Kutokana na uteuzi uliofanywa na Mhe. Rais naona kama TAMISEMI itakuja kusimama kwa muda bila kupiga hatua yeyote. Serikali za Mitaa ina vijana wasomi tena digrii ya pili na kuendelea ambao wangeteuliwa kuachana na Wakurugenzi waliaoachwa. Nimeona kwenye Jamii Forums kuwa mmojawapo wa Mkurugenzi aliyeteuliwa alikuwa Meneja wa Hoteli. Sijaamini, lakini kama ni kweli Mhe.Rais alishauriwa vibaya. Kazi ya ushauri ilikuwa itoke kwa Mhe.Waziri aliye na dhamana na TAMISEMI. Kuna vijana wazuri sana kwenye Local Government mfano:- Maafisa utumishi, Maendeleoya Jamii, Mafisa Elimu, Waweka Hazina, Wahandisi wa Ujenzi na Maji, Maafisa Ardhi, Maafisa Misitu, Waganga wa Wilaya n.k.wako wengi na uteuzi ungewagusa hawa. Kumteua mtu ambaye hana uelewa na Local Government italeta shida kubwa.
Huu ni ushauri tu lakini naomba ufanyiwe kazi.
Huu ni ushauri tu lakini naomba ufanyiwe kazi.