Tamko dhidi ya Ramli ni unafiki mkubwa wa Serikali

Tamko dhidi ya Ramli ni unafiki mkubwa wa Serikali

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,351
attachment.php

Nimeachwa kidogo na muda na matukio.

Majuzi Serikali sikivu kupitia waziri mmoja ilitangaza kupiga marufuku ramli za wanaoitwa Waganga wa Kienyeji kwa sababu kuwa mauwaji ya maalbino yanachangiwa na wao.

Nikaona walakini mara tatu kwenye hili tamko.

1. Huku ni kunyima haki ya msingi ya kuchagua aina ya matibabu anayotaka mja. Ramli ni sehemu ya mchakato wa tiba ya Kiafrika na wakati fulani hatuwezi kuanza tiba pasi na kupiga ramli ili tujue tatizo.

2. Unafiki ni mwingi sana kwa kuwa tangu tatizo la mauwaji ya albino yaanze sijasikia mwanasiasa au mfanyabiashara mkubwa akishikiliwa kwa tuhuma hizi zaidi ya kukamata wahusika wadogo. Hatua hii naiona kama kuwatoa sadaka waganga wa kienyeji na wateja wao ili kujisafisha.

3. Unafiki ni mwingi zaidi pale ambapo tunakuja kugundua kuwa wapiga ramli kwa nia mbaya ni wanasiasa ili waendelee kubaki kwenye nyadhifa zao. Tamko lile ni kama kukata tawi walilokalia (si mpaka lifanyiwe kazi?)

4. Ramli za waganga zinakemewa huku ramli zingine zinazofanywa makanisani zikiachwa bila kushughulikiwa huku tukijua fika kuwa ni utapeli au nguvu za giza. Makanisani watu wanatoa mapepo ya kansa, sukari, umasikini na wakati fulani kutibia walemavu kwa jina la (...)!
 

Attachments

  • sangoma.jpg
    sangoma.jpg
    23.2 KB · Views: 656
Kupiga ramli kwa waganga wa kienyeji ni kuchawia, njia hizo ovu hazifai kuendekezwa kwenye jamii ya kitanzania ili kupunguza kasi ya mauaji kwa njia za kichawi.
 
Na hakuna atayeweza kuzuia ramli isipigwe. Ni sayansi iliyodumu kwa karne nyingi
 
Kupiga ramli kwa waganga wa kienyeji ni kuchawia, njia hizo ovu hazifai kuendekezwa kwenye jamii ya kitanzania ili kupunguza kasi ya mauaji kwa njia za kichawi.

Hata kuponya watu kwa jina la mzungu fulani aliyeishi zamani ni kuchawia pia. Wewe ni nani hata uweke viwango vya wema na ubaya katika tiba?
 
Na hakuna atayeweza kuzuia ramli isipigwe. Ni sayansi iliyodumu kwa karne nyingi

Tumeharibiwa na dini fulani za kipuuzi ambazo zina maovu makubwa ndani yao! Hawaoni shida watu wakifanya dhambi nyingine lakini wanakemea sana vitu vyenye muelekeo wa kiimani.

Kuna jambo tunalikosa hapa!
 
Back
Top Bottom