TAMISEMI yahalallisha Rushwa Mabaraza ya Kata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAMISEMI yahalallisha Rushwa Mabaraza ya Kata

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by akajasembamba, Jan 2, 2011.

 1. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Rushwa husababishwa na mambo mengi, ila KIPATO KIDOGO ni chanzo kimojawapo kikubwa.Watumishi wa Mabaraza ya Kata (Ward Tribunals) hawana kipato kabisa na wanategemea Rushwa! Watanzania wengine wanaweza wasielewe uzito au umuhimu wa Mabaraza ya Kata na ya Vijiji kwa kuwa wapo mijini, lakini kwa walio vijijini wanaguswa zaidi na Mabaraza haya, maeneo mengi ya vijijini hakuna hata Mahakama za Mwanzo karibu achilia mbali mahakama za wilaya kesi zao hupelekwa ktk Mabaraza haya. Mabaraza haya si mageni na yameanzishwa siku nyingi miaka 26 iliyopita, Sheria husika ya Mabaraza ya Kata, Ward Tribunals Act No.07/1985 ilipitishwa na Rais wa kwanza Mwalimu Nyerere, na imeendelea kuwepo hadi leo, ila yamepata umaarufu zaidi baada ya Sheria ya Ardhi Na.04/1999 ilipoyapa mamlaka pekee ya kusikiliza kesi za madai ya Ardhi.Sheria hiyo inaweka wazi kifungu cha 6(3) kwamba Katibu(Secretary) wa Baraza ni lazima apewe ajira ya kudumu katika Halmashauri ya Wilaya husika, lakini maajabu ya firauni hakuna Makatibu walioajiriwa na hakuna anayelipwa mshahara. Pia kifungu cha 27 kinasema kwamba wajumbe wa Baraza walipwe Sitting Allowance, lakini hawalipwi, cha kutia kichefu chefu Wajumbe hao wanaenda kazini kila mara na wakati hawalipwi posho wala mishahara! Wanategemea rushwa na kutoza faini ambazo hazijaanishwa katika sheria kubwa kuliko hata Mahakama za Wilaya. Wakurugenzi wa Halmashauri hutoa majibu kwamba hawana bajeti ya kuhudumia Mabaraza ya Kata wala kuajiri Makatibu, hii ni sanaa kwa kuwa Sheria imepitishwa na Bunge na Rais ameridhia, iweje Bajeti isiwepo ya kuajiri walau Katibu mmoja, pia Bajeti za sitting allowance za Madiwani na Watumishi wengine zinatoka wapi! Mabaraza haya hayana usimamizi na yamegeuzwa Migodi ya Rushwa na kunyanyasa wananchi, na hakuna anayejali kwa kuwa wanaoenda Mabaraza ya Kata ni masikini. Sheria husika inataja Waziri wa TAMISEMI kuwa muhusika mkuu wa Mabaraza haya, lakini hatujui kama ana habari nayo
   
Loading...