuwa kutakuwa na mazungumzo baina ya CHADEMA, CCM na Serikali.

Hivyo, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga, linapenda kumpongeza Mhe Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, kwa kuongoza ujumbe wa CHADEMA kwenda kwenye Mazungumzo ya awali baina ya CHADEMA, CCM na Serikali yenye nia ya kuleta maridhiano katika Taifa.

CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, tunatambua nia njema ya viongozi wetu na tunaendelea kuunga mkono mazungumzo hayo ambayo tunaamini yatakuwa na tija kwa Taifa.

Mwisho, tunawatakia mazungumzo mema. Tunaanza na Mungu tutamaliza na Mungu

No Hate, No Fear.

Imetolewa leo Jumapili, 22 Mei 2022

Emmanuel Ntobi,

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa Shinyanga.
images%20(2).jpg
 
Mbowe analipa fadhila maana angesota sana jela hadi achakae , Sasa ni zamu ya kula ruzuku tu

USSR
 
Siasa za Majukwaani zunarudi Mama anaupiga mwingi.

Mama aliambiwa kuwa ADUI zake sio WAPINZANI bali wako humohumo CCM.
 
Ndugu zangu, BAVICHA. Poleni kwa majukumu ya kupigania haki katika nchi yetu. Nawapongeza kwa ujasiri wenu. Najua wajibu wenu ni kuwasapoti viongozi wenu lakini nawaambia ukweli huu hapa chini.

Je, mnajua kuwa haya mnayoyafanya leo na CCM yalipata kufanyika huko nyuma kati ya CCM na CUF ya Maalim? CCM walijifanya kuleta Mwafaka ili watawale kwa utulivu ili wakisubiri uchaguzi ufike ili waibe kura tena. Na Tume huru feki ikaundwa Zanzibar. Na 2015, Maalim alipowashinda kwenye sanduku la kura, wakafuta matokeo. Samia anataka Mwafaka mwingine sasa na CHADEMA ili atawale bila kusikia makongamano ya katiba ama vurugu nyingine. Ikifika 2025, ndio mtamjua vizuri. Amekwishasema kuwa anataka kuwa Rais mpaka 2030. Hataki upinzani wowote nje wala ndani ya CCM. Na anajua kuwa hawezi kuwa Rais kwa uchaguzi huru na wa haki.

Mabadiliko ya kweli ni pale CCM itakapolazimishishwa kuleta Katiba mpya. Watu mashuhuri km Waryoba, Butiku, Mkapa (RIP), nk walikwishaunga mkono hili swala la Katiba mpya. Nyie kazi yenu ingekuwa ni kuilazimisha CCM kuleta ile Katiba ya wananchi. Wakilazimishwa kupitia nguvu ya wananchi, wataleta Katiba ambayo wataiheshimu kwa kuogopa wananchi. Njia sahihi ni ile mliyoitumia kabla Mbowe hajapakaziwa ugaidi. Pale ndipo CCM ilipigwa panapouma. Lakini haya mazungumzo ya Ikulu, naona hali ile ya Zanzanibar 2015 ikijirudia 2025.

Atakayekuja 2030 (wa CCM), atandelea hivyo hivyo. CCM wanajua "wanavyoshinda" hizi chaguzi. Wanajua wizi ndio unawasaidia. Wataendelea kupokezana kijiti hivi hivi kwa ghirba. Msijidanganye. Mwaka 1992 mkapa leo ni muda wa kutosha kabisa kuwaelewa CCM. CCM ni ile ile.
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

MKOA WA SHINYANGA.

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

YAH: TAMKO LA KUIPONGEZA CHADEMA NA VIONGOZI KWA KUKUTANA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.

Mnamo, Mei 20, 2022 Ujumbe wa Chama ukiongozwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe ulikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ikulu- Chamwino Dodoma.

Baraza la Uongozi Mkoa Shinyanga linatambua kuwa, kwa muda mrefu sasa tumekuwa na jitihada mbalimbali za kuhitaji mazungumzo yenye lengo la kuleta maridhiano.

Aidha, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga linakumbuka taarifa ya Mwenyekiti Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe, aliyoitoa wakati akihutubia kikao cha Baraza Kuu, Mei 11, 2022 Mlimani City. Mhe Mwenyekiti Taifa alitujulisha wajumbe wa Baraza Kuu, Umma wa Watanzania na Dunia kuwa kutakuwa na mazungumzo baina ya CHADEMA, CCM na Serikali.

Hivyo, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga, linapenda kumpongeza Mhe Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, kwa kuongoza ujumbe wa CHADEMA kwenda kwenye Mazungumzo ya awali baina ya CHADEMA, CCM na Serikali yenye nia ya kuleta maridhiano katika Taifa.

CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, tunatambua nia njema ya viongozi wetu na tunaendelea kuunga mkono mazungumzo hayo ambayo tunaamini yatakuwa na tija kwa Taifa.

Mwisho, tunawatakia mazungumzo mema. Tunaanza na Mungu tutamaliza na Mungu

No Hate, No Fear.

