Takwimu hizI zinaleta maana kwa CUF na CHADEMA??

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Mwaka huu tunaingia tena kwenye uchaguzi, jee yaliyotokea mwaka 2005 yatatokea tena mwaka huu??

Lengo la TAKWIMU hizi ni kuonyesha ni kwa kiasi gani kwa kila mkoa kati ya watu mia ni wangapi walikipigia chama gani kura kwa nafasi ya urais. Kwa mfano kati ya watu mia (100) kwenye mkoa wa Iringa, watu 94 waliipigia kura CCM, watu 4 wakaipigia chadema na mtu mmoja akaipigia CUF.


Hapa maana yake ni kuwa mkoa wa Iringa unaongoza kitaifa kwa asilimia kwa kuipa kura CCM. Wakati CCM ilipata kura nyingi kutoka mwanza,kura 713,088 CUF zake ni 216,700 kutoka mkoa wa Dar es salaam na CHADEMA ni kura 98,072 kutoka Mkoa wa Kilimanjaro. CCM ilipata kura chache kabisa kwenye mkoa wa Kaskazini Pemba, kura 7,777 wakati CUF ilipata kura 4,776 kwenye mkoa wa Iringa nayo CHADEMA ikaambulia kura 128 huko kwenye mkoa wa Kusini Unguja.


Ukichambua kiasilimia. Asilimia kubwa kwa CCM ni kutoka mkoa wa Iringa, asilimia 94.20, CUF ni kutoka mkoa wa Kaskazini Pemba aslimia 85.66 na CHADEMA ni kutoka mkoa wa Kilimanjaro asilimia 20.61. Uchache wa asilimia kwa CCM umetoka kwenye mkoa wa Kaskazini Pemba asilimia 12.03 kwa CUF ni kutoka mkoa wa Arusha asilimia 1.21 na CHADEMA ni asilimia 0.20 kutoka Kaskazini Pemba.


Twakimu hizi zitatusaidia kujua chama gani kilipata asilimia nyingi kwenye mkoa gani na mkoa upi ulitoa kura nyingi kwa chama gani. Inawezekana ikawa ndiyo msingi wa kujifanyia tathimini kama ule wito wetu wa kutaka kumuondoa Kikwete mkakati wake tuuanzaje.


Hapa hakuna haja ya kushambuliana bali tuzitumie takwimu hizi kujifanyia tathimini kwamba tangu baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 tumefanya kazi gani ya kupunguza asilimia na wingi wa kura inazopata CCM kwenye mikoa yetu. Bila kuwa na mikakati yakinifu ya kupunguza asilimia na wingi wa kura inazopata CCM hakuna njia ya mkato ya kuiondoa madarakani.


MLINGANISHO WA % ZA KURA ZA WAGOMBEA URAIS KWA CCM, CUF, CHADEMA MWAKA 2005
NO
Region
CCM
Region
CUF
Region
CHADEMA
1
Iringa
472,612 (94.20%)
North Pemba
55,360 (85.66%)
Kilimanjaro
98,072 (20.61%)
2
Singida
319,870 (90.90%)
South Pemba
49,791 (77.05%)
Arusha
67,618 (15.34%)
3
Rukwa
259,421 (89.94%)
M.Magharibi
46,832 (31.16%)
Mara
56,493 (12.42%)
4
Mbeya
568,458 (88.87%)
Pwani
83,821 (24.37%)
Manyara
36,834 (10.71%)
5
S.Unguja
47,545 (88.58%)
Lindi
66.775 (22.90%)
Kigoma
41,100 (9.48%)
6
Dodoma
497,792 (87.47%)
N. Unguja
14,968 (22.81%)
Kagera
49,867 (7.35%)
7
Manyara
321,026 (86.35%)
Dar' salaam
216,700(22.79%)
Mwanza
59,142 (6.58%)
8
Morogoro
548,837 (85.83%)
Tabora
95,047 (21.02%)
Shinyanga
54,631 (6.55%)
9
Tanga
272.504 (84.77%)
Mtwara
73,667 (16, 64%)
Dar'Salaam
52,979 (5.57%)
10
Ruvuma
304,611 (84.57%)
Shinyanga
131,526(15.76%)
Rukwa
13,035 (4.51%)
11
Kagera
572,498 (84.43%)
Tanga
67,260 (12.43%)
Ruvuma
13,973 (3.88%)
12
Arusha
361,237 (81.96%)
Mwanza
106,558(11.86%)
Mbeya
24,524 (3.83%)
13
Kigoma
345,298 (79.61%)
S. Unguja
5,717 (10.65%)
Singida
12,977 (3.69%)
14
Mwanza
713,088 (79.37%)
Ruvuma
36,426 (10.11%)
Iringa
17,691 (3.53%)
15
Mtwara
350,117 (79.09%)
Morogoro
60,051 (9.39%)
Dodoma
15,777 (2.81%)
16
Mara
354,613 (77.95%)
Dodoma
444,971 (8.00%)
Morogoro
15,668 (2.45%)
17
Tabora
345,549 (75.98%)
Kigoma
34,410 (7.93%)
Mtwara
9,145 (2.07%)
18
N.Unguja
49,566 (75.53%)
Mara
31,533 (6.93%)
Tabora
7,618 (1.68%)
19
Shinyanga
621,975 (74.54%)
Kagera
39,710 (5.86%)
Pwani
5,642 (1.64%)
20
Lindi
215,717 (73.99%)
Singida
14,705 (4.18%)
Lindi
4,644 (1.59%)
21
Pwani
251,068 (72.93%)
Mbeya
18,382 (2.87%)
Tanga
7,225 (1.30%)
22
Kilimanjaro
344,539 (72. 24%)
Rukwa
7,207 (2.50%)
M.Magharibi
507 (0.34%)
23
Dar ‘salaam
671,134 (70.59%)
Iringa
4,776 (0.95%)
N.Unguja
206 (0.31%)
24
M.Magharibi
102,256 (68.03%)
Manyara
7,171 (1.93%)
S.Unguja
128 (0.24%)
25
S.Pemba
12,844 (21.15%)
Kilimanjaro
9,437 (1.88%)
S.Pemba
130(0.21%)
26
N.Pemba
7,777 (12.03%)
Arusha
5,324 (1.21%)
N.Pemba
130 (0.20%)

