Talaka sio mzuri kwa malezi ya mtoto

Talaka sio mzuri kwa malezi ya mtoto

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,600
Habarini

Leo napenda kuongelea suala zima la talaka kwa kipindi cha hivi karibuni au siku hizi kinachukuliwa kama fashion yaani mtu anadai talaka ili tu jamii imuone yeye ndio kaacha na sio kaachwa, au mtu ana muacha mkewe ili tu apate nafasi ya kusema mm ndio nimeacha. Bila kuangalia watoto ambao wamebarikiwa kuwapata kuwa wakiacha watoto watakosa malezi ya wazazi wawili kitu ambacho kina mnyima haki mtoto.

Mtoto anapolelewa na baba na mama inakuwa vizuri na ina aminika mtoto huyo anaweza kuwa na malezi mazuri ukitofautisha na watoto ambao wameleewa na mzazi mmoja hii ni tofauti kabisa huyu mtoto anaelelewa na mzazi mmoja anakosa malezi sahihi mfano mtoto amekosea lakini katika kukosea huko kama baba yake angekuwepo au mama yake angekuwepo angeweza kukumea na akaelewa sasa shida inakuja

Sehemu ambapo mama anatakiwa kumkanya mtoto anamkanya baba na sehemu ambapo baba alitakiwa akemeee anakemea mama inaleta shida sana ndugu yangu tupunguze kudai talaka na kutoa kwa malezi bora ya watoto wetu.
 
Umenena vyema. Wengi wanatoa talaka bila kujali kuwa wana jukumu la kuwapa malezi bora watoto alioshiriki kiwaleta duniani.
 
Back
Top Bottom