Imetolewa leo Jumapili, 22 Mei 2022

Emmanuel Ntobi,

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa Shinyanga.View attachment 2234597
 
Bavicha na nyie mnaanza kuiga ujinga wa CCM kusifia viongozi. Huu upuuzi ndio umetufikisha hapa kama taifa kwa kusifia mambo yasiyo na ulazima. Matokeo yake upambe ndio imekuwa sifa ya mwanachama na sio utendaji. Acheni huu ujinga mara moja, toeni sifa baada ya kuona tija ya huo mkutano, tena sio hizo sifa za kiduwanzi.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

MKOA WA SHINYANGA.

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

YAH: TAMKO LA KUIPONGEZA CHADEMA NA VIONGOZI KWA KUKUTANA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.

Mnamo, Mei 20, 2022 Ujumbe wa Chama ukiongozwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe ulikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ikulu- Chamwino Dodoma.

Baraza la Uongozi Mkoa Shinyanga linatambua kuwa, kwa muda mrefu sasa tumekuwa na jitihada mbalimbali za kuhitaji mazungumzo yenye lengo la kuleta maridhiano.

Aidha, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga linakumbuka taarifa ya Mwenyekiti Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe, aliyoitoa wakati akihutubia kikao cha Baraza Kuu, Mei 11, 2022 Mlimani City. Mhe Mwenyekiti Taifa alitujulisha wajumbe wa Baraza Kuu, Umma wa Watanzania na Dunia kuwa kutakuwa na mazungumzo baina ya CHADEMA, CCM na Serikali.

Hivyo, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga, linapenda kumpongeza Mhe Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, kwa kuongoza ujumbe wa CHADEMA kwenda kwenye Mazungumzo ya awali baina ya CHADEMA, CCM na Serikali yenye nia ya kuleta maridhiano katika Taifa.

CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, tunatambua nia njema ya viongozi wetu na tunaendelea kuunga mkono mazungumzo hayo ambayo tunaamini yatakuwa na tija kwa Taifa.

Mwisho, tunawatakia mazungumzo mema. Tunaanza na Mungu tutamaliza na Mungu

No Hate, No Fear.

Imetolewa leo Jumapili, 22 Mei 2022

Emmanuel Ntobi,

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa Shinyanga.View attachment 2234597
Naunga mkono ila twende taratibu pongeza pongeza hizi wamezoea Sana upande ule , tafadhalin ,tafadhalin,
 
Ndugu zangu, BAVICHA. Poleni kwa majukumu ya kupigania haki katika nchi yetu. Nawapongeza kwa ujasiri wenu. Najua wajibu wenu ni kuwasapoti viongozi wenu lakini nawaambia ukweli huu hapa chini.

Je, mnajua kuwa haya mnayoyafanya leo na CCM yalipata kufanyika huko nyuma kati ya CCM na CUF ya Maalim? CCM walijifanya kuleta Mwafaka ili watawale kwa utulivu ili wakisubiri uchaguzi ufike ili waibe kura tena. Na Tume huru feki ikaundwa Zanzibar. Na 2015, Maalim alipowashinda kwenye sanduku la kura, wakafuta matokeo. Samia anataka Mwafaka mwingine sasa na CHADEMA ili atawale bila kusikia makongamano ya katiba ama vurugu nyingine. Ikifika 2025, ndio mtamjua vizuri. Amekwishasema kuwa anataka kuwa Rais mpaka 2030. Hataki upinzani wowote nje wala ndani ya CCM. Na anajua kuwa hawezi kuwa Rais kwa uchaguzi huru na wa haki.

Mabadiliko ya kweli ni pale CCM itakapolazimishishwa kuleta Katiba mpya. Watu mashuhuri km Waryoba, Butiku, Mkapa (RIP), nk walikwishaunga mkono hili swala la Katiba mpya. Nyie kazi yenu ingekuwa ni kuilazimisha CCM kuleta ile Katiba ya wananchi. Wakilazimishwa kupitia nguvu ya wananchi, wataleta Katiba ambayo wataiheshimu kwa kuogopa wananchi. Njia sahihi ni ile mliyoitumia kabla Mbowe hajapakaziwa ugaidi. Plae ndio CCM ilipigwa panapouma. Lakini haya mazungumzo ya Ikulu, naona hali ile ya Zanzanibar 2015 ikijirudia 2025.

Atakayekuja 2030 (wa CCM), atandelea hivyo hivyo. CCM wanajua "wanavyoshinda" hizi chaguzi. Wanajua wizi ndio unawasaidia. Wataendelea kupokezana kijiti hivi hivi kwa ghirba. Msijidanganye. Mwaka 1992 mkapa leo ni muda wa kutosha kabisa kuwaelewa CCM. CCM ni ile ile.
Mkuu binafsi naona hoja yako imeshiba Sana ,thanks,
 
Alipofanya Zito alionekana mpuuzi, saiv kafanya Mbowe yuko sahihi na anapigiwa makofi.
 
Naona mmekubali sasa na hadi Pongezi mnatoa.. Mliwacheka sana ACT mkajifanya wajanja sana.. Haya sasa mnekula matapishi yenu.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

MKOA WA SHINYANGA.

