Elections 2010 Tamko la kuahirisha uraia

Isaac

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
1,400
1,176
Mimi Isaac 'Ankali' leo tarehe 5 November 2010,natamka kwa hiari yangu bila kushurutishwa na yeyote kuwa ninaahirisha Utanzania wangu kwa kipindi cha miaka 5. Uamuzi huu unakuja baada ya kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi na kutangazwa kwa mshindi ambaye sikumchagua.
Sambamba na tamko hili ninautangazia umma kuwa mimi si mmoja wa walioitoa nchi yangu kwa mafisadi. Ninaipenda nchi yangu na nitarejea kuwa raia wa Tanzania mara tu ccm itakapoondoka madarakani miaka 5 ijayo.
Pia,kwa kipindi chote nitakachokuwa nimesitisha Uraia nitaendelea kumtambua Dr. Wilbrod Peter Slaa kuwa Rais halali wa Tanzania na nitatimiza yote atakayoagiza. Vilevile nitamtambua Fred Mpendazoe kuwa mbunge halali wa Segerea.

N.B: Niko tayari kuwajibika kwa uamuzi wangu huu mzito.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom