Tambwe amponda Hamad Rashid kung'ang'ania madaraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tambwe amponda Hamad Rashid kung'ang'ania madaraka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Manyanza, Feb 12, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  MKUU wa Kitengo cha Propaganda wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tambwe Hiza, amemshangaa aliyewahi kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kwa kung’ang’ania madaraka.
  Tambwe alitoa kauli hiyo jana dhidi ya Hamad ambaye ni Mbunge wa Wawi (CUF) wakati akihojiwa kupitia kipindi cha Kurunzi kinachorushwa hewani na Televisheni ya Mlimani.
  Alisema anamshangaa mbunge huyo pia anashangaa kitendo cha kusakamwa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuingiliwa katika maamuzi yao licha ya chama hicho kustahili kuwa viongozi wa kambi ya upinzani bungeni na kufanya maamuzi yao.
  Alisema Hamad amekuwa kiongozi wa kambi hiyo kwa kipindi kirefu hivyo alitakiwa kuwaachia nafasi hiyo CHADEMA.
  “Jamani mimi nashangaa hawa watu wanasema CCM inang’ang’ania madaraka lakini pia wanatakiwa kukumbuka kwamba hata wao wanapenda kuwa viongozi hebu ona kulikuwa na haja gani ya kuwaonea CHADEMA.
  Kama hoja ni kuwa na nafasi ya kuwasilisha hoja hata kama hujawa kiongozi wa upinzani unaweza kuiwasilisha kwa njia ya barua kwa Spika au vinginevyo,” alisema Tambwe.
  Alisema anawashangaa na watu ambao wanadai CCM imepoteza umaarufu wake jambo ambalo si kweli kwa kuwa ndicho chama ambacho kimeongoza katika chaguzi zote na hata kumwezesha Rais Jakaya Kikwete kushinda katika uchaguzi.
   
 2. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Aliongea vizuri sana lakini akaja akaharibu hapo kwenye blue, nadhani alishituka maana angeipamba CDM mwanzo mwisho asingepata posho lake siku hiyo.... si unajua watu wa propaganda? hata kwenye ukweli lazima aweke fitina
   
Loading...