Tambiko la Kwamsisi kupisha barabara na fidia ya Tsh 21,000,000

Halafu watu wa huko wengi ni wa dini ya hakhi..nikisema wavaa kobazi ni wachawi na walonzi wa kutupa watu hawaamini..sasa nadhani mnashuhudia wenyewe njinsi hali halisi ilivyo kupitia waumini wa kwamsisi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ujinga ww
Uislamu hauruhusu uchawi kabisaaa ayo ni mambo ya watu wnywe kwaio usiyaingize kwny dini kabisaaa
 
Nadhani Mwamposa na Manabii wenzie waisaidie Serikali kwenda kuifukuzia mbali hiyo mizimu, hii ni fursa nzuri kwao kutangaza biashara yao ya Maji na Mafuta ya Upako..
Wataishia kuwala pesa wasojua kitu mna ni waongo
 
Nilisema Mimi
IMG-20211215-WA0026.jpg
 
Upanuzi wa barabara ya Tanga ni ule mkakati wa kati wa kuziunganisha barabara za Arika mashariki na ule mkakati wa juu wa kuwa na barabara inayotoka Cairo Misri mpaka Cape town J'burg.. Ni mradi ndani ya mradi wa mabilion ya Dola.

Mkakati huo kwenye ujenzi wake unajumuisha barabara ya lami ya kiwango cha kimataifa, njia za waenda kwa miguu, alama za barabarani, ma culverts, madaraja ya juu na chini, kingo mitaro, taa za barabarani nknk

Barabara inapita kwenye mapori, misitu, mashamba makubwa na madogo, mito, vijiji, miji, majiji, kwenye makazi ya watu shughuli za kijamii nknk., Kwahiyo kwa namna moja ama nyingine fidia haiepukiki kwenye mazao, mashamba, makazi na uwekezaji mwingine.. Tena ni fidia kwa viwango vile vile vya kimataifa.

Afrika bado ni bara ambalo lina maeneo vigoli ama bikira kwa maana ya kwamba hayajaathiriwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia ya kisasa ama hayajaguswa kabisa yapo bado kwenye uasili wake.. Afrika bado ina maeneo yanayofaa kuingizwa kwenye mpango mkakati wa urithi wa dunia.

Afrika bado ina maeneo mengi yenye vilinge, maeneo ya ibada za kimila, matambiko na mizimu.. Haya maeneo yote yanapaswa kuheshimiwa na kupewa hadhi yake yanayostahili...KWAMSISI Handeni ni mojawapo ya maeneo hayo

Kuna fidia imeandaliwa na wazee wa Kwamsisi kwa ajii ya kufanya tambiko eneo hilo ambalo barabara inapaswa kupita.. Wametoa makisio ya milion 21 za kitanzania kwa ajili ya shughuli yote yaani

. Kufanya tambiko la mwanzo la kuondoa kila kitu
. kufanya tambiko wakati kazi inaendelea
. Kufanya tambiko la kufunga na kushukuru barabara ikishapita

Hii si kazi ndogo asilani na si kazi inayojumuisha pesa tuu

Cha aibu na pengine cha kushangaza ni mkuu wa wilaya wa Handeni kufika Kwamsisi na timu yake na kuitisha mkutano wa hadhara kwa ajili ya KUOMBA PUNGUZO kwenye milion 21 akisema ni nyingi sana kwa shughuli ndogo tu ya tambiko

Kwa ukubwa wa mradi kuomba punguzo kwa niaba ya mkandarasi kunazua maswali mengi bila majibu. Lakini je wale wazee wa Kwamsisi wakikataa pesa na kuhitaji vifaa vya kazi husika serikali itaweza?

View attachment 2008673
Hivi Uchawi Upo?
 
Ameleta dharau sana. Mambo ya mila ni makubwa, tena jambo lenyewe ni kwa msisi, wazee ilipaswa wakaze uzi na wajitoe kwenye uhusika wa lolote baya litakalotokea.
 
Haaa
Wapo manabii wa ukweli ondoa shaka . Kikubwa ni kuwapatia nafasi waende wakiweka kambi hapo mbona kinaeleweka . Serikali wanaamini waganga na wachawi lakini wachungaji waliopakwa mafuta na Bwana hawapewi nafasi
Ni kweli kabisa Mkuu.Hata Nabii Eliya alikuwa mmoja tu lkn aliwapiga bao Manabii zaidi ya mia nne wa mungu baali (mungu wa uongo).
 
waliostraabika kitambo, kwamba wakitaka kujenga kinu cha Nuclear wanatafuta wazee wa hiyo sehemu kwanza.
Ustaarabu ni irabu pana sana.. Hakuna kabila duniani isiyofanya mila au tambiko hasa kwenye ujenzi na biashara
 
Ustaarabu ni irabu pana sana.. Hakuna kabila duniani isiyofanya mila au tambiko hasa kwenye ujenzi na biashara
Huko kuna kuabudu mapepo bila kujua. Kufanikiwa kunaweza kuwepo, ila si vyema kuangalia tu mafanikio. Iangaliwe na njia inayotumika kufika kwenye mafanikio.. Eh Mungu tuongoze kwenye njia zilizo sahihi.
 
Back
Top Bottom