Tamko la ACT-Wazalendo juu ya Ripoti ya CAG mwaka 2013/2014

Tamko la ACT-Wazalendo juu ya Ripoti ya CAG mwaka 2013/2014

mdau kbt

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
401
Reaction score
166
Tamko la Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe kuhusu Ripoti ya CAG mwaka 2013/2014

1) Taarifa nyingine ya CAG imetoka, kwa mujibu wa Katiba ya JMT na kwa mujibu wa sheria za nchi. Taarifa hii imechelewa kutolewa kulingana na mabadiliko ya Ratiba za Bunge ambapo hapo awali taarifa ilikuwa ikitoka mwezi Aprili na kuwezesha kuchangia katika mchakato wa Bajeti ya nchi. Taarifa ya mwaka huu na ile ya mwaka Jana imetoka wakati wa Bunge la Bajeti na hivyo Bajeti ya Serikali haijazingatia hoja za ukaguzi ili kuboresha mfumo wa matumizi ya fedha za umma. Ni vema utaratibu wa zamani wa ripoti kutolewa mwezi Aprili urejewe ili wabunge waweze kutumia ripoti hizo wakati wa kamati katika kujadili makadirio ya Bajeti za Wizara mbalimbali.

2) Taarifa kama miaka iliyopita bado sio nzuri. Mapato mengi ya Serikali bado yanapotea. Uk. 53 wa Taarifa unaonyesha kuwa mizigo inayoingizwa nchini kupita kwenda nchi jirani zinazotumia bandari zetu hubakia nchini na kuingizwa sokoni hivyo kukwepa kodi. Mwaka 2013/2014 mizigo ya transit iliyobaki nchini kiudanganyifu ilikuwa zaidi ya bidhaa 6000 kwa mujibu wa Taarifa ya CAG. Hivyo kodi ya tshs 836 bilioni haikulipwa kwa mizigo hiyo sawa sawa na 10% ya makusanyo yote ya kodi za ndani. Tshs 836 bilioni ilipotea mwaka 2013/14 peke yake. Wakati hili linatokea Serikali ipo ukata mkubwa na kushindwa kuendesha miradi yake mbalimbali. Fedha iliyokwepwa idara ya forodha peke yake inalipa Madeni yote ya wakandarasi wa barabara wanaoidai TANROADS na riba kulimbikizwa kila mwaka. Fedha hii ingelipa Madeni yote ya mfuko wa PSPF wanayoidai Serikali. Fedha hizi zingeweza kulipia miradi 2 mikubwa nchini ya BVR na vitambulisho vya Taifa ambayo inasuasua kutokana na ukata.

Natoa wito kwa CAG kwanza kuweka wazi orodha ya bidhaa hizo zilizobakia nchini na kuingizwa nchini bila kulipa kodi. Vile vile CAG aweke wazi wafanyabiashara wote walioagiza bidhaa hizi na vyombo vya kiuchunguzi vichukue hatua za kuwashtaki wafanya biashara hawa mara moja.

Natoa wito kwa Kamati ya Bunge ya PAC kuwaita mara moja maafisa wa TRA kujieleza mbele ya kamati kuhusu suala hili na kuandaa taarifa maalumu bungeni ili kuanika uoza huu unaopoteza mapato mengi sana ya Serikali.

3) CAG kaonyesha kuwa kuna ubadhirifu mkubwa sana kitengo cha maafa cha ofisi ya Waziri Mkuu ambapo tshs 163 billioni za chakula cha maafa hazikukusanywa katika kipindi cha miaka 5 iliyopita. Huu ni kama mrija wenye wastani wa tshs 32 bilioni kuchotwa kwa kisingizio cha chakula cha maafa kwa wananchi. Kwa malezo ya CAG ni kwamba Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamekula fedha za chakula cha misaada. Maana hakuna uthibitisho wa kuwa mahindi yaliyogawanywa na taarifa kutolewa na Wakala wa Akiba ya Chakula (NFRA). Kitengo cha maafa ofisi ya PM kimekuwa mrija wa wizi wa fedha za umma, wizi ambao umekuwa ukifanyika bila ya kugunduliwa kwa miaka 5 sasa. ACT Wazalendo inaisihi Kamati ya Bunge ya PAC kufanya uchunguzi maalumu kwenye kashfa hii ya tshs 163 bilioni katika Ofisi ya Waziri Mkuu na Wakala wa Hifadhi ya Chakula ( NFRA).

