Tamko la Kafulila kwa Umma (kufuatia mbunge wa Bahi kukamatwa kwa Rushwa)...

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
WAKATI Mbunge wa Bahi, Omar Badwel anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za kupokea rushwa, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ameilipua Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) kuwa imekithiri kwa rushwa.

Kutokana na tuhuma hizo, Kafulila amemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuvunja kamati hiyo, vinginevyo yeye atajiondoa.

Pia mbunge huyo ameitaka Kamati ya Maadili kulitumia Bunge kumvua ubunge, Badwel, kutokana na tuhuma za kupokea rushwa zinazomkabili.

Kafulila alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari huku akisisitiza kuwa, wananchi hawatakuwa na imani tena na kamati hiyo.

"Ikumbukwe Juni 13, 2011 nilieleza bungeni namna wabunge wa Kamati ya LAAC wanavyoomba rushwa kwa watumishi wa Serikali, huku nikimtaja kwa jina Mbunge wa Bahi, Omary Badwel kuwa ni miongoni mwao," alisema Kafulila ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo.

"Nilijitoa mhanga kwa kutaja majina ya wabunge wanaoomba rushwa kwa watumishi wa Serikali, lakini hatua hazikuchukuliwa, sasa leo Takukuru wamemtia mbaroni mmoja wao, bado hamuamini," alisema Kafulila.

"Sasa naomba niweke wazi kwamba kama Spika hataivunja kamati hii na kuunda nyingine nitajiondoa kwenye kamati kwa sababu itakuwa imepoteza imani kwa wananchi," alisema Kafulila.

TAMKO LA NDUGU DAVID KAFULILA KUHUSU MBUNGE WA JIMBO LA BAHI KUKAMATWA NA TAKUKURU KWA RUSHWA.
JUNE 03, 2012

Kwanza niwashukuru ndugu zangu wanahabari kwa kuitikia wito wangu kukubali kuja kunisikiliza. Mtakuwa mmesikia na kusoma kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu taarifa ya aibu inayolikumba Bunge letu tukufu kufuatia taarifa kutoka vyombo vya dola kuwa mbunge mwenzetu kutoka jimbo la Bahi Ndugu Omary Badwel anashikiliwa na vyombo vya dola kwa kosa la jinai na la aibu sana la rushwa.

Ningependa kuwakumbusha wana habari kuwa nimepata kuzungumza Bungeni mwaka jana 2011 kuhusu tabia ovu kwa baadhi ya wabunge kuomba rushwa watumishi wa serikali katika mchakato wa kusimamia serikali. Ilikuwa ni Bunge la mwezi June, tarehe 13, 2011 wakati nikichangia hoja ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano. Hapa nilitoa taarifa iliyowahusu wabunge watatu akiwemo huyu anayeshikiliwa na vyombo vya dola sasa, Ndugu Omary Badwel. Kwakuwa hakuna hatua iliyochukuliwa, leo napenda niweke msimamo wangu wazi katika maeneo yafuatayo;

1. Kwakuwa nilijitahidi sana kwa kila namna kujenga heshima ya kamati hii ya LAAC bila kupewa ushirikiano toka kwa wadau wote, TAMISEMI pamoja na BUNGE, naomba kutamka rasmi kuwa sina imani tena na Kamati hii kwakuwa imepoteza uhalali kuweza kuendelea kuwa kamati ya kusimamia na kudhibiti hesabu za serikali.

2. Kwa kuzingatia hoja hiyo, Ni wajibu wa Spika kutafakari upya kuhusu hadhi ya Kamati hii na kuipanga upya kwa maslahi ya Umma, heshima na hadhi ya Bunge letu.

3. Nikiwa mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Bunge, Na kwakuwa linayo mamlaka ya kumvua ubunge mbunge yeyote kwa azimio la Bunge, nitaiomba Kamati kushughulikia suala hili kibunge na kuhakikisha tunakwenda na azimio katika mkutano ujao wa Bunge kuhakikisha hatua stahiki zinachulikuwa kulinda heshima ya Bunge ili muhusika aendelee kuchukuliwa hatua za kijinai kama raia wa kawaida.

4. Kwakuwa suala hili linahusu heshima na hadhi ya Bunge, Ni muhimu Kamati ya Uongozi kuhakikisha suala hili linakuwa la kwanza katika ratiba za vikao vya mkutano ujao. Napenda kurudia kuwa, nilisema mwanzo na hakuna aliyechukua hatua. Hii ni mara ya mwisho na ninaahidi kutoendelea kushiriki tena vikao vya kamati hii ya aibu kama Mh. Spika hataona busara na umuhimu wa kuipangua kamati hii. Serikali legelege ni matokeo ya Bunge legelege kwakuwa ni kazi ya Bunge kusimamia na kuidhibiti serikali kikatiba. Watendaji wa serikali kujua bei za wabunge ni msiba.

…………………………………………
David Kafulila (MB).
 
Nani anayo orodha ya wabunge wengine ambao Kafulila anasema alishawahi kuwataja tuwaanike hapa!!
 
Aluta Continua.
 
