Tamko la Kafulila kwa Umma (kufuatia mbunge wa Bahi kukamatwa kwa Rushwa)...

Ikumbukwe katika bunge la bajeti la mwaka jana (2011) David Kafulila (Kigoma Kusini,NCCR Mageuzi) aliwataja kwa majina wabunge watatu; Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki-CCM), Zubein Mhita (Kondoa Kaskazini-CCM) na Omar Badwel (Bahi-CCM)kuhusika na kuomba rushwa toka kwa maafisa watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Handeni. Wilaya ambayo kwa miaka mitatu mfululizo ilikuwa imepata hati chafu toka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)!

Toka awaanike wabunge hao watatu, hakuna lolote la msingi la hatua tulisikia limechukuliwa!

Mpaka hivi karibuni ambapo Omar Badwel yule yule aliyetajwa kuomba hongo Handeni kubambwa akiomba hongo ya milioni moja katika wilaya nyingine ya Mkuranga.

Sasa tayari, Omar Badwel amefikishwa mahakamani. Je wale wengine wawili yaani Godfey Zambi na Zubein Mhita nini hatima yao?

Je hatuoni hivi sasa kuna ukweli kwa yale ambayo David Kafulila alisema bungeni?

Lakini hawa ni wachache tu. Je wale wabunge wengine ambao kina January Makamba walisema walipokea rushwa katika mchakato wa kuwapata wabunge wa bunge la Afrika Mashariki nao vipi?
 
yani kamati za bunge zenye kazi ya kusimamia na kufuatilia fedha za serikali nazo zina ufisadi...si mchezo...kweli watu wana njaa hapa bongo
 
Back
Top Bottom