TAKUKURU yaikalia Kooni EGMA, ni kuhusu Malipo hewa ya USD millioni 6

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Kampuni ya Enterprise Growth Market Adviser (EGMA) inakabiliwa na kesi ya hati fungani, inayohusu malipo ya USD 6,000,000 ililipwa kwa madai ya kuisaidia Tanzania kupata mkopo wa USD 600,000,000. TAKUKURU imegundua kwamba fedha hizo 6,000,000 zilitakatishwa na watumishi wa Umma wasio waaminifu.

Imeahidi kuwashughulikia wote bila kujali hadhi wala nafasi ya mtu.
IMG-20160126-WA0008.jpg
 
Hili saga likitakuwa ni kipimo cha makali ya "Takukuru Mpya"..Kazi kwako ndugu Valentino..umepewa nafasi ya kuthibitisha kama unaiweza spidi ya JPM
 
Yes ni kipimo kikubwa cha awamu ya tano, maana balozi sefue alishamtaja mwenye kampuni na wote waliochukua pesa shida sijui why hawakamatwi wakati kila kitu kipo wazi na uchunguzi wazungu washafanya, au ndio mambo ya uchunguzi juu ya uchunguzi?
 
Fratern Mboya ametangulia mbele ya haki, aliyebaki ni Harry Kitilya ambaye ndio atalibeba hili gunia la misumali!! Mustapha Mkullo hawezi kuchomoka hapa kwani inasemekana nae alichukua mgao kutoka kwenye hili fungu!! Kitilya akibanwa vizuri atataja jamaa waliokula nao bingo
 
Kesi zote hizi cha mtoto kwa ESCROW
Kama Escrow hamna kesi basi na hizi ni sinema tu
 
Namuona kitilya huyo kwa mbali anakutana na kasheshe kazi anayo wakati wanaiba walidhani mchezo washitakiwe tu.
 
Back
Top Bottom