Talanta yako ni ipi?

TAECOLTD

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
1,051
1,835
Kinachowaangusha wengi katika ulimwengu huu ni kutotambua wewe ni nani, kila mwanadamu anazaliwa na kipawa ambacho kimejificha hivyo jukumu lako ni kutafuta na kukitambua.

Pale utakapotambua kipawa chako ndipo mwanzo wa mafanikio yako, kuna idadi kubwa ya watu wamekufa na kuzikwa na vipawa vyao ambavyo bado hawajavitumia duniani.

Pia kuna idadi kubwa ya watu wanatembelea vipawa vya watu na ndio sababu kila mara huanguka na kutofikia malengo yao sababu hufanya sababu mwingine alifanya akafanikiwa sana.

Mtu huyo mwaka juzi aliingia kuimba ili awe kama msanii mkubwa huko akabuma, mwaka jana akaingia kuigiza ili awe kama fulani napo ikabuma, mwaka huu akaamua kuwa mwandishi pia ikabuma, usishangae mtu huyo mwakani akawa jambazi.

Maandiko yanatuambia kuhusu talanta namna zilivyogawiwa, kuna wale wanatumia talanta zao vyema nao huongezewa talanta nyingine lakini yule ambae haitambui talanta yake huchukuliwa na kupewa mtu mwingine.

Usishangae kukuta mtu anaweza kuimba, anaweza kuigiza, anaweza kuandika, anaweza kucheza na vyombo vyote vya sanaa jua aliitambua talanta yake akaifanyia kazi na talanta zake zikaongezwa maradufu.

Sasa wewe leo unakurupuka kutaka kuwa kama fulani je umejiridhisha kwamba hicho ndio kipawa ambacho umezaliwa nacho? Kazi ni juu yako hakikisha mwaka huu usiishe pasipo kutambua kipawa chako ndugu yangu kipawa chako ndio mafanikio yako hivyo pasipo hivyo utaishia kuruka ruka na mwisho kukata tamaa kuhisi umelogwa au una laana.

Nikutakie siku njema mpendwa!

Mtenga Gerald

TAECO LTD.

============

JINSI YA KUJUA VIPAJI VILIVYOMO NDANI YAKO

Je, unakijua kipaji au vipaji vilivyopo ndani yako?

Moja ya swali ambalo watu wengi huwa wanauliza ni jinsi ya kugundua wao wana vipaji gani.Wakati wa utoto unaweza kuwa ulionesha vipaji vyako ila wazazi au walezi wako hawakuweza kuvitambua.

Ulipoingia kwenye mfumo wa elimu ndio kabisa ulikwenda kuua vipaji vyako. Kwa sababu kwenye mfumo wa elimu haijalishi una vipaji gani, lengo kubwa ni kufaulu. Huenda umemaliza kusoma na hata kazi unafanya ila umegundua ulichosomea au kazi unayofanya huifurahii. Katika wakati kama huu unafikiri umeshapoteza muda wako mwingi na huwezi tena kujua kipaji chako. Hivyo unajilazimisha kukaa kwenye kazi ambayo huifurahii ili tu kusogeza siku.

Hivyo ndivyo maisha yanavyotakiwa kwenda? Unatakiwa kuishi maisha yenye furaha na sio kusukuma siku ziende. Haijalishi umri wako umekwenda kiasi gani au umekaa kwenye kazi muda mrefu sana, ukitaka kubadilika hakuna kinachokuzuia. Katika wakati wowote kwenye maisha yako unaweza kubadili uelekeo wa maisha yako kama unaona unakoelekea hakuna matumaini yoyote. Unaweza kuvigundua vipaji vyako hata kama ulishavisahau kabisa au hukupata nafasi ya kuvijua.

KUNA NJIA KUU TATU ZA KUJUA VIPAJI VYAKO, NJIA HIZO NI;

1. Kufanya mambo mengi.
Moja ya njia za kujua vipaji vyako ni kufanya mambo mengi na kujua ni yapi unayafurahia kufanya. Njia hii ni ya kujaribu na kukosea. Katika njia hii unajaribu kufanya mambo tofauti tofauti na katika hayo kuna machache utafurahia kuyafanya. Katika hayo machache utajua vipaji vyako ni nini. Njia hii ndiyo inatumika na watu wengi sana kujua vipaji vyao. Usione aibu kujaribu mambo mapya kwa kuogopa kushindwa. Fanya mambo mengi ambayo hujawahi kuyafanya, jaribu kucheza michezo mbalimbali, jaribu kuimba, jaribu kuandika, jaribu kujifunza kucheza vyombo, pia jaribu kuchora.