4) ACT Wazalendo inalitaka Bunge kuchukua stahiki dhidi ya Wizara ya Ujenzi kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha kuwa Wizara ilidanganya Bunge katika kupitisha Bajeti ya tshs 252 bilioni ambapo kati yake tshs 87 bilioni ziliibiwa au matumizi yake kutoeleweka.

5) ACT Wazalendo inampongeza CAG kwa kuendelea na zoezi la kisheria la kukagua mahesabu ya vyama vya siasa. Hii inaweka misingi ya uwajibikaji kuanzia kwenye vyama vya siasa, taasisi muhimu sana katika ujenzi wa demokrasia. Vyama vya siasa vichukulie ripoti ya CAG kama changamoto ya kutoa kwanza kibanzi kwenye macho yao ili kuwa na ' moral standing' ya kupambana dhidi ya ubadhirifu wa fedha za umma nchini.

Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo
 
Bavicha leo wapo pamoja na mafisadi dhidi ya Zito,duh kweli adui yao namba moja ni Zito na siop ccm tena
 
Kama kawaida yake kudakia vilivyopikwa na wengine then atumie kutafuta kick kwa Wananchi kwa manufaa yake binafsi na kusema kuwa yeye ndio chanzo cha hayo.
 
Ni vigumu sana ubadhirifu kudhibitiwa hasa ikizingatiwa wawakilishi wa wananchi hawafanyi kazi zao vyema. Unapokuwa na bunge ambalo zaidi ya 70% wanatokea chama tawala inakuwa ngumu sana haya mambo kudhibitiwa kikamilifu.

Nawaasa vyama vya upinzani vipapambane mwaka huu, ili bunge liwe na uwakilishi unaokaribiana wa chama tawala na vyama vya upinzani...
 
Kama kawaida yake kudakia vilivyopikwa na wengine then atumie kutafuta kick kwa Wananchi kwa manufaa yake binafsi na kusema kuwa yeye ndio chanzo cha hayo.

Mkuu supreme leader yeye ndio amewezesha ripoti hii kwa nguvu zake binafsi akiwa nje ya Bunge. Na hii ripoti inaonyesha ni jinsi gani kijana ana uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi peke yake. Tumpe sifa zake SWAHIBA kipenzi wa ccm
 
Uchambuzi makini wenye mapendekezo yakinifu ya utatuzi wa shida iliyopo kwenye serikali ya waovu. Na haya ndio masuala ya kujadili ili tuondokane na umasikini lakini pia kutengeneza uadilifu serikalini. Ukiwa na viongozi wa aina hii wenye kujadili issues ni afya rutubishi kwa taifa.
 
Well done Zitto. Sio lazima uwepo bungeni ndio utumikie watu. Wewe ni Frontliner wa muda wote katika kulinda mali za umma.

Go Zitto!
 
Kiongozi anapaswa kuwa hivi sio kulopoka hovyo bila mpangilio, nchi imejaa uchafu konazote, bila uzalendo wa kweli bado tunawakati mgum
 
Uchambuzi makini wenye mapendekezo yakinifu ya utatuzi wa shida iliyopo kwenye serikali ya waovu. Na haya ndio masuala ya kujadili ili tuondokane na umasikini lakini pia kutengeneza uadilifu serikalini. Ukiwa na viongozi wa aina hii wenye kujadili issues ni afya rutubishi kwa taifa.
Ajabu mtu anakurupuka anakuja na chukizake kwenye vitu muhim, kiukweli nchi inahitaji watu makin tofauti na hapo tutaendelea kulialiatu
 
Watu tuache chuki . kama wewe unaona maoni yake sio mazuri au yana mapungufu tuelimishe. Unapo mtukana sisi ambaye hakuna chuki nae tunakuona kama mpuuzi tu.
 
