Tambwe Hizza ndani ya 'Tuongee asubuhi' - Star tv... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tambwe Hizza ndani ya 'Tuongee asubuhi' - Star tv...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Dec 16, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Yule aliyekuwa mkurugenzi wa propaganda wa chama cha CCM ndugu Tambwe Hizza anaongea kupitia Tuongee Asubuhi muda huu...Jamaa anadai CUF wanajifunza siasa na wala sio chama cha siasa anamsifu Hamad Rashidi kwa kuchukua uamuzi wa kugombea ukatibu mkuu,anadai CCM hakuna mgogoro na wala hakujawai kuwa na mgogoro na wala hakina agenda ya siri ya kuharibu vyama vingine kama watu wanavyosema,anadai tatizo vyama vya upinzani vinaendeshwa kindugu na kibinafsi,anamsifu raisi kwa kutoa uhuru watu kusema na wanautumia vibaya na raisi kakaa kimya,anasema ana mashaka na wanaharakati wa Tanzania ati wamejitengenezea ajira tu(na hii imekuwa ni kauli ya karibu wanachama na viongozi wa CCM) anasema kama wangekuwa ni wanaharakati wa kweli iliwapasa wawe na kazi zao nyingine na uhanaharakati wawe wanafanya kama part-time(mawazo ya kijinga namna gani haya)...anasema CCM ni chama makini Tanzania kwa kizazi hiki!! My take!! Jamaa ni mnafiki sana yaani ukimsikiliza unaweza ukapandwa na hasira sana.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa sasa ana cheo gani ndani ya CCM? Au amebaki kuwa mkereketwa tu!!
   
 3. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ...anasema kama kiongozi ni mbovu (asiondolewe) asubiriwe mpaka mda wake (wa uongozi) uishe ili aondolewe kwa mujibu wa katiba!
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Cheo chake ni mgombea wa kudumu wa ubunge katika jimbo la Temeke kupitia chama chochote cha siasa. Ukumbuke alianza kugombea Temeke kupitia NCCR mwaka 1995, akaja kupitia CUF 2000 na 2005, akaja kupitia CCM 2010 alipochujwa mapema ndani ya CCM
   
 5. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ...hana imani na wanaojiita "wanaharakati" coz wao wenyewe hawana demokrasia kwenyewe taasisi zao (wanahodhi kila kila kitu cha taasisi).
   
 6. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  anajibu hoja... ccm hakuna mgogoro, makamba hakutimuliwa, alijiuzulu na sekretary yake yote! baada asilimia za kura za uchaguzi mkuu 2010 kushuka.
   
 7. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  mwakilishi cuf anasema... lipumba si mwenykiti wa kwanza wa cuf, yeye ni mwenyekiti wa 3 wa chama baada ya mzee mapalala na mwingine sijampata vizuri jina lake.
  pia anadai, kwa sasa ndani ya cuf, hakuna mtu mwenye sifa kama lipumba ambaye anaweza akapewa kiti hicho... mwenyekiti ni nembo ya chama.
   
 8. M

  MCHUMIA NCHI Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo jamaa ni li KILAZA ajabu,lilishawahi sema hakuna umuhimu wa kubadili katiba,mtangazaji wa Mlimani tv akaliuza kwanini?Likajibu''Basi tu'!'
   
 9. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  huyo jamaa huwa nikimuona tu kwenye tv napata kichefuchefu na huwa nimeiaribu siku yangu kwa siku hiyo
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mnh kweli ulipoteza muda wako kumsikiliza Tambwe Hizza
   
 11. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Hiza bonge la mnafiki! Anasahau alivyokuwa anaitukana CCM wakati Kikwete anagombea urais? Alimwita JK ana sura ya mama. Isitoshe kwenye kampeni za kugombea ubunge huko Temeke wakatai CCM walipomsimamisha Cisco alimwita kwamba yeye ni burushi babake ni Giriki. Mamake Cisca alizimia.
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuhusu hili la uana harakati liko wazi kabisa, wana harakati wetu wamekosa umakini ni wako kwa ajili ya posho na kujitafutia umaarufu si watu makini hata chembe, na isitoshe hata CDM sio chama cha siasa, ni wanaharakati wa siasa

   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Anatumia haki yake ya msingi ya uhuru wa kuongea na kuishabikia CCM, na wewe fanya hivyo kwa Chama chako. Ukipandisha hasira haikusaidii na wala humsaidii mtu yeyote.
   
 14. M

  MCHUMIA NCHI Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Masuala ya Chadema yanaingiaje humu?Mi shoga mingine bana!
   
 15. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa aliogopa umande sasa unatarajia nini hapo upstairs kama sio garasha tu? Sijui magamba walimpokea kwa vigezo gani mpaka kumpa uongozi au nao ni walewale..
   
 16. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kweli wewe jinias.. tuongezee lingine tuburudike
   
 17. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Tambwe hiza asituhangaishe yeye ni 'opportunist' na watu wa namna hii kwa ndani huwa ni 'bendera fuata upepo' na watu wa kaliba hii hawawezi kuleta maendeleo maana hudandia hoja tu kuliko kuwa chanzo cha hoja. Kwa idadi ya wanachama ni kweli CCM ni chama imara, lakini kwa muundo wa maendeleo ya wananchi na nguvu ya hoja, sioni kama ni chama chenye nguvu kuliko vingine. Wakati mwingine hata Mtikira na DP yake walikuwa na hoja kubwa kuliko CCM.
   
 18. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Maoni yako yanaheshimiwa lakini hayana 'mshiko' maana ni kusema watz waliofuatilia hoja za CDM na kuwapatia kura zile tusizozijua kwa uhakika idadi yake (ila jaji Lewis Makame) nao ni wanaharakati? Mi naona wanaharakati wamesaidia sana TZ yetu kuwa na wanasiasa wanaoweza kuwaza kabla ya kutenda kuliko ilivyo kuwa wakati wa 'zidumu fikra...'
   
 19. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Sawa CCM hakuna mgogoro na kujiuzulu si dalili ya migogoro, akamuulize mzee Lowasa maana wanongea ndo atajua anachosema, maana na yeye alijiuzuru si kwa mgogoro labda!!
   
 20. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Naona jamaa kapata jukwaa kidogo tu kalitumia kujipendekeza kwa Dr Dr Dr Dr Dr Kikwete. Hapo ndio siasa za CCM zinapochosha, ina maana bila kujipendekeza haupati madaraka? Mbona Mzee wa Monduli ameamua kuyatafuta kwa uwezo binafsi baada ya juhudi za kujipendekeza kuwa hawajakutana barabarani kugonga ukuta. Hivyo hata Tambwe inabidi atambue kuwa wakati wa kujipigania binafsi umefika sio kutegemea mbeleko ambayo sasa anabebewa Nape. Huo uhuru wa watu kusema unaosema kauleta JK ina maana katoka nao kwao Msoga au uko kwenye katiba?
   
Loading...