Tamaduni Music hawajawahi kufanikiwa kwenye chochote kile wanachokianzisha

Mkuu umefafanua vizuri sana .
Kwa upande wangu naona Mentality yao ndo imewanyima fursa nyingi bado wana uzamani akilini mwao.

Mtu kama Nikki mbishi ndo kabisa Ni Maskini jeuri
 
Sio nyota ni vile hataki kujiongeza, yan kwa kifupi hana maarifa
tatizo vinega, hippop culture imewaingia kwenye damu, kila kitu wanawaza harakati

Hip pop culture hata KRC ONE imemshinda usa , mziki ni dynamic unabadilika kila muda, hata hip pop ilipoanza ilikuja kufanya mabadiliko ya dominance ya rock, funk , break dance nk hivyo wajitahidi kubadilika

mwangalie mtu kama kofi olomide ndombolo yake ya kipindi anaanza kuwika na kofi wa sasa wakikutana lazima wagombane

wanamuziki wengi wa kizazi hiki wengi hawajui kuimba, huwezi kufananisha na uwezo walikuwa nao tamaduni , ila wanaangalia nini jamii wanataka kusikia na nini wamechoka kusikia, binadamu hawana shukrani akipata kitu muda si mrefu anakiona hakina maana ,anataka kipya hata kama kibaya roho yake ndio hulizika

hata ivyo ndugu yangu mansu le hana shida ndogondogo fremu nyingi nyumbani kwao pale sinza mugabe zanampa pesa nyingi. fremu moja milion anazo karibu sita , nadhani karidhika
 
Nimekupata kinoma noma...
 
Hili andiko umeandika kisomi sana sajo ., kuna mtu ana master namjua aliwai kuimba daz , anaandika kama wewe , vipi bado upo mbeya? Bode kinyozi wako anakupa hapa sinza

Only strong survive , fitina kwenye mziki ni janbo la kawaida , nikuuliza hakuna mwanamuziki yoyote bado yupo kwenye Game ambaye alikuwa na bifu na luge , fela nk?

je kwa sasa mziki upo monopolize kama zamani?
kuna platform kibao ambazo unaweza kuweka kazi bila bugza yoyote, hata tv ,radio hazibani kama zamani, je tamaduni wametumia hizi fursa?

yote kwa yote nakupa ongela kwa uchambuzi wako, yote ni kweli ..ila kisiwe kigezo sana , kumbuka msemo huu GEMU NI GUMU
 
Tamaduni wabadilike kifikra. Kuendelea kung'ang'ania muziki ambao hauhitajiki sokoni ndo anguko lao. Hata wanamuziki wa Congo baada ya kuona wanapotea wameamua kubadilika.. zamani walikuwa wanatoa nyimbo ndefu za hadi dakika 10 ila siku hizi na wao wanatoa nyimbo za dakika 3 hadi 4. Na yale masebene wamepunguza. Kina Pepe Kale wakifufuka watashangaa sana kuona Werrason katoa wimbo wenye verse ya Hiphop. Wacongo pia walikuwa ni wabishi mno kupiga bila vyombo lakini siku hizi nao kuna matamasha wanapiga bila vyombo ili mradi mkono uende kinywani. Kimsingi muziki una mabadiliko dunia nzima. Tamaduni wao wakubali kubadilika na kuacha UJEURI. Kujifanya unasimamia misingi ya Hiphop huku unazidi kutumbukia kwenye umaskini ni upuuzi mtupu.
 
Only strong survive , fitina kwenye mziki ni janbo la kawaida , nikuuliza hakuna mwanamuziki yoyote bado yupo kwenye Game ambaye alikuwa na bifu na luge , fela nk?
Ni kweli, only the strong survive. Kina Ngwair et al walishindwa kuhimili depression wakawa mateja na mauti yakawakuta. Chanzo ni mambo hayahaya kuwa unafanya kazi sana, kipaji kipo na hutoki.

Wapo waliohimili mabifu na kina Fela mpaka leo wapo wakifanya muziki, na wapo waliokubali terms za magodfather na mpaka sasa wanaendelea. Hata hawa Tamaduni muzik bado wapo kwenye game licha ya mabifu na hao magodfather ila ndio hivyo sasa hakuna kutoboa. Unakuwa underground deile

Nyimbo ya Babu Talent ina miaka 6 youtube ila ina viewers laki 2..unaona kabisa uwiano haupo. Kuna mtu anaitwa Kalighraph Jones namba zake zinasomeka balaa, anajitapa mpaka kwa wanaijeria.. ni kwamba anabadilika badilika na anaendana na wakati. Sometimes ubishi unakwamisha mambo.


GEMU NI GUMU
Nabadilikia humu humu - Lord Eyez
 
Magodfather hawakwepeki na wapo karibu kwenye kila biashara. Kuna mfanyabiashara alikuwa yupo vizuri sasa siku moja ma-godfather wakampa mchongo na kumwambia chao kitakuwa kiasi gani. Hela ilipolipwa akataka kuwapunja. Wazee wakamwambia bora chukua tu zote endapo utataka kwenda tofauti. Yule jamaa kweli akala zote mwenyewe. Wale mafaza wakawa wametulia kama hakuna kinachoendelea. After 2 years jamaa kajikuta jela kwa kesi ya uhujumu uchumi huku bank accounts zote zikiwa freezed na biashara kufungwa. Ni kwamba lazima ukubali watu wale na wewe ule.
 
Dah noma sana mkuu.

Hapa ndio niliposema kuwa inabidi wana wabadili mentality, wafanye muziki kibiashara. Ukifanya biashara wewe unachoangalia ni faida, hutajali tena style au nini..kama vile wanavyofanya weusi, utaimba ili uuze. Tupac anasema, "Everybody Rap, we dont rap, we rap to make money"
Msikilize hapa dakika 1:08

Kwa hiyo wana wanatakiwa wabadilike waache kukaza, wakae na magodfather wafanye biashara. Ni kama ishu za maridhiano za CCM na Chadema,now wanapongezana na picha kwenye mabango, mambo yanaenda😃😃
 
Imagine leo 2pac akifufuka akasikiliza rapper Snoop Dog anaimba Sensual seduction? 😀😀
 
Wafanye MARIDHIANO NA MA GOD FATHER WA HUU MZIKI ukitaka kula lazma uliwe na pia waimbe Mambo ya mapenz wajiingize kwenye SHOWBIZ,,mfano Nikki mbishi akae chini na msanii binti bongo movie mmoja ampe hela kiasi waact wapenz then penz linanoga humohumo anatoa ngoma ,,hivi hawamuonagi mdgo wao mondi harmonize
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…