Jaribu vitu vingi uwezavyo ili kujua ni kipi unafurahia kufanya. Kwa njia hii itakuchukua muda mrefu kidogo kufikia kile unachopenda kufanya. Usiogope kuhusu muda, maana muda huu ni muhimu kuliko ambao unaendelea kupoteza kwa kufanya kitu ambacho hufurahii.

2. Fikiri kama fedha isingekuwa tatizo.
Kwa asilimia kubwa unafanya unachofanya kwa sababu ya fedha. Unaweza kuwa hufurahii kabisa unachofanya ila kwa vile ndio kinakupatia fedha za kuendesha maisha inakubidi uendelee kukifanya. Habari mbaya kwako ni kwamba huwezi kufanikiwa sana kwenye jambo lolote kama kinachokusukuma kufanya ni fedha. Ili kugundua vipaji vyako na kuacha kutumikia tu fedha jiulize kama fedha isingekuwa tatizo kwako ungefanya shughuli gani?

Yaani kama kila siku ungekuwa na uhakika wa kupata fedha unayohitaji ili kuendesha maisha yako hata kama hufanyi shughuli yoyote, ungetumia muda wako kufanya nini? Hicho kinachokujia kwenye mawazo yako ndio kipaji chako.

3. Ni shughuli au watu gani unawahusudu?
Unaweza kubisha mbele za watu ila unapokuwa mwenyewe kuna watu ukiwaona unavutiwa sana na shughuli wanazofanya. Wakati mwingine ukiona habari yoyote inayohusisha shughuli hiyo unavutiwa kuifuatilia. Shughuli hizi ambazo ukiziangalia unavutiwa kuzifuatilia au wakati mwingine unatamani kuzifanya ndipo kipaji chako kilipo. Unaweza kuwa unavutiwa na vitu fulani kwa muda mrefu ila kwa kuwa hujisikilizi wewe mwenyewe unashindwa kupata kujua vipaji vyako.

Ni muhimu sana kujua kipaji au vipaji vyako ili kuweza kufanikiwa kwenye maisha yako. Ni rahisi kujua vipaji vyako kama kweli utakuwa na nia ya kuvijua. Acha kuteseka kwenye maisha yako kwa kujisukuma kufanya shughuli ambazo huzifurahii hata kidogo. Jua ni vipaji gani unavyo na anza kuviendeleza ili uweze kufurahia maisha yako.
 
Unashauri asiyejua afanye nini atambue talanta yake??
Hiyo ndio kazi yako kuweza kuitambua...hakuna uchawi kwenye hilo... kila kiumbe ana namna yake ya kutambua talanta yake hivyo naweza nikakuambia namna Mimi nikivyotambua talanta yangu lakini ukaijaribu na bado ikabuma hivyo ukaona Mimi ni muongo....
 
Hivyo hivyo hata vyama vina talanta yake, ccm ina talanta yake, CDM nayo pia na CUF pia ndio maana yake!
 
choooche choche talanta yako chocheaaaaaaa
Kinachowaangusha wengi katika ulimwengu huu ni kutotambua wewe ni nani, kila mwanadamu anazaliwa na kipawa ambacho kimejificha hivyo jukumu lako ni kutafuta na kukitambua.

Pale utakapotambua kipawa chako ndipo mwanzo wa mafanikio yako, kuna idadi kubwa ya watu wamekufa na kuzikwa na vipawa vyao ambavyo bado hawajavitumia duniani.

Pia kuna idadi kubwa ya watu wanatembelea vipawa vya watu na ndio sababu kila mara huanguka na kutofikia malengo yao sababu hufanya sababu mwingine alifanya akafanikiwa sana.

Mtu huyo mwaka juzi aliingia kuimba ili awe kama msanii mkubwa huko akabuma, mwaka jana akaingia kuigiza ili awe kama fulani napo ikabuma, mwaka huu akaamua kuwa mwandishi pia ikabuma, usishangae mtu huyo mwakani akawa jambazi.

Maandiko yanatuambia kuhusu talanta namna zilivyogawiwa, kuna wale wanatumia talanta zao vyema nao huongezewa talanta nyingine lakini yule ambae haitambui talanta yake huchukuliwa na kupewa mtu mwingine.

Usishangae kukuta mtu anaweza kuimba, anaweza kuigiza, anaweza kuandika, anaweza kucheza na vyombo vyote vya sanaa jua aliitambua talanta yake akaifanyia kazi na talanta zake zikaongezwa maradufu.

Sasa wewe leo unakurupuka kutaka kuwa kama fulani je umejiridhisha kwamba hicho ndio kipawa ambacho umezaliwa nacho? Kazi ni juu yako hakikisha mwaka huu usiishe pasipo kutambua kipawa chako ndugu yangu kipawa chako ndio mafanikio yako hivyo pasipo hivyo utaishia kuruka ruka na mwisho kukata tamaa kuhisi umelogwa au una laana.