Mbona mimi nasikia kuwa wbaunge wote wanaokaa kwenye hizi kamati ni wala rushwa na huwa wanasumbua sana Menejimenti za mashirika na taasisi nyingine za serikali wakienda huko kiukaguzi maana ni kama omba omba wakifika huko! duh aibu!
 
Si kweli kuwa ni Rais alwatimua mawaziri wazembe na kuvunja baraza la mawaziri ... Ni Bunge Rais mwnyewe hakuwa na uwezo huo ... too Feeble for that!! Si kweli kuwa serekali ya Tanzania kwa sasa inaweza kufanya jambo lolote la maana ... labda hiki kinachojitokeza sasa ... Ni Mwanaga na njia..!!

Naanza kuona, kumbe kwa namna fulani bunge linaweza kuziba ombwe la uongozi wa taifa hili !!!

Hapa naona Bunge linaweza kufanya episode nyingine letz wait and see ... am watching!!
 
Alikuwa amesahaulika huyu jamaa sasa ameibuka vuuup anatafuta umaarufu tu
 
Kafulila go back to school my friend and peruse on the Priciples of natural justice...You know what I mean.
 
Bunge hili hili ndo matumaini yetu yamelalia hapo lakini ndo Bunge hilo hilo la wala rushwa.
Hivi wananchi hatuna power ya kuvote for NO CONFIDENCE to every leader?
Hapa tulipofikia sasa, RAIS + W/MKUU + MAWAZIRI + WABUNGE = 0
Nani anabisha?

Siungi mkono tamko la Ndugu Kafulila.
Siungi mkono kwa sababu nafahamu ,pamoja na matatizo yetu ya kimfumo na kitaasisi ,bado tunaamini katika utawala wa sheria ambao ni moja ya misingi na viashiria vya dhana ya demokrasia.
Hadi hapo mahakama itakapotamka vinginevyo ,mbunge mtuhumiwa asitendewe kama mtu aliyepatikana na hatia.Kwa sasa bado ni mtuhumiwa tu.
Vinginevyo,kwa siasa zetu za ajabu ,zinazoratibiwa na CCM & washirika wake,tunaweza kupoteza wabunge wetu wengine mahiri kama tukikubaliana na hoja iliyoletwa.Eti mtu avuliwe ubunge kwa kutuhumiwa tu!Hata mahakama hazifikii hukumu bila kuzingatia na kupima ushahidi.
Hata hivyo,ni juu ya mbunge anayetuhumiwa kutafakari na kufuata kile dhamira yake inamuelekeza.
Kama kweli anafahamu ametenda kosa husika,hana sababu yoyote ya kusubiri hukumu ya mahakama kuweza kufanya uamuzi.Alipaswa awe amkwisha kujiuzulu nafasi yake tangu jana alipokamatwa.
Nataka kueleweka wazi kuwa matazamo wa kisheria (legality) usiwekwe katika fungu moja na mtazamo wa kimaadili (morality) ingawa dhana hizi mbili,aghalabu, huhusiana katika mazingira mahususi.Hoja hii inaimarishwa na ukweli kuwa mtuhumiwa anaweza kuwa alitenda kosa kabisa ,dhamira yake ikimshuhudia,lakini hatimaye, mwenendoo & hukumu /ushahidi wa kimahakama ukaaamua kutomtia hatiani.
Ni kwa kuzingatia ukweli huu, bado Ndugu Kafulila anaendelea na majukumu yake ya kibunge,licha ya kuwa na kesi mahakamani na chama chake kuhusiana na uanachama wake.Vinginevyo,asingetoa tamko lake kama mjumbe wa kamati ya bunge, bali kama mwanachi anayewajibika!
 
CCM kwishilia mbali na huu mchezo wa kulindana. Karibu wote wanaomba rushwa kwa namna moja au nyingine
 
Alikuwa amesahaulika huyu jamaa sasa ameibuka vuuup anatafuta umaarufu tu

Tatizo hatupendi ukweli uonekane kama ukweli,hii ni kasumba chafu kwa mtu akifumua uozo fulani kwa maslahi ya nchi kisha watu wengine wakabeza juhudi hizo.Tuna wasiwasi miongoni mwetu kama kweli ni wazalendo wa kweli kwa taifa na watu wake.
 
Leo nina ombi moja kubwa. Hawa watuhumiwa wa kudai na kupokea rushwa tunawasikia na kuwaona wakipelekwa mahakamani, wachache sana wamepatikana na hatia. Hata hivyo hilo siyo tatizo langu, langu ni hili. Je, kuna mtanzania anaeweza kunitajia mtanzania ambaye hapokei wala kutoa rushwa? Ni vyema akatutajia ili tuige maisha ya mtu wa aina hiyo. Naomba sanasana jamani majina ya wasioomba wala kupokea rushwa.
 
Nikumbushe kuwa kwa kuzingataia dhana ya "uhuru wa mahakama", hakuna chombo chochote,ikiwemo bunge, chenye uwezo wala mamlaka ya kujadili suala lililo mahakamani.
Hiki ni kizingiti kikubwa kwa Kafulila wakati huu anapojiandaa kupeleka hoja bungeni ili kutimiza lengo lake la kuona Ndudu Badweli anasimamishwa ubunge.Ingefaa atafakari upya nia yake hiyo.
 
Back
Top Bottom