Tambiko la Kwamsisi kupisha barabara na fidia ya Tsh 21,000,000

1 Corinthians 10:20-22

20 No, but the sacrifices of pagans are offered to demons, not to God, and I do not want you to be participants with demons. 21 You cannot drink the cup of the Lord and the cup of demons too; you cannot have a part in both the Lord’s table and the table of demons. 22 Are we trying to arouse the Lord’s jealousy? Are we stronger than he?
--
20 La, sivyo. Lakini sadaka inayotolewa kwa sanamu inatolewa kwa mashetani, na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi muwe na ushirika na mashetani. 21 Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na kunywa katika kikombe cha mashetani pia. Hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya mashe tani. 22 Je, tunataka kujaribu kumfanya Bwana awe na wivu? Je, sisi tuna nguvu kuliko yeye?​
Hata yesu alitolewa kafara, mtoto pekee wa abraham alitaka kutolewa kafara,, kuna binti wa mfalme wa israel alutolewa kafara, vichanga vilitolewa kafara,
Kafara zipo
 
Wameshaambiwa wasiguse hata mti, watoe pesa ya tambiko kwanza.
Kuna watu wanasema sijui apelekwe nani akaombe! Kumbukeni hapo ni Mambo live hapahitaji maigizo wala watu wa michongo.
Ni kweli hii michongo ya wazungu iliwahi washinda wazungu wa kijerumani kule njombe kwenye mstu wa nyumba nitu miaka ya 1800
 
Upanuzi wa barabara ya Tanga ni ule mkakati wa kati wa kuziunganisha barabara za Arika mashariki na ule mkakati wa juu wa kuwa na barabara inayotoka Cairo Misri mpaka Cape town J'burg.. Ni mradi ndani ya mradi wa mabilion ya Dola
Mkakati huo kwenye ujenzi wake unajumuisha barabara ya lami ya kiwango cha kimataifa, njia za waenda kwa miguu, alama za barabarani, ma culverts, madaraja ya juu na chini, kingo mitaro, taa za barabarani nknk
Barabara inapita kwenye mapori, misitu, mashamba makubwa na madogo, mito, vijiji, miji, majiji, kwenye makazi ya watu shughuli za kijamii nknk., Kwahiyo kwa namna moja ama nyingine fidia haiepukiki kwenye mazao, mashamba, makazi na uwekezaji mwingine.. Tena ni fidia kwa viwango vile vile vya kimataifa..

Afrika bado ni bara ambalo lina maeneo vigoli ama bikira kwa maana ya kwamba hayajaathiriwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia ya kisasa ama hayajaguswa kabisa yapo bado kwenye uasili wake.. Afrika bado ina maeneo yanayofaa kuingizwa kwenye mpango mkakati wa urithi wa dunia..
Afrika bado ina maeneo mengi yenye vilinge, maeneo ya ibada za kimila, matambiko na mizimu.. Haya maeneo yote yanapaswa kuheshimiwa na kupewa hadhi yake yanayostahili...KWAMSISI Handeni ni mojawapo ya maeneo hayo
Kuna fidia imeandaliwa na wazee wa Kwamsisi kwa ajii ya kufanya tambiko eneo hilo ambalo barabara inapaswa kupita.. Wametoa makisio ya milion 21 za kitanzania kwa ajili ya shughuli yote yaani
. Kufanya tambiko la mwanzo la kuondoa kila kitu
. kufanya tambiko wakati kazi inaendelea
. Kufanya tambiko la kufunga na kushukuru barabara ikishapita
Hii si kazi ndogo asilani na si kazi inayojumuisha pesa tuu
Cha aibu na pengine cha kushangaza ni mkuu wa wilaya wa Handeni kufika Kwamsisi na timu yake na kuitisha mkutano wa hadhara kwa ajili ya KUOMBA PUNGUZO kwenye milion 21 akisema ni nyingi sana kwa shughuli ndogo tu ya tambiko
Kwa ukubwa wa mradi kuomba punguzo kwa niaba ya mkandarasi kunazua maswali mengi bila majibu.. Lakini je wale wazee wa Kwamsisi wakikataa pesa na kuhitaji vifaa vya kazi husika serikali itaweza?View attachment 2008673
Ile miti inayogoma kutoka ni kwasababu tambiko halijafanyika,daaaaah
 
Wameshaambiwa wasiguse hata mti, watoe pesa ya tambiko kwanza.
Kuna watu wanasema sijui apelekwe nani akaombe! Kumbukeni hapo ni Mambo live hapahitaji maigizo wala watu wa michongo.
Hakuna siasa hapo
 
Back
Top Bottom