Total
9,123,952 (80.28%)

1,327,125 (11.68%)

668,756 (5.88%)



Hakuna mkoa wowote ambao CHADEMA iliongoza kwa kupata asilimia nyingi ya kura kuliko vyama vingine. Hata Kilimanjaro ambako ndiko ilikopata asilimia nyingi ya kura, CCM ndiyo iliongoza kwa kupata asilimia nyigi zaidi ya kura (72.24%) kuliko CHADEMA (20.61%) na CUF (1.88%)


WINGI WA KURA KWA KILA MGOMBEA URAIS KWA CCM, CUF NA CHADEMA 2005
CCM CUF CHADEMA
1
Mwanza
713,088

Dar es salaam
216,700

Kilimanjaro
98,072
2
Dar es Salaam
671,134
Shinyanga
131,526
Arusha
67,618
3
Shinyanga
621,975
Mwanza
106,558
Mwanza
59,142
4
Kagera
572,498
Tabora
95,047
Mara
56,493
5
Mbeya
568,458
Pwani
83,821
Shinyanga
54,631
6
Morogoro
548,847
Mtwara
73,667
Dar es salaam
52,979
7
Dodoma
491,792
Tanga
69,260
Kagera
49,867
8
Iringa
472,612
Lindi
66,775
Kigoma
41,100
9
Tanga
472,504
Morogoro
60,051
Manyara
39,834
10
Arusha
361,237
North Pemba
55,360
Mbeya
24,524
11
Mara
354,613
M. Magharibi
46,832
Iringa
17,691
12
Mtwara
350,117
South Pemba
46,791
Dodoma
15,777
13
Kigoma
345,298
Dodoma
44,971
Morogoro
15,668
14
Kilimanjaro
344,539
Kagera
39,710
Ruvuma
13,973
15
Tabora
343,549
Ruvuma
36,426
Rukwa
13,035
16
Manyara
321,026
Kigoma
34,410
Singida
12,977
17
Singida
319,526
Mara
31,533
Mtwara
9,145
18
Ruvuma
304,611
Mbeya
18,382
Tabora
7,618
19
Rukwa
259,421
North Unguja
14,968
Tanga
7,225
20
Pwani
251,068
Singida
14,705
Pwani
5,642
21
Lindi
215,717
Kilimanjaro
9,437
Lindi
4,644
22
Mjini Magharibi
102,256
Rukwa
7,207
Mjini Magharibi
507
23
North Unguja
49,566
Manyara
7,171
North Unguja
206
24
South Unguja
47,545
South Unguja
5,717
South Pemba
130
25
South Pemba
12,844
Arusha
5,324
North Pemba
130
26
North Pemba
7,777
Iringa
4,776
South Unguja
128

JUMLA
9,123,952

1,327,125

668,756

Hapa Rangi zinatusaidia kuona kwa mfano nafasi ya Mwanza kwenye CUF na CHADEMA na nafasi ya Dar es salaam kwa CCM na CHADEMA na pia nafasi ya Kilimanjaro kwa CCM na CUF.
Nawasilisha!!
 
Takwimu zilizopikwa na tume ya uchaguzi (inayomilikiwa na ccm) hazina ukweli wowote ule
 
CUF ni Chama cha Waislamu/magaidi, mnapojadili mambo ya takwimu msilisahau hili! Wenye kukasirika mtakasirika mpaka machozi yatawatoka lakini ukweli unabaki pale pale!
 
Back
Top Bottom