alishawahi kusema kuwa akihamia CCM toka upinzani basi lazima awe kalala na mama yake!
KASHAMLALA?
Umenikumbusha story iliyo-hit wakati huu mwana siasa huyu alivyokuwa machachari (by then alikuwa anajoin CUF akitokea CCM), maneno hayo kimsingi hayakuwapendeza wana CCM achilia mbali watu wenye akili zao timamu. Siku alipo achana na siasa za mageuzi (wengi huziita siasa za upinzani) akikiacha chama cha CUF na kurudi nyumbani CCM (nyumba aliyoirushia vijembe kwa lugha isiyofaa) magazeti yali report kwa headings tofauti zikimkejeli kwa reflection ya swali ulilouliza hapo juu. Tunachoweza kujifunza kutokana na kauli zake, ni muhimu kwa wana siasa kupima kauli na maneno kabla hawajayatamka because ni maneno yakishatamkwa hayarudi kinywani tena, na mbaya zaidi yataendelea kuwa hukumu juu yako.
Pili, ukiachilia kuwa kwa siku za karibuni, Urais kama Taasisi, imefanywa rahisi, kiasi kwamba kila mtu anadhani anaweza kuwa mkuu wa Kaya, ni muhimu kuwapa watu nafasi ya ku-excercise demokrasia, sasa kama wana sifa stahiki ni jambo la vikao vya chama husika/au wananchi kuamua kupitia sanduku la kura. TUSIWABEZE, tusiwatukane, tusiwakejeli bali tuwasikilize kupitia mijadala ya wazi, tuwaulize maswali magumu, tupime majibu yao kama yana kidhi haja, tuwajadili kisha tufanye maamuzi sahihi, hapo naamini tutapata kiongozi tumtakaye.
Tatu, kuongoza nchi maskini ni mzigo kwa kiongozi mtendaji lakini siku za hivi karibuni imekuwa tofauti, hata media zina report, bwana so and so 'KAULA', bibi so and so 'KAULA' wakimaanisha kachaguliwa au kuteuliwa kuwatumikia Watanzania katika wadhifa fulani. Kiongozi unaula? kweli? hapo kuna kiongozi au mtawala? tena mtawala asiyejali maslahi ya watu achilia mbali nchi yake.