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

YAH: TAMKO LA KUIPONGEZA CHADEMA NA VIONGOZI KWA KUKUTANA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.

Mnamo, Mei 20, 2022 Ujumbe wa Chama ukiongozwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe ulikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ikulu- Chamwino Dodoma.

Baraza la Uongozi Mkoa Shinyanga linatambua kuwa, kwa muda mrefu sasa tumekuwa na jitihada mbalimbali za kuhitaji mazungumzo yenye lengo la kuleta maridhiano.

Aidha, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga linakumbuka taarifa ya Mwenyekiti Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe, aliyoitoa wakati akihutubia kikao cha Baraza Kuu, Mei 11, 2022 Mlimani City. Mhe Mwenyekiti Taifa alitujulisha wajumbe wa Baraza Kuu, Umma wa Watanzania na Dunia kuwa kutakuwa na mazungumzo baina ya CHADEMA, CCM na Serikali.

Hivyo, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga, linapenda kumpongeza Mhe Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, kwa kuongoza ujumbe wa CHADEMA kwenda kwenye Mazungumzo ya awali baina ya CHADEMA, CCM na Serikali yenye nia ya kuleta maridhiano katika Taifa.

CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, tunatambua nia njema ya viongozi wetu na tunaendelea kuunga mkono mazungumzo hayo ambayo tunaamini yatakuwa na tija kwa Taifa.

Mwisho, tunawatakia mazungumzo mema. Tunaanza na Mungu tutamaliza na Mungu

No Hate, No Fear.

Imetolewa leo Jumapili, 22 Mei 2022

Emmanuel Ntobi,

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa Shinyanga.View attachment 2234597

Vijana wa Tanzania Wote wawe UVCCM au BAVICHA Wote hawajui kuwa hawa wazee wa nchi hii lao ni moja hawatakii mema wao na kizazi kijacho kwa matendo yao wanayoifanyia nchi. Wangekuwa wanajitambua wote kwa pamoja wangekuwa wanapinga ufisadi unafanyika kuhujumu nchi na wao wanaambulia makombo na mzigo wa madeni ambao itawabidi waulipe wakati hawa wazee watakaokuwa wamekwisha liwa na funza!!
Inashangaza kuona wote wanashangilia umoja wanaounda kutaka watawale milele kwa kigezo cha siasa za kistaarabu; bila kuwalazimisha hawa wazee wote huko CCM na Chadema hawawezi kuondoka kwa hiari!! Mnajidanganya kuwa eti wanawatayarishia ili mje kuwa na nchi ya Amani wakati nchi ndio inazidi kuwa masikini!!
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

MKOA WA SHINYANGA.

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

YAH: TAMKO LA KUIPONGEZA CHADEMA NA VIONGOZI KWA KUKUTANA NA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.

Mnamo, Mei 20, 2022 Ujumbe wa Chama ukiongozwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa Mhe Freeman Mbowe ulikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ikulu- Chamwino Dodoma.

Baraza la Uongozi Mkoa Shinyanga linatambua kuwa, kwa muda mrefu sasa tumekuwa na jitihada mbalimbali za kuhitaji mazungumzo yenye lengo la kuleta maridhiano.

Aidha, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga linakumbuka taarifa ya Mwenyekiti Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe, aliyoitoa wakati akihutubia kikao cha Baraza Kuu, Mei 11, 2022 Mlimani City. Mhe Mwenyekiti Taifa alitujulisha wajumbe wa Baraza Kuu, Umma wa Watanzania na Dunia kuwa kutakuwa na mazungumzo baina ya CHADEMA, CCM na Serikali.

Hivyo, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga, linapenda kumpongeza Mhe Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, kwa kuongoza ujumbe wa CHADEMA kwenda kwenye Mazungumzo ya awali baina ya CHADEMA, CCM na Serikali yenye nia ya kuleta maridhiano katika Taifa.

CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, tunatambua nia njema ya viongozi wetu na tunaendelea kuunga mkono mazungumzo hayo ambayo tunaamini yatakuwa na tija kwa Taifa.

Mwisho, tunawatakia mazungumzo mema. Tunaanza na Mungu tutamaliza na Mungu

No Hate, No Fear.

Imetolewa leo Jumapili, 22 Mei 2022

Emmanuel Ntobi,

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa Shinyanga.View attachment 2234597
kwishney!
 
Muendelee kumuita Hayati "Mwendazake" mtabaki kuridhiana mpaka mbadilishe mihemeko yenu ...ya Kibinafsi.

Wananchi wanawaangalia. Macho Kodo masikio ardhini

Tuwekeeni ajenda yenu pia, sio kila kukicha pongezi tu.. Pongezi haitoi au kupunguza makali ya bei panda tuuu, haipunguzi madeni tunayowarithisha vijana wetu, rushwa, ufuataji wa sheria na katiba....majipujipu N.k

Chadema lazima ijitathmini na ujumbe mtakao pelekea wananchi, Katiba Mpya sio Uchumi mpya, Wananchi wanahitaji uchumi wa kujumuisha wote....yaliyopita yamepita. Tugange mbele.

Tupo pamoja.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom