Tamka neno lolote la faraja kwa walimu

Tamka neno lolote la faraja kwa walimu

Wakuu
Kama uzi unavojieleza naomba tutamke neno lolote la faraja kwa walimu wetu yaani kuanzia wale wa chekechea, shule ya msingi, sekondari, vyuo vya kati, vyuo vikuu maana wote hao ni walimu tu.
Ili watufundishie watoto wetu kwa moyo mmoja
Walimu mtulie kama maji mtungini,
Kazi wanayoifanya ni kubwa, ni kazi ambayo hata Yesu Kristo aliifanya, na hata hao wanaowadharau na kuwadhihaki wamejifunzia kusoma na kuandika kupitia walimu, leo hii tunaukanyaga udongo ambao ndiyo tuliumbwa kutokana nao, kamwe hakuna anayeona thamani yake isipokuwa pale akiwa na shida nao. Walimu jipeni moyo ipo siku furaha yenu itarejea.
 
Mwenye Enzi Mungu awape amani ndani yenu na aweke utisho wa moto Serikalini ili iogope na kuwapa haki yenu walahi [emoji2972]
 
Natamani sana nipate mke mwalimu ni wavumilifu sana na hawana tamaa
 
Wakuu
Kama uzi unavojieleza naomba tutamke neno lolote la faraja kwa walimu wetu yaani kuanzia wale wa chekechea, shule ya msingi, sekondari, vyuo vya kati, vyuo vikuu maana wote hao ni walimu tu.
Ili watufundishie watoto wetu kwa moyo mmoja
Walimu mtulie kama maji mtungini,
Halafu kuna uzi humu mtu kaandika UKIMUONA MWALIMU ANAKUNYWA BIA PIGA MAWE.. ..hii chuki imetoka wapi

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom