Takwimu Hizi zinashangaza

Bundewe

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
400
141
Katika uchaguzi wowote, ni jambo la kawaida kuwa na kura chache zinazoharibika, hii inatokana na mambo mengi ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo wa baadhi ya wapiga kura, maelekezo kuwa na utata au hata wapiga kura kupiga "kura za maruhani" kama ilivyotokea miaka ya nyuma huko Pemba.

Takwimu za uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Bariadi Magharibi 2010 hata hivyo zinashangaza ambapo inaonesha kwamba Chenge amepata kura 50,107 = 30%, Isaac Cheyo kura 34,298 = 20% kura zilizoharibika ni 78,171 = 46%. Inawezekanaje kura zilizoharibika kuwa nyingi kiasi hiki? Nyingi kuliko kura alizopata mshindi??? Hii sio namna nyingine ya kuchakachua matokeo.....?

Katika jimbo hilo hilo, kura za urais zilizo haribika ni 3,047 sawa na 3.3%.
 
Ni kweli hizo ni takwimu za ajabu sana. Ila usukumani watu wengi sana hawajui kusoma na kuandika inaweza kua imechangia kuharibika kwa kura.!
 
sasa kw kza urais zihhribike 3pc tu tungetegeme iwe bt 30 na 40 at least
 
Kama usukumani watu hawajui kusoma na kuandika ref. Maswa, Mwanza yote, Geita mbona hazikuharibika?
 
Ni kweli hizo ni takwimu za ajabu sana. Ila usukumani watu wengi sana hawajui kusoma na kuandika inaweza kua imechangia kuharibika kwa kura.!

Huo ndio mtaji ambao CCM wanautumia kuendelea kutawala.
 
Watakwimu wa tume walihitimu mafunzo ya hisabati na takwimu toka chuo cha Ihemi-Iringa. Wehu kweli hao wanatuchefua watalaamu.
 
Kama hawajui kusoma na kuandika,jambo ambalo ni kweli kwa kiasi fulani,why basi waharibu 48% za ubunge,wakati kwenye urais wameharibu 3%? Na kumbukeni wagombea urais walikuwa wengi zaidi kuliko ubunge,hivyo tulitarajia hao wasiojua kusoma wajichanganye zaidi kwenye kura za urais na kuziharibu
 
Kiini macho, hzo takwim ni za kupikwa, wasukuma si wajinga wa kariba hiyo, ushahd angalia kura za urais kwanin asilimia ile ile ya watu wasiojua kusoma na kuandika isjtokeze hapo kwenye urais? Chezea chenge wewe...
 
Katika uchaguzi wowote, ni jambo la kawaida kuwa na kura chache zinazoharibika, hii inatokana na mambo mengi ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo wa baadhi ya wapiga kura, maelekezo kuwa na utata au hata wapiga kura kupiga "kura za maruhani" kama ilivyotokea miaka ya nyuma huko Pemba.

Takwimu za uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Bariadi Magharibi 2010 hata hivyo zinashangaza ambapo inaonesha kwamba Chenge amepata kura 50,107 = 30%, Isaac Cheyo kura 34,298 = 20% kura zilizoharibika ni 78,171 = 46%. Inawezekanaje kura zilizoharibika kuwa nyingi kiasi hiki? Nyingi kuliko kura alizopata mshindi??? Hii sio namna nyingine ya kuchakachua matokeo.....?

Katika jimbo hilo hilo, kura za urais zilizo haribika ni 3,047 sawa na 3.3%.

Chezea Chenge wewe!
 
Back
Top Bottom