Nikutakie siku njema mpendwa!

Mtenga Gerald

TAECO LTD
 
Hiyo talanta ungeiandika kwa white language (English) wengine sisi hatujui iyo lugha.
 
Mkuu umesema watu wengi uanguka na kutofikia malengo yao kutokana na kutembelea talanta za wengine na kwenye para ya nne umetoa mfano wa mtu ambaye alijaribu kuimba, kuigiza na kuwa mwandishi.

Lakini katika maelezo ya jinsi ya kujua talanta umesema moja ya njia ya kujua talanta au kipaji chako ni kutoona aibu kujaribu mambo tofauti bila kujali kama utafaulu au utashindwa. Naomba ufafanuzi kwani naona kama kuna contradiction hapo kutokana na kwamba kile kitendo cha kujaribu mambo tofauti ni kama kiashiria cha kutembelea talanta za wengine (kwa mujibu wa maelezo ya awali).
 
Sijui English ndio maana nikaandika kwa lugha ya Tanzania...sikuandika ili iwafikie wanaojua English tu, Asante ndugu

Kwa faida ya aliyetaka kujua talanta kwa kiingereza mimi nijuavyo neno hilo talanta au kipaji kwa kiingereza ni talent au flair. Pia neno endowment hutumika.
 
Huko tunapo kwenda,vipaji/talanta zetu,tutazitambua tu.
Zamani ulikuwa unatakiwa usome tu then unapata kazi.
Siku hizi kusoma sio guarantee ya kupata kazi.
Na hata ukipata kazi sio lazima ikuridhishe.
So kuishi kwa talanta/kipaji chako,ndio trend inayokuja sasa hivi.
 
Mkuu umesema watu wengi uanguka na kutofikia malengo yao kutokana na kutembelea talanta za wengine na kwenye para ya nne umetoa mfano wa mtu ambaye alijaribu kuimba, kuigiza na kuwa mwandishi.

Lakini katika maelezo ya jinsi ya kujua talanta umesema moja ya njia ya kujua talanta au kipaji chako ni kutoona aibu kujaribu mambo tofauti bila kujali kama utafaulu au utashindwa. Naomba ufafanuzi kwani naona kama kuna contradiction hapo kutokana na kwamba kile kitendo cha kujaribu mambo tofauti ni kama kiashiria cha kutembelea talanta za wengine (kwa mujibu wa maelezo ya awali).
Mkuu ni wapi nimesema swala la kujaribu mambo mbalimbali kama njia ya mafanikio???? Hakuna sehemu nimecontradict...soma upya na kwa umakini kile nilichoandika ndugu
 
Mkuu umesema watu wengi uanguka na kutofikia malengo yao kutokana na kutembelea talanta za wengine na kwenye para ya nne umetoa mfano wa mtu ambaye alijaribu kuimba, kuigiza na kuwa mwandishi.

Lakini katika maelezo ya jinsi ya kujua talanta umesema moja ya njia ya kujua talanta au kipaji chako ni kutoona aibu kujaribu mambo tofauti bila kujali kama utafaulu au utashindwa. Naomba ufafanuzi kwani naona kama kuna contradiction hapo kutokana na kwamba kile kitendo cha kujaribu mambo tofauti ni kama kiashiria cha kutembelea talanta za wengine (kwa mujibu wa maelezo ya awali).
Okay nimekupata Mkuu hayo ya kujua namna ya kujua vipawa vyako sijaandika Mimi, nimeishia kwenye jina langu kisha TAECO LTD...hayo maelezo ya ziada sueelewi yameingia aje na ni nani kayaongeza
 
Pia niulize kitu. Hizi talanta lazima mtu azitafute au kuna zingine uja tu kwa mtu automatically?

Nauliza hivi kwa sababu kuna watu wengine talanta zao uanza kuonekana tena kwa kasi ya ajabu tangu wakiwa na umri mdogo mfano kwenye umri wa miaka minne na kufanya mambo makubwa kiasi cha kushangaza watu. Watu hao ni wazi kwamba wanakuwa na talanta hizo bila hata kuangaika kuzitafuta kutokana na umri wao kuwa mdogo kwani wanakuwa hawajajitambua.
 
Okay nimekupata Mkuu hayo ya kujua namna ya kujua vipawa vyako sijaandika Mimi, nimeishia kwenye jina langu kisha TAECO LTD...hayo maelezo ya ziada sueelewi yameingia aje na ni nani kayaongeza

Sawa mkuu. Nami nimekupata.
 
Naitaji, Kujenga nyumba na kuongeza kiwango cha Elimu namshukuru mungu niliyopanga niyafanye mwaka 2015 yametimia! Mungu anisaidie nitimize haya mwaka 2016
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom