esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 555
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Kilimanjaro, inawashikilia watu 11 wakiwamo watumishi 10 wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mjini Moshi.
Wanashikiliwa kwa tuhuma za kukabidhi vitambulisho vya taifa mikononi mwa matapeli. Pia, inamshikilia Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kiusa iliyopo Manispaa ya Moshi, Hemed Shaban kwa tuhuma za kudai 100,000 ili atoe kitambulisho cha taifa kwa mhusika.
Mkuu wa Takukuru mkoani hapa, Holle Makungu alisema osi yake ilipokea taarifa kutoka kwa raia mwema Aprili 9, mwaka huu, kuhusu kuombwa fedha ili apewe kitambulisho chake, ndipo walipoandaa mtego wa kumnasa mtuhumiwa. “Aprili 9, mwaka huu tulipokea taarifa kutoka kwa raia mwema (jina limehifadhiwa) akidai alitakiwa kutoa shilingi 100,000 ili apewe kitambulisho chake, hii ni kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Takukuru Namba 1 ya 2007,” alisema.
Makungu alisema mtuhumiwa alikamatwa baada ya kujitambulisha kuwa ni osa wa Nida na baada ya upekuzi alikutwa na vitambulisho vingine vya wananchi, ambavyo bado havijawakia walengwa. Alisema watumishi wengine wa Nida, wanaendelea kuhojiwa ili kubainisha uhusiano na ushirikiano walionao na mtuhumiwa Shabani na sababu za kumpatia vitambulisho vinavyotakiwa kukabidhiwa walengwa.
“Uchunguzi zaidi unaendelea ili kuwabaini watumishi hao na jinsi wanavyoshirikiana na mtuhumiwa huyu, kitendo hiki ni kinyume na Kifungu cha 31 cha Sheria ya Takukuru Namba 11 ya mwaka 2007,” alisema. Makungu alisema uchunguzi utakapokamilika, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Aliwatahadharisha wananchi kwamba vitambulisho vya taifa, vinatolewa na Nida bila gharama yoyote