mamayoyo1
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 1,011
- 1,019
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaotamani kugombea uongozi bila kufuata taratibu na sheria.
Tahadhari hiyo ilitolewa jana na kamanda wa TAKUKURU wa wilaya ya Nachingewa, Buddy Ebrahim kwenye kongamano la maadili,lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya mkoa wa Lindi.
Buddy alisema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unaotatajiwa kufanyika mwakani, kuna baadhi ya watu wanaotamani kuomba uongozi kupitia chaguzi hizo wameanza kuwalaghai wapiga kura kwa kuwahaidi na kuwapa fedha na vitu.
Alisema vitendo hivyo havikubaliki. Kwasababu nikosa kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007. Kwahiyo serikali kwa kutumia vyombo vyake, ikiwemo taasisi hiyo vinawafuatilia kwa karibu wanaotajwa kutenda vitendo hivyo.
"Watu wanaofanya vitendo hivyo na wanaotamani kufanya, watambue kwamba serikali inawaona na inawajua. Kwasababu inamacho mengi kuliko matundu ya chandarua,"alisisitiza Buddy.
Kamanda huyo aliwaasa wapiga kura, kwamba kabla ya kuwapigia kura wagombea waanze kujiuliza kama wanaotaka kuwachagua wanataka uongozi ili wawe watumishi wao au kwa ajili ya masilahi yao binafsi. Huku akiwasihi wawakatae watu wanaotumika na kuwakumbatia watu wenye vipato na uchumi mkubwa ili wachaguliwe kuwa viongozi.
Hata hivyo kamanda huyo alibainisha kwamba uwezo wa kiuchumi hakuzuii mtu kuchaguliwa na kuwa kiongozi. Hata hivyo baadhi yao wanatumia uwezo huo kuwanunua wapiga kura. Jambo ambalo linaweza kusababisha madhara makubwa iwapo watachaguliwa na kuwa viongozi.
Alisema watu wenye uchu wa uongozi kiasi cha kutumia fedha na mali, iwapo watapewa uongozi wanaweza kutengeneza sheria zitakozolinda masilahi yao. Kwahiyo watakwamisha shuguli za maendeleo ya wananchi.