Tamasha la Pasaka lazua kizaazaa cha kisiasa

Tamasha la Pasaka lazua kizaazaa cha kisiasa

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
552
*Jana wakati wa kusherehekea sikukuu ya Pasaka kulikuwa na Tamasha kubwa la muziki wa Injili katika uwanja wa Taifa jijini Dar, huku maelfu ya watu mbalimbali wakiongozwa na waziri mkuu Mizengo Pinda walijumuika kuwaona na kuwasikiliza waimbaji maarufu wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi.

*Jambo mojawapo kubwa ambalo limekuwa gumzo mitaani, mitandaoni na kwenye vyombo vya Habari na sasa limeanza kuleta kizaazaa ni Kitendo cha Kushangiliwa sana kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe mara tu alipotambulishwa huku hali ikiwa kinyume kabisa kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda.

*Baadhi ya Watu hususani viongozi waandamizi wa Serikali na makada wa CCM wameshtushwa, wamesononeshwa na wamechukizwa sana na kitendo hicho kwa kudai kuwa kilikuwa kina nia mbaya ya kuidhalilisha serikali na CCM kwa ujumla, na sasa wanajipanga kumpa onyo kali muandaaji wa Tamasha hilo Msama Promotion(Inasemekana huyu jamaa ni kada mzuri wa CCM pia) asiruhusu tena kitendo hicho kujirudia hasa huko mikoani ambako tamasha hilo litaendelea kufanyika ambako pia kuna viongozi wa Serikali(DC, RC, Mawaziri) lakini kuna Wabunge wa CHADEMA kwa kuhakikisha MC hamtambulishi mwanaCHADEMA yoyote katika hadhira hiyo.

Maafisa hao wamekwenda mbali zaidi na kudai kulikuwa na ulazima gani kwa MC kumtambulisha Freeman Mbowe pale uwanjani kama hakuwa mgeni rasmi?

*Wakati huo huo baadhi ya makada wa CCM wameanza kujipanga kuitumia kama mwendelezo wa propaganda ya kutaka kuonyesha kuwa CHADEMA inaungwa mkono sana na jamii ya Kikristo na hivyo kuhalalisha ile dhana ya kusema CHADEMA ni chama cha Kikristo.
 
Waacheni watoto wadogo waje kwangu maana ukombozi unakaribia...

Kila mtu anapenda nguo mpya sasa ya PINDA ndio uliyokuwa nayo na unataka mapya kwa MBOE
 
Kwa hiyo analaumiwa "Msama" kwani ndo aliyewaamuru wananchi wamshangilie Mbowe? Pole sana CCM, mmekosa mwana na Maji ya moto!!!!
Wanasema kulikuwa kuna haja gani ya Lazima kumtambulisha rasmi Freeman Mbowe mbele ya wahudhuriaji wakati hakuwa mgeni rasmi wa Tamasha hilo?
 
Wanasema kulikuwa kuna haja gani ya Lazima kumtambulisha rasmi Freeman Mbowe mbele ya wahudhuriaji wakati hakuwa mgeni rasmi wa Tamasha hilo?
Utaachaje kumtambulisha kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni? Au hujui kuwa na yeye ni kiongozi mkubwa wa nchi?
 
...
*Wakati huo huo baadhi ya makada wa CCM wameanza kujipanga kuitumia kama mwendelezo wa propaganda ya kutaka kuonyesha kuwa CHADEMA inaungwa mkono sana na jamii ya Kikristo na hivyo kuhalalisha ile dhana ya kusema CHADEMA ni chama cha Kikristo.
Kwani Pinda ni muisilamu?
 
Wanasema kulikuwa kuna haja gani ya Lazima kumtambulisha rasmi Freeman Mbowe mbele ya wahudhuriaji wakati hakuwa mgeni rasmi wa Tamasha hilo?

Ni kutafuta mtu wa kumlaumu tu, kwani aliyetambulishwa alikuwa ni Mbowe tu? Mbona kuna watu wengine walitambulishwa? Watachoka sana hawa thithimwewe!!!!
 
Mimi nilikuwepo Uwanjani...kwa hali ile hata ukiwazuia watu wasimshangilie Mbowe kwenye matamasha, watamshangilia mioyoni mwao....
Bahati mbaya sana mimi sikuwepo uwanjani, ila ninataka kujua zaidi kuhusu
1/'Atmosphere' alikuwaje kabla, wakati na baada ya kutambulishwa kwa Mbowe

2/Je Unahisi ni kwanini ulikuwa vile?

3/Nini tafsiri yake kiimani(!?), Kisiasa au kijamii?
 
Pinda amechuja sana. Hii nchi kama ingekuwa inachagua viongozi kwa MERIT Pinda asingestahili hata kuwa Mwenyekiti wa Kijiji.
 
Hakuna jipya chini ya jua! Daudi alipomshinda Goliathi na kumuua, wanawake walimshangilia sana Daudi. Kitendo hicho kilimchukiza mfalme Sauli ambae aligeuka kuwa adui mkubwa wa Daudi huku akitafuta sana kumuua! Mwisho wa siku Mfalme Sauli alikufa na Daudi akawa Mfalme wa Israel kwa kuwa Mungu alimchagua! Mwisho wa siku CCM itakufa CDM itashika ufalme!
 