Watu tuache chuki . kama wewe unaona maoni yake sio mazuri au yana mapungufu tuelimishe. Unapo mtukana sisi ambaye hakuna chuki nae tunakuona kama mpuuzi tu.

Swadaktaa mkuu...unakuta mtu anaamua tu kucomment pasi na kuisoma taarifa yenyewe....
 
Anapotokea Zitto tu Chadema lazima wawe upande wa ccm no matter what? wewe Zitto analeta maswala ya msingi wewe unaingiza chuki alizokupandikiza Mbowe zitasaidia nini? Watanzania tubadilike?

Hiyo taarifa awe ameitoa yeye binafsi ni sawa koz kama mwananchi amewajibika,akiwa ameitoa kama kiongozi wa chama ni sawa koz chama kwa mujibu wa katiba kimempa mamlaka hayo kiongozi wa chama,lakini hata akiwa amelitoa pamoja na viongozi wa ACT kiujumla ni sawa vilevile,unaacha kujadili hoja za msingi alizoziweka hapo unaleta chuki,Nani asiyejua kuwa katika historia ya nchi yetu kamati ya PAC ilionekana kuwa na Meno japo hata kama ni kidogo only under ZZK? angalia sasa hivi yale aliyoyaacha yote nayo yamesimama hatusikii chochote bado watu kama nyie mnajifanya hamtambui aliachokifanya.

Imefika wakati Mkubali ZZK ni mpambanaji na chuki zenu kwake hazina maana wala hazitusaidii watanzania.Ripoti ya CAG imetoka hakuna hata Boya mmoja wa chadema anayejaribu hata kui-analyse na kuibuka na tamko lolote as if iko poa,mmekalia tu ooh Nyalandu anapiga picha na mademu inatusaidia nini sisi? Zitto pambana bro iko siku watakuelewa japo najua hata sasa wanakuelewa ila wanaona aibu kukukubali.
 
Ile ni ripoti ya CAG haya ni maelezo na mapendekezo ya chama chake yanayotokana na taarifa ile. Sasa sijui hapo unafiki unaingiaje!!!. Hata prof Lipumba huwa ana utaratibu wa kuita press ikiwa kuna jambo kubwa limetokea na linagusa maslah ya taifa.....kunya anye kuku akifanya bata hivyo kahara.....
 
Hakika taifa hili kama hata 40% tu ta wananchi ni kama wanachadema wanaochangia humu hakika tutabaki kuwa wa mwisho forever na tutabaki kuwa watu wa kulialia na hakuna ukombozi wa kweli utakaotokea zaidi ya CCM kuendelea kututawala milele,kuna haja gani ya kumtukana Zitto katika alichokiandika hapo? hakina maana? ni bora uache upite wenye kukiona cha maana wajadili.
 
Hakika taifa hili kama hata 40% tu ta wananchi ni kama wanachadema wanaochangia humu hakika tutabaki kuwa wa mwisho forever na tutabaki kuwa watu wa kulialia na hakuna ukombozi wa kweli utakaotokea zaidi ya CCM kuendelea kututawala milele,kuna haja gani ya kumtukana Zitto katika alichokiandika hapo? hakina maana? ni bora uache upite wenye kukiona cha maana wajadili.

Shida hawapo tayari kujadili masuala muhimu kwa taifa ila wapo tayari kujadili watu hasa wale wasiowapenda....kwa namna hii bila kuipa akili uhuru wa kufikiria na kufanya maamuzi chanya ni kweli tuna safari ndefu katika kuuondoa umasikini.
 
Back
Top Bottom