....tatizo kutatua matatizo ya nayowakabili Watanzania kwa kutumia
video clips mfano elimu, njaa, maradhi nk.....

...WAMESUBIRI AHADI MPAKA WAMECHOKA.....
 
Yamekuwa hayo tena? Yaan viongozi wa chama cha msimu wanakubalika zaid ya wale wa chama cha wanajim-siami ......wassira, Nape na mwigulu bado wanaamin katika unajim?
 
mbowe hakushangiliwa kwasababu ya ukristo wake (kwa sababu hata pinda ni mkristo)
jambo la msingi la kuliangalia ni kwamba hawahwa waliomshangilia pinda ndio wle wale waliomshangilia mbowe, tofauti iliyopo ni ukubwa wa jinsi walivyoshangilia! ntijitahidi nifafanue kwa ufupi
pinda alishangiliwa kama mgeni rasmi, kama kiongozi na kama waziri mkuu wa nnchi..
lakini mbowe alishangiliwa (na watu walewale) kama mpiganaji wao (ndivyo watu wanavyoamini), alishangiliwa kama agent wa mabadiliko ambayo washangiliaji hawa wanaitaka, kwasababu washangiliaji hawa wengi wao ni walala hoi kama akina sisi ambao kwao chama si ishu bali wanachohitaji ni 'change'..
trust me, hata angeenda zittto, lema, slaa, sugu,mdee au hata dogo nasari angeshangiliwa kuliko pinda..
 
Mbowe alienda kuangalia waumini waliompa chama akiendeshe
 
*Jana wakati wa kusherehekea sikukuu ya Pasaka kulikuwa na Tamasha kubwa la muziki wa Injili katika uwanja wa Taifa jijini Dar, huku maelfu ya watu mbalimbali wakiongozwa na waziri mkuu Mizengo Pinda walijumuika kuwaona na kuwasikiliza waimbaji maarufu wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi.

*Jambo mojawapo kubwa ambalo limekuwa gumzo mitaani, mitandaoni na kwenye vyombo vya Habari na sasa limeanza kuleta kizaazaa ni Kitendo cha Kushangiliwa sana kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe mara tu alipotambulishwa huku hali ikiwa kinyume kabisa kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda.

*Baadhi ya Watu hususani viongozi waandamizi wa Serikali na makada wa CCM wameshtushwa, wamesononeshwa na wamechukizwa sana na kitendo hicho kwa kudai kuwa kilikuwa kina nia mbaya ya kuidhalilisha serikali na CCM kwa ujumla, na sasa wanajipanga kumpa onyo kali muandaaji wa Tamasha hilo Msama Promotion(Inasemekana huyu jamaa ni kada mzuri wa CCM pia) asiruhusu tena kitendo hicho kujirudia hasa huko mikoani ambako tamasha hilo litaendelea kufanyika ambako pia kuna viongozi wa Serikali(DC, RC, Mawaziri) lakini kuna Wabunge wa CHADEMA kwa kuhakikisha MC hamtambulishi mwanaCHADEMA yoyote katika hadhira hiyo.

Maafisa hao wamekwenda mbali zaidi na kudai kulikuwa na ulazima gani kwa MC kumtambulisha Freeman Mbowe pale uwanjani kama hakuwa mgeni rasmi?

*Wakati huo huo baadhi ya makada wa CCM wameanza kujipanga kuitumia kama mwendelezo wa propaganda ya kutaka kuonyesha kuwa CHADEMA inaungwa mkono sana na jamii ya Kikristo na hivyo kuhalalisha ile dhana ya kusema CHADEMA ni chama cha Kikristo.
TanganyikaTANU
Nimesema mara nyingi kwamba tunahitaji kuwekeza vyama vyetu ktk mioyo ya watz kuliko kugawa kadi za vyama. Watz wa leo wanaweza kukudanganya kwa mbwembwe nyingi tu za kuhama toka chama hichi na kwenda chama chengine lkn moyo wake bado ukabaki ktk chama cha zamani! Kilichojitokeza kwenye tamasha la pasaka kwa mtazamo yangu ni mapenzi na shauki ya kumuona watu wanayempenda jambo ambalo huwezi kulizuia. Nishawahi kusema kuwa "nguvu au heshima ya mtu katika jamii husika haipati kwa sababu ya kuwa na pesa, au madaraka au cheo, la asha heshima na power ya mtu hutokana na yeye mwenyewe. Mapenzi ya mtu kwa jambo lolote ni hisia zako ambazo huwezi kuzizua hata kwa mtutu wa bunduki. Ndugu wangu watz wanataka mabadiliko.
 
Last edited by a moderator:
Mbowe alienda kuangalia waumini waliompa chama akiendeshe

Malaria Sugu! ile software ya Invisible inayokufatilia hadi chooni haijatambua hii ID! sasa hivi na hii inakula ban!!
Wewe jamaa mbishi aisee siku ile uliyokiri kufungua ID zaidi ya mia na zote zikala ban kwenye thread hiyo hiyo ukafungua ID nne zote zikaunganishwa na ban juu!!!
Kazi ipo na huyu mtu aisee!!
 
CDM na KANISA ni two sides of the same coin!
 
Back
